Kuwekeza Tanzania - TPN specifics.

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,017
7,220
Shukrani za dhati kwa TPN -hasahasa Mwenyekiti wake mzalendo Mtsimbe- kwa kujitahidi kubuni njia mbalimbali za kuwezeshana katika uwekezaji. Leo naomba niirudishe tena TPN hapa JF huku nikiwa na swali.

Je TPN specifically ina program gani za kuwawezesha watanzania (especially waishio nje- diaspora) kuwekeza Tanzania? Nitatoa mfano.

Lets say kuna Mtanzania yuko Michigan ana USD 35,000 na anataka kuja kuanzisha mradi wa duka Tanzania. Atahitaji taarifa za kodi, utaratibu wa kutoa mizigo bandarini au airport, sehemu ambazo zingefaa zaidi kwa aina hiyo ya biashara, jinsi ya kupata mahali pa kufungua hilo duka, products zinazopendwa zaidi etc... Je mtu wa aina hii akiwasiliana na TPN ategemee ushirikiano wa kiwango gani?

Natangaliza shukrani kwa niaba ya wajasiriamali in the making...
 
Mzalendo ZeMarcopolo,

Asante sana kwa swali la msingi.

Kwanza napenda kukujulisha kuwa TPN ilijiunda tena upya katika AGM yake iliyofanyika August 2008 baada ya kupata mawazo mengi ya kuboresha ikiwepo JF.

Kutokana na hilo, tuko katika hatua ya mwisho ya kutengeneza Website ambayo pamoja na mambo mengine, itakuwa na Business Information na hata Potential Partners na Business Profiles zao ambazo pia zitaainisha masuala ya Partnership na Capital.

Nia yetu ni kuona pia walio na Capital kutoka nje yaani Tanzanian Diaspora nao wanaweza kuweka katika Website hiyo mahitaji yao ya Miradi au Biashara. So, it will be some sort of MATCHING. TPN will be there to guarantee both parties na kujenga kuaminiana.

Hata hivyo kwa sasa hivi kama kuna mtu ana shida na information zozote na ni Mwanachama wa TPN bado tunaweza tukamsaidia na kumpatia hata sources ya information mbalimbali.

Moja ya sababu kwa nini TPN ina-plan kuwa na Diaspora Summit ni pamoja na kufikia maelewano kati ya Wadau wa Ndani na Diaspora ni nini hasa kifanyike katika kuboresha Investment kwa Tanzania Diaspora ina a "Practical Sense".

Tafadhali nijulishe kama majibu yangu yanajitosheleza.
 
asante kwa maelezo ya kutosheleza. Maelezo yako yamenifanya niibue swali lingi. Je kwa nini TPN pamoja na kuwa na kurugenzi au idara nyingi lakini inachukua muda mrefu sana kutake-off. Mpaka sasa kwenye website yake inaonekana TPN ni NGO inayoandaa makongamano tu. Sasa wengi wetu tungetaka kujiunga na body inayowawezesha watu kuinvest practically ikiendana sambamba na makongamano kwa ajili ya nadharia lakini msisitizo uwe kwenye vitendo. Wasiwasi wangu hasa ni kwamba diaspora itakuwa slow kwenye kujiunga na NGO ambayo action zake zote ni makongamano. Mimi niko tayari kujiunga na TPN (kama nilivyoahidi siku za nyuma)lakini najiuliza mwezi mmoja baada ya kujiunga nitanufaika vipi, miezi miwili, mwaka mmoja , miwili, mitatu baada ya kujiunga TPN itaniwezesha vipi kuwa katika better position??? Hivi ni vitu vya msingi kuviweka bayana ili diaspora iwe tayari kujiunga.
Kwenye website haielezewi bayana ada ya kujiunga ni sh. ngapi, ila kama sikosei nilipata ambiwa kuwa membership fee ni sh. laki moja kwa mwaka. Sasa kwenye list ya wanachama nimeona majina 505, which means that kila mwaka TPN inakusanya sh. milini 50 kama ada za wanachama. Hiki kiasi kinatosha kuiwezesha TPN kuwa na activity inayoonekana kila siku.
Baada ya kupitia majina ya members wake tathmini yangu ni kwamba TPN ina potential kubwa kuliko jinsi inavyoperfom.
 
Mzalendo, asante kwa maswali na hoja zako za ziada. Nitazifafanua kama ifuatavyo.

Maelezo yako yamenifanya niibue swali lingi. Je kwa nini TPN pamoja na kuwa na kurugenzi au idara nyingi lakini inachukua muda mrefu sana kutake-off. Mpaka sasa kwenye website yake inaonekana TPN ni NGO inayoandaa makongamano tu. Sasa wengi wetu tungetaka kujiunga na body inayowawezesha watu kuinvest practically ikiendana sambamba na makongamano kwa ajili ya nadharia lakini msisitizo uwe kwenye vitendo. Wasiwasi wangu hasa ni kwamba diaspora itakuwa slow kwenye kujiunga na NGO ambayo action zake zote ni makongamano.
.

Kama ulifuatilia mijadala yaTPN, utagundua kuwa TPN ilianza rasmi July 2007. Na napenda nikujulishe kuwa kuna mafanikio mengi sana ambayo tayari yamepatikana. Mafanikio hayo si ya Ngonjera au ya kisiasa bali ya vitendo. Tafadhali rejea:

https://www.jamiiforums.com/matanga...-karibuni-tanzania-professionals-network.html

na

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nzanians-diaspora-summit-december-2009-a.html

Kwa maelezo ya kina na mafanikio kisha nijulishe kama bado utahitaji maelezo ya ziada.

Mimi niko tayari kujiunga na TPN (kama nilivyoahidi siku za nyuma) lakini najiuliza mwezi mmoja baada ya kujiunga nitanufaika vipi, miezi miwili, mwaka mmoja , miwili, mitatu baada ya kujiunga TPN itaniwezesha vipi kuwa katika better position??? Hivi ni vitu vya msingi kuviweka bayana ili diaspora iwe tayari kujiunga.

Unayozungumza ni ya kimsingi na ndiyo Changamoto kubwa. Wengi wanataka kujiunga ili wafaidi moja kwa moja. Tuliopo sasa tunawajibika kujenga mazingira hayo kwa TPN kujijengea uwezo katika maeneo mablimbali ya msingi. Wachache tuna mawazo ya "What Can We Do For Our Country" and not the opposite way. Hata hivyo napenda kukufahamisha kuwa tayari tuna members wengi ambao ni Diaspora na kama nilivyodokeza tayari tuna Chapter UK na USA, unaweza kuwasiliana nami nikakupatia contacts kama uko maeneo hayo.

So Mkuu, be specific na nina uhakika TPN itakusaidia. Research tuliyoifanya huko nyuma inaonyesha kuwa matatizo yetu ya Kujiwezesha Kiuchumi ni ya namna tatu:
- Maarifa ya Ujasiliamali - TPN inatoa Elimu
- Mitaji - TPN ina model ya kuwaunganisha members wapate mitaji na kuwapa access ya Mikopo. Pia TPN sasa ina Fund.
- Masoko - TPN ni mtandao na katika huo mtandao tunautumia pia kama Market Place na Networking (Its like Jamatini thing but much better).

Kama una mawazo ya kuboresha zaidi, tunakukaribisha tuendelee kushauriana.

Kwenye website haielezewi bayana ada ya kujiunga ni sh. ngapi, ila kama sikosei nilipata ambiwa kuwa membership fee ni sh. laki moja kwa mwaka. Sasa kwenye list ya wanachama nimeona majina 505, which means that kila mwaka TPN inakusanya sh. milini 50 kama ada za wanachama. Hiki kiasi kinatosha kuiwezesha TPN kuwa na activity inayoonekana kila siku.
Baada ya kupitia majina ya members wake tathmini yangu ni kwamba TPN ina potential kubwa kuliko jinsi inavyoperfom.

Kama nilivyodokeza, TPN website inatengenezwa upya na itakuwa na Information zote muhimu. Tunaomba uvumilie kidogo tu.

Kuhusu fees, zilifanyiwa marekebisho kwenye last AGM. Registration ni TZS 50,000 na Monthly Subscription ni TZS 10,000. Kinadharia TPN ina members na Wapenzi zaidi ya Million 5. Hata hivyo walioko katika list kwa sasa ni zaidi ya 1000.

Tunakubaliana na wewe kuwa TPN ina potential kubwa sana na hilo tayari tunaliona kutoka katika yanayotokea sasa hivi. Tungependa kukua kwa uhakika na kujenga mfumo wa mageuzi halisi ya kiuchumi kuanzia kwa mtu binafsi. Bado kazi ni kubwa lakini naamini kwa dhamira na utashi tulionao, tutafika.
 
Mz Mtsimbe,
nakumbuka TPN ilianzishwa summer 2007 na nimekuwa nikiifuatilia kwa karibu sana, kwa sababu maalum.
Labda niulize kwa aina nyingine ambayo itakuwa more specific.
Je TPN mpaka sasa imefanya makusanyo ya sh. ngapi? Ina kiasi gani cha pesa kwenye akaunti? Na je katika bajeti ya mwaka 2008 ni nyanja gani zilipewa kipaumbele katika bajeti? Na zimetumia kiasi gani cha pesa ( percentage wise)?

Kwanini nauliza sana kuhusu pesa!!?

Iwapo TPN ina wanachama 1000 ambao wanatoa sh. 10,000 kila mwezi. Ina maanisha inakusanya sh. milioni 10 kila mwezi. Kwa mwaka ni sh. milioni 120. Ukijumlisha na ada za mwaka ambazo ni sh. 50,000 zinazotolewa na kila mwanachama (mil. 50 in total) inakuwa sh. milioni 170 kwa mwaka. Hizi ni pesa toka kwa wanachama tu. Kuna donations kama zile za fundrising iloyofanywa na TPN kwa kushirikiana na Mh. Sitta.

Nadhani utakubaliana na mimi kuwa NGO inayokusanya sh. 170 milioni inapaswa kuonekana kwenye macho ya watanzania, just by activities zake. Je TPN ina permanent office? Ziko wapi? Maana kiasi hivho kinatosha bila wasiwasi kuwa na ofisi na kuajiri waendesha NGO at least watatu full time.

Je TPN ina gari lililonunuliwa kwa jina la TPN?

Mbona kila inapozungumzwa TPN tunakuona wewe tu? Wako wapi Dr. Vera Ngowi, Janet Mbene na timu zao?

Hapa ninachokifanya ni kujaribu kuitafuta TPN physically out of paper works, web pages and conference halls.

Mpaka sasa nimefurahishwa sana na jinsi ulivyo willing kuelezea masuala ya yote ya TPN kwa undani wake, kitu kinachodhihirisha kuwa unastahili kuiongoza TPN.
 
Mz. Mtsimbe

Nakumbuka kuwa seminars mnazoandaa huwa zina ada. Na hata kuingia kwenye AGM kulikuwa na ada ya sh. elfu 5. Kwa hiyo TPN ina mapate kedekede, yanatumika vipi mapato haya?

By the way, sijaipitia katiba ya PTN kwa undani ila conventional wisdom ni kwamba AGM haipaswi kuwa na entrance fee kwa sababu inatakiwa kuwa ni haki ya mwanachama. Nadhani hii sh. 5000 ni bora ingeitwa mchango maalum, kwa maana ya kwamba uwe nayo usiwe nayo utaruhusiwa kuhudhuria AGM...
 
Mzalendo, naona topic sasa imebadilika tofauti na title yake na hata swali la msingi ulilouliza "Je TPN specifically ina program gani za kuwawezesha watanzania (especially waishio nje- diaspora) kuwekeza Tanzania? Nitatoa mfano".

Hata hivyo usijali nitajitahidi nikujibu. Sina uhakika kama kwa uhakika ulifanya marejeo katika threads nilizokupa hapo juu, maana mengi unayouliza hapa yalishaulizwa na kujibiwa. Nevertheless let me clarify the issues.

Nakumbuka TPN ilianzishwa summer 2007 na nimekuwa nikiifuatilia kwa karibu sana, kwa sababu maalum.
Labda niulize kwa aina nyingine ambayo itakuwa more specific.
Je TPN mpaka sasa imefanya makusanyo ya sh. ngapi? Ina kiasi gani cha pesa kwenye akaunti? Na je katika bajeti ya mwaka 2008 ni nyanja gani zilipewa kipaumbele katika bajeti? Na zimetumia kiasi gani cha pesa ( percentage wise)?

Kwanini nauliza sana kuhusu pesa!!?

Iwapo TPN ina wanachama 1000 ambao wanatoa sh. 10,000 kila mwezi. Ina maanisha inakusanya sh. milioni 10 kila mwezi. Kwa mwaka ni sh. milioni 120. Ukijumlisha na ada za mwaka ambazo ni sh. 50,000 zinazotolewa na kila mwanachama (mil. 50 in total) inakuwa sh. milioni 170 kwa mwaka. Hizi ni pesa toka kwa wanachama tu. Kuna donations kama zile za fundrising iloyofanywa na TPN kwa kushirikiana na Mh. Sitta.

Naambatanisha report ya utendaji ya TPN kwa mwaka mzima. Ni matumaini yangu utapata muda wa kupitia na kupata majibu ya maswali hayo. Kama wewe ni member unaweza pia kuomba Audited Report ya Mahesabu kwa ajili ya kuipitia. Nikufahamishe tu kuwa TPN inaendeshwa kwa uwazi na ukweli wa hali ya juu.

Nadhani utakubaliana na mimi kuwa NGO inayokusanya sh. 170 milioni inapaswa kuonekana kwenye macho ya watanzania, just by activities zake. Je TPN ina permanent office? Ziko wapi? Maana kiasi hivho kinatosha bila wasiwasi kuwa na ofisi na kuajiri waendesha NGO at least watatu full time.

Maswali hayo yamejibiwa katika report (attached) na hata katika Threads nilizoku-refer hapo juu. Kwa sasa TPN ina Staff wawili wa kudumu, Office Administrator na msaidizi wake.

Je TPN ina gari lililonunuliwa kwa jina la TPN?

NO. Not for now as it is not a priority. Kwa nini unafikiri tununue gari tu Mzalendo? Tushauriane.

Mbona kila inapozungumzwa TPN tunakuona wewe tu? Wako wapi Dr. Vera Ngowi, Janet Mbene na timu zao?

Swali hili pia lilishajibiwa. Please find time to go through the threads so that we dont waste time going through same issues again and again.

Hapa JF, mimi nimejaindikisha kwa jina langu halisi. Niliwakaribisha wana JF TPN na najaribu pia kutoa taarifa mbalimbali. TPN Office inayo namna yake ya kuwasiliana kupitia mikutano, magazeti, Radio, TV nk. Kama wewe ni mfuatiliaji utagundua kuwa kuna maofisa wa namna mbalimbali wanaohusika. So, hapa JF mimi ni member kama ulivyo wewe at the same time natumia fursa hii kuwasilisha issues mbalimbali ambazo nadhani wana JF ni vema wakijua.

Hapa ninachokifanya ni kujaribu kuitafuta TPN physically out of paper works, web pages and conference halls.

Report niliyoambatanisha inajibu maswali yako.

Mpaka sasa nimefurahishwa sana na jinsi ulivyo willing kuelezea masuala ya yote ya TPN kwa undani wake, kitu kinachodhihirisha kuwa unastahili kuiongoza TPN.

Asante mkuu, tuendelee kusaidiana.
 
Attachments

  • TPN Executive Committee Operations Report 2007-2008.pdf
    84.2 KB · Views: 128
Nakumbuka kuwa seminars mnazoandaa huwa zina ada. Na hata kuingia kwenye AGM kulikuwa na ada ya sh. elfu 5. Kwa hiyo TPN ina mapate kedekede, yanatumika vipi mapato haya?

Mkuu, Si wanachama wote wa TPN walio-active hasa katika ulipaji. Kiburi ambacho TPN tunacho ni kuwa tusingependa kujiendesha kwa misaada ya kuombaomba hata pale ambapo hapa umuhimu. Kwa hiyo yunajitegemea wenyewe katika mambo mengi sana na njia mojawapo ni kuchangia katika mikutano hiyo ambayo hata hivyo michango hiyo wakati mwingine bado ni midogo kuliko matumizi halisi. Nadhani umepata picha kutoka katika report.

By the way, sijaipitia katiba ya PTN kwa undani ila conventional wisdom ni kwamba AGM haipaswi kuwa na entrance fee kwa sababu inatakiwa kuwa ni haki ya mwanachama. Nadhani hii sh. 5000 ni bora ingeitwa mchango maalum, kwa maana ya kwamba uwe nayo usiwe nayo utaruhusiwa kuhudhuria AGM...

Mzalendo pitia katiba ya TPN kutoka Website yetu under RESOURCES. Unakaribishwa sana TPN na kama ni makini katika mambo ya pesa na ubunifu, huenda ukatufaa ukigombea uongozi katika mambo ya fedha.

Kama utakuwa na maswali zaidi karibu TPN. Ila ni busara pia ukajiridhisha na majibu mengi ya kina yaliyotolewa huko nyuma kabla hujauliza ili kuepuka repeatition.
 
Back
Top Bottom