Kuweka Huawei na Tecno kwenye kundi moja kiubora ni sahihi?

Chief-Mkwawa kuna jamaa yangu anatumia tecno boom j8, tangu jana ananisumbua kuhusu simu yake kujiwasha Data yenyewe,nimemuelekeza ku hard reset lakini bado tatizo lipo palepale mpaka hivi sasa kantumia ina picha imejiweka apn za kichina. Nb. Nilishawahi kumshauri asinunue tecno wala simu yoyote ya Mediatek akashindwa kunielewa sababu ya mwonekano wa simu
P2nu7o5.jpg
 
Wengine mnaiga tu mkumbo! Nitajie programs ambazo unazipata kwenye Samsung hazipo tecno.? Mnachonunua ni brand name ya Samsung na sio ubora wa simu.Mnatembea na charger battery mbovu.Tecno specification zake zipo vizuri

Well said mkuu, yaani ukisoma baadhi ya maoni ya ajabu unabaki unashangaa - programs zote ambazo ziko customised for android OS zipo karibu kwa simu zote regardless ya brand ya simu na apps nyingine unaweza kuinstall muda wowote ukitaka kupitia playstore na sites nyingine, haya nambo ya kutisha watu mpaka wajisikie kwamba kama awakununua a branded phone basi wameliwa - wateja wangapi wanaitaji hyperfast phone, kwani wanataka kuzitumia kufanya mahesabu ya Quatum Physics, cold fussion au exotic games who needs these stuff !!

Mambo mengi (specs) wanazo zisema humu ni vitu vinavyo fanyika ndani kwa ndani ya processor speed ya processor inapunguzwa sana inapo tolewa nje kusafirishwa kwenye data na address buses, mara zote default za speed za memory ndiyo zina dictate kila kitu regardless front side bus speed.

Wateja wote wa simu wabazitumia kwa ajili ya voice comm na data, simu yenyewe
hata iwe na speed gani italazimishwa kufuata speed ya teknolojia inayo tumiwa na service provider - modem ya simu inafanya handshake na ya provider na kukubaliana speed hipi itumike, yote hayo yanafanyika automatically. Muwe wakweli kwamba speed kubwa inahitajika katika masuala ya video games and the like hapo hapo kwenye simu lakini linapokuja suala la kuwasiliana na watu wengine kwa ya voice au data via air systems za provider ndiyo zina dictate throuput ya nawasiliano siyo simu yako. Mambo mengi watu wanayo yaleta humu wanaya copy kutoja kwenye IT review sites ambazo kiuharisia ziko pale kibiashara zaidi kuliko kiufundi ndio maana napataga wakati mgumu kukubaliana nao.
 
Mi natumia tecno zipo mbili! Phantom z mini na tecno C9 nazipenda wala sijutii kuwa nazo.Wengi mnafuata mkumbo Wa watu.Km unajua zifafanue technically kwann Samsung ni bora kuliko tecno
Mkuu, nakuomba mtafute mtu anayetumia Samsung Galaxy J7 ambayo ina the same specifics na na hiyo simu yako tecno C9 ambazo utofauti ni processor tu tecno C9 inatumia mediatek wakati samsung galaxy J7 inatumia Qualcomm /exynos na tofauti nyingine ipo kwenye battery ambapo galaxy J7 imeiacha C9 kwa 300mAh kisha naomba ufanye comparison ya hivi vitu kwenye hizo simu
1. Camera quality
2. Ubora wa display (kipi ni kioo angavu zaidi)
3. Multitasking on app load (fanya kufungua apps kama 25 hivi kwenye kila simu kisha bonyeza button ya multitasking anza kuload hizo app moja baada ya nyingine uone ni simu gani inatumia mwingi kuload)
4. Download games mbili kati ya hizi kisha angalia ni simu ipo inaload faster hizo game (GTA Vice City, Grand auto theft San Andreas, need for speed most wanted, modern combat 5)
Ukishafanya comparison kwa kutumia hizo factors 4 hapo juu, majibu itakayopata usije kutoa ushahidi hapa ila baki nayo kisha utakuwa imepata uhalisia sahihi wa simu ipi ni bora pamoja na kuwa the same specs, na kama unaishi Arusha nipm nikutafute tufanye comparison kwa kutumia simu yangu, natumia HTC One A9 ambayo ina specs kama ya hiyo simu yako C9 ukiwa umenizidi battery kwa 900mAh na tunatofautiana processor yangu ni Qualcomm na yako ni Mediatek
 
Chief-Mkwawa kuna jamaa yangu anatumia tecno boom j8, tangu jana ananisumbua kuhusu simu yake kujiwasha Data yenyewe,nimemuelekeza ku hard reset lakini bado tatizo lipo palepale mpaka hivi sasa kantumia ina picha imejiweka apn za kichina. Nb. Nilishawahi kumshauri asinunue tecno wala simu yoyote ya Mediatek akashindwa kunielewa sababu ya mwonekano wa simu
P2nu7o5.jpg
Nahisi kachijanganya tu kwenye setting..maaana mimi natumia hiyo simu na haijawai fanya mambo kama hayo
 
download dolphin emulator cheza rom yoyote ya nintendo wii halafu tuonyeshe hapa.

na pia android ni bure naweza run app zake popote pale, unapotoa hela kununua simu hulipii apps na software sababu zile ni bure unalipia hardware yaani display, camera, battery, processor, gpu, modem etc
Hawa watu wanajionesha jinsi gani weupe vichwani na ni wagumu kweli kweli kushaurika wakiamini wanaonewa
 
Chief-Mkwawa kuna jamaa yangu anatumia tecno boom j8, tangu jana ananisumbua kuhusu simu yake kujiwasha Data yenyewe,nimemuelekeza ku hard reset lakini bado tatizo lipo palepale mpaka hivi sasa kantumia ina picha imejiweka apn za kichina. Nb. Nilishawahi kumshauri asinunue tecno wala simu yoyote ya Mediatek akashindwa kunielewa sababu ya mwonekano wa simu
P2nu7o5.jpg
mkuu huyo ni malware na hapo amesharoot simu kisiri siri na kujieka kama system app na proof ni hapo ulipo hard reset, ukireset simu inafuta kila kitu kasoro system files tu.

na hilo ni moja ya tatizo la mediatek na simu za kichina, ukisearch humu jukwaani kuna mamia ya thread ya simu za Tecno zinajiwasha data.

hizo ni dalili za kwanza data ikijiwasha itaanza kujidownload apps na kudisplay matangazo na kudownload picha na video za ngono.

kuwatoa hapo ni kuflash simu na kuanza upya au uwe na box lenye ant virus kama miracle halafu uzime simu uconect simu na pc yenye box halafu uwascan
 
Naona screen yake haipo sensitive sana na kamera sjmi nzuri sana especially ya mbele....
zamani wakati naanza kuchagua simu nilikuwa najua kioo kizuri ni kikubwa, simu ikiwa na kioo kikubwa hata kioo chake itakuwa unatouch kwa usahihi na kuandika haitakuwa shida.

siku moja nikatype kwenye iphone 4, japo screen yake ilikuwa ni ndogo ila nilikuwa natype kwa usahihi kuliko simu zenye screen kubwa.

baadae nikaja kusoma kuwa latency ya touch ndio kila kitu, ile response toka mguso hadi kuipeleka kwenye simu jinsi inavyokuwa ndogo ndio jinsi kioo kinavyokuwa vizuri na hukosei.



hapo ni simu flagship lakini zipo ambazo latency inazidi 100ms kwenye hizi Tecno zetu sitashangaa latency ikiwa hata 500ms
 
zamani wakati naanza kuchagua simu nilikuwa najua kioo kizuri ni kikubwa, simu ikiwa na kioo kikubwa hata kioo chake itakuwa unatouch kwa usahihi na kuandika haitakuwa shida.

siku moja nikatype kwenye iphone 4, japo screen yake ilikuwa ni ndogo ila nilikuwa natype kwa usahihi kuliko simu zenye screen kubwa.

baadae nikaja kusoma kuwa
Kuwa nini mkuu?

Nilikua natumia sony xperia z2, nilikua sikosei kosei maneno ila hii tecno c9 ambayo wanasema ni toleo jipya nakosea sana na naona haipo sensitive sana....
 
Simu yenye ubora kwa sasa IPhone, inafutia Sonny, BlackBerry, Microsoft, Samsung, huawei, ........ zinafuatia hizo zingine. Kwa cm OG tu
 
Kuwa nini mkuu?

Nilikua natumia sony xperia z2, nilikua sikosei kosei maneno ila hii tecno c9 ambayo wanasema ni toleo jipya nakosea sana na naona haipo sensitive sana....
sorry post ilijituma ikiwa nusu, cheki tena nimei edit.

issue ni latency toka unapogusa kioo hadi kupelekwa mahala husika. latency ikiwa kubwa na wewe unagusa mara kwa mara ndo inaleta huo mkanganyiko.
 
Sipati picha ndio ingelipuka Tecno badala ya Sumsung
Wenye tecno tungehamishwa nchi kwa kelele za wenye sumsung
 
Naomba ni wajibu ki IT nkitumia diploma nlioko nayo,,

Kwanza kabisa mnabishana bila kujua tifauti zenu
Kuna wengne wanapenda brand name wengne wanaprefer specifications,

Kwamfano:
Unaeza ukakuta
*tecno Ina 2GB RAM,internal memory16,battery 3000 MAh Android version ya 6.0 (marshmallow)

Na ukakuta
*Samsung Ina 1GB RAM,internal memory 8,b battery 2500 mAh Na Android version ya 4.1.2 (jelly bean)
(Hapo juu nmezungumzia smartphone znazotumia Android OS Na sio Mac OS kama apple)

Kulingana Na tofaut za hapo juu, wale wapenda majina atafuata Samsung bila kujali uwezo wa battery kuhifadhi moto au ukubwa wa memory ya ndani au speed..

Kulingana Na maelezo yahizo smartphone mbili hapo juu tecno ndio Bora kwa performance lakin inakua underrated kutokana Na brand name .. Na kwa ukubwa huo wa Samsung utakuta inauzwa ghali sana kuliko teno ilioizid ukubwa kwasabu ya jina..


Pia kumbuken tecno inauzwa Africa tuu Na sio ulaya,,,,(ulaya tecno Hamna ila ni sim nzur sana)
Ukiongelea performance sijui unapata mtazamo gani,
Umesahau kuna aina za RAM

Umesahau SOc...hao tecno sindo wenye soc vimeo?


Umesahau hardware, s2 ya 2011 hadi leo ipo mtaan,wapi H6 wapi p5

Umesahau displays

Umesahau GpU

Umesahau camera sensor

Optimization

Memory used

Mbona kuna vitu vingi vya kuzingatia and still unasema wewe ni IT man
 
Hii wallpaper niliipiga na simu hii hii ,tecno unatoa kweli picha ya quality hii na yenye blur kwa zile zisizolengwa /zilizo mbali !?

e92f448a1d538e27dde019f6a64710b5.jpg
202bc4e3c6c52bfdcce31caa70a491c3.jpg
9c35f92f93f04e76f9ba543d335713e5.jpg



Mwenye tecno na wewe sababu zote ni android hebu nawe fungua multi pages kama hizo ,hiyo samsung galaxy s6
 
Back
Top Bottom