Kuwe na ukomo wa Ubunge Tanzania

Ubunge mwisho miaka 10, as it's for the president!

Ninasajesti mtz yoyote anayetaka kugombea ubunge, afanye hivyo, akishinda mara moja abakiwe na mara yake moja kama ilivyo kwa rais kuwa na term mbili tu.

NAFIKIRI HII ITASAIDIA sana watz kuangalia nini mtu amefanya kwa miaka hiyo kumi, na kama ameboronga, basi akamatwe.

Nasema hivi, kwasababu nahukia sana kuona mbunge tangu nimezaliwa miaka ya sabini hadi leo nina miaka 30 yeye bado tu ni mbunge, akiboronga bado tu anachaguliwa, wananikera.

Mnasemaje wajameni?

This is undemocratic and may limit some very capable individuals whose contribution is much needed.If there is a need to kick an MP out of parliament, the people have that call.

The presidential post is very different in nature, potency and scope, and therefore the limit is applicable accordingly. One can work in the executive arm of government for years and conclude his service as president (Mkapa, Mwinyi and Kikwete did this) but one cannot say the same about the legislature.If all MPs are going to be rookies or sophomoric, who will show the other the bathroom door?

Rather than petitioning for a myriad of draconian measures, it would be far better to organize the people in some grassroot civic education groups so they can vote out incompetents by the ballot box.

It is quite possible that the constituent is quite satisfied with a "statesman MP" a la Ted Kennedy. It is quite necessary to have some time tested leadership in parliament, one can hardly attain this within two terms.An MP should not be defined by the length of his service, but by her contribution.
 
Juzi nilimsikia waziri mkuu(mtoto wa mkulima) kuwa 2015 hatagombea tena .na akapendekeza kuwe na ukomo wa kuwania ubunge yaani miaka 15.upande wangu naona imekaa njema vipi wakuu wa jf mnalionaje hilo?
 
Ubunge mwisho miaka 10, as it's for the president!

Ninasajesti mtz yoyote anayetaka kugombea ubunge, afanye hivyo, akishinda mara moja abakiwe na mara yake moja kama ilivyo kwa rais kuwa na term mbili tu.

NAFIKIRI HII ITASAIDIA sana watz kuangalia nini mtu amefanya kwa miaka hiyo kumi, na kama ameboronga, basi akamatwe.

Nasema hivi, kwasababu nahukia sana kuona mbunge tangu nimezaliwa miaka ya sabini hadi leo nina miaka 30 yeye bado tu ni mbunge, akiboronga bado tu anachaguliwa, wananikera.

Mnasemaje wajameni?
inabidi uwachukie wananchi wanaomchagua na si yeye. kwani huwa anagombea peke yake? si kuna wagombea wengine pia?
 
Napendekeza Ubunge nao ungekuwa na term limit kama Urais. However, nadhani ubunge ungepewa term 3 – kwamba mtu awe anaruhusiwa kuwa mbunge kwa term tatu tu mfululizo (miaka 15). Baada ya hapo awe harusiwi kuwa Mbunge for 5 years then awe anaruhusiwa kugombea tena baada ya kusita kuwa mbunge kwa miaka 5. Nadhani taifa letu lina wasomi/watu wengi ambao nao wanahitaji na wanahitajika kuleta michango, mawazo, mawazo tofauti, fikra mbadala, na utaalamu wao majimboni na bungeni. Nadhani miaka 15 inatosha kwa mtu kulitumikia jimbo lake, wananchi na Bunge letu tukufu na kwamba ni muhimu kuwapisha wengine nao waweze kutumikia jimbo, wananchi na Bunge. Tafakari...............!
 
GreatThinkers,

Mwanzo tulihitaji mawazo mapya, watanzania wameanza kuwa wapya kimtazamo.
Nimefanya utafiti watanzania wengi wamechoshwa na mawazo mgando.
Nawapa Big up sana tuu
Mzee mwakijiji,
Rev Kishoka,
(Late);Regia Mtema
Mawazo yenu nami yamenisaidia sana.

Tatizo watu wameng'ang'ania dola na hawataki kushindwa chaguzi.
Tumejionea sote namna wanavyopiga usingizi mjengoni.
Kwa macho yangu nimemuona Wasira anasinzia/analala tuuu
Nimemuona hata Six nae kauchapa
Lakini je, kweli watu hawa waliohudumu toka enzi za Mwalimu je wanafit ktk ulimwengu wa leo.

Nashauri kuwe na ukomo wa ubunge
Nawasilisha
 
Ila kuna wengine ni potential sana ebu fikiria watu kama kina dr slaa wawe 50 bungeni halafu wote tuwawekee limit si nchi watauza waliobaki bungeni
 
Tatizo sio ukomo ,kuna nchi za masultani huko uarabuni ,au tuseme falme za kiarabu na wengi wetu humu kama ni wafanya biashara au watembezi au wapekuzi mnaweza kabisa kuziona nchi hizo zilivyo na maendeleo.

Hivi mnajua ni WaTz wangapi walikuwa wameajiriwa katika sehemu mbalimbali huko,rafiki yangu alikuwa ni mwananjeshi katika jeshi la Arab Emirates ni Mtz kwa maana alikuwa na pasi yake ya kiTz aliniambia kuwa walikuwemo wengi sana wakifanya kazi katika Jeshi mpaka pale 1991 wakati wa vita vya kumuondoa ,Sadam ,ambapo wengi wa wanajeshi wanaomiliki passport za nje ,waliamuliwa kuachichwa kazi ili kulifanya jeshi hilo liwe na wazalendo watupu.

Nikirudi kwenye mada ,hivyo hao wafalme na familia zao wengi wao wamo kwenye kushika hatamu kwa muda mrefu sana ,wengine wakihitimisha kwa kufikiliwa na kifo ,nchi zao na uongozi wao haukusababisha shida wala ubadhirifu wenye kuathiri wananchi wao ,seuze shida za maji na umeme katika nchi hizo ni hadithi zisizo aminika. Hivyo kuwepo katika uongozi kwa muda mrefu isiwe sababu ya wengine kupata shida na kulalamika.

Nilionalo kwa upande wangu ni ukosefu wa ufuatiliaji wa sheria kwa wahusika ,kwa maana hapa Tanzania sheria hazifuatwi ipasavyo ,tunaoneana haya na aibu ,kumbuka hapo awali tulisema tusimuonee haya mvivu au mzururaji ,tukamsahau asietimiza wajibu wake.

Rushwa imetawala nchi ,kiasi ya kwamba imefika wakati kuzuilika ni vigumu sana ,hakuna takururu wala polisi wote hawa ni viranja wa kula rushwa au naongopea ? Rushwa haizuiliki tena hapa Tanzania nini kifanyike ?

Hizi posho za wabunge ni rushwa inayotolewa huko bungeni na mishahara minono ,wakati wao ni waajiriwa wa wananchi kama wengine ,wananchi ndio wa kuamua wabunge walipwe mshahara wa kiasi gani badala ya kupangiwa na serikali ,kusema kweli mshahara wa wabunge unavuka mipaka ,ukiangalia wengine toka waingie bungeni hawajachangia wala kusema kitu ,zaidi ya kwenda na kurudi ,hata asipochaguliwa baada ya miaka mitano ana hasara gani ?? Hivyo ukomo wa kuwepo kwake bungeni hauna maana ikiwa mshahara ni mkubwa hata kwa mwaka mmoja. Na wakimaliza miaka mitano wanapewa jackport.

Nafikiri angalizo ni kwa kiwango cha mshahara wanachopewa ukilinganishwa na wafanya kazi wengine wa serikali na si muda wa wao kuwa wabunge.
 
Ila kuna wengine ni potential sana ebu fikiria watu kama kina dr slaa wawe 50 bungeni halafu wote tuwawekee limit si nchi watauza waliobaki bungeni

Short and clear.
King Kong II-Thanks, basi wanaosinzia au wanaohudhuria bila kuchangia hoja yoyote nao wafikiriwe
 
Kuwe na sera/sheria-anayesinzia au kutohudhuria au kama hachangii hoja mjengoni apigwe chini
 
Katiba ya JMT imeweka ukomo Wa urais!ni wakati Sasa katiba ikafanyiwa marekebisho au katiba mpya itakayotengenezwa iweke ukomo Wa ubunge!!Haina maana wabunge wasiwe na ukomo Wa kuwa wabunge wakati rais Wa nchi yeye amewekewa ukomo Wa miaka kumi tu!!Wabunge hawa wana uwezo wakumchafulia rais kwa sababu wao wanajua wataendelea kuwepo bungeni maana hawana ukomo Wa kuwa hivyo!!lingine ni kuwa unakuta ndani ya jimbo kuna mbunge mzigo mtoa rushwa anendelea kuwa mbunge bila kikomo huku ndani ya jimbo lake hakuna maendeleo!!
 
Hayooo yoote yamo kwenye katiba pendekezwa ikipita ile katiba yote yako addressesd!!! Issue tupiganie katiba mpya!!!!
 
Ubunge mwisho miaka 10, as it's for the president!

Ninasajesti mtz yoyote anayetaka kugombea ubunge, afanye hivyo, akishinda mara moja abakiwe na mara yake moja kama ilivyo kwa rais kuwa na term mbili tu.

NAFIKIRI HII ITASAIDIA sana watz kuangalia nini mtu amefanya kwa miaka hiyo kumi, na kama ameboronga, basi akamatwe.

Nasema hivi, kwasababu nahukia sana kuona mbunge tangu nimezaliwa miaka ya sabini hadi leo nina miaka 30 yeye bado tu ni mbunge, akiboronga bado tu anachaguliwa, wananikera.

Mnasemaje wajameni?
Umewaza visuri sana. Hebu endelea kuwaza na mengine. TUMAINI JEMA HILI. Ukomo ukiwepo kwa Wabunge, nchi itapata maendeleo sana hii. Watu wataacha siasa na watakuwa wanafanya kazi katika majimbo yao. UKOMO KWA WABUNGE MUHIMU
 
Moderator tafadhali unganisha mawazo ambayo yametolewa mara kadhaa kwa hoja hii. Tutupie na katika Katiba mpya, hili lisimamiwe. Tunataka nchi iendelee hii na watu watafanya kazi, wataacha siasa.
 
Na ukomo wa uenyekiti wa chama uwepo pia; mfano huko Chadema mtu anaweza kua party chairman milele.
 
Hoja ya wabunge kuwa na ukomo ilikuwepo kwenye rasimu ya pili ya jaji Warioba lkn ilipingwa vikali na wajumbe wa BMK. Naomba hii hoja iwekwe kwennye katiba.

Tumechoka kuwaona baadhi ya watu wakijigeuza wafalme katika majimbo yao. Mf. Vangimembe Lukuvi, Mtemi Chenge, n.k.
 
labda kingine ni vyama vya upinzani kususia chaguzi zote
Mkuu unamfahamu Dovutwa? Unamfahamu Peter Mziray? Unamfahamu Augustine Lyatonga Mrema? Hawa ni wenyeviti wa vyama vya upinzani vyenye unasaba na chama tawala.

Hawa kamwe hawawezi kususia uchaguzi. Na wasiposusia jumuiya za kimataifa zitaona kuna ushiriki wa vyama vya upinzqni ktk chaguzi.
 
Uko sawa kabisa kususia chaguzi haihusu kitu kuna vyama vya upinzani uchwara vitashiriki na Bunge lote kuwa chini ya chama cha wahuni, wauaji na mafisadi.

Back
Top Bottom