Kuwasomba Wananchi Kwenye Mikutano toka Mbali, Je! Hotuba ni Kwa Wageni au Wenyeji?

M.L.

Senior Member
Feb 11, 2012
185
119
Imekuwa ni kawaida kwa CCM-Mafisadi na CUF kusomba wananchi toka maeneo ya mbali kwenda kufanywa hadhira kwenye mikutano ya vyama hivyo ugenini; mfano, jana CCM ilisomba wananchi kadhaa toka Dodoma mjini kwenda Msalato kwenye uzinduzi wa kampeni za udiwani kata ya Msalato; vile vile CUF ilisomba watu toka Dar na Tanga kwenda Arusha kutengeneza hadhira katika mikutano yao V4C. Je! lengo hasa ni nini na matokeo yake ni yepi?

Kwa hali kama hii, kuna haja gani ya kuwasafirisha watu ili ukawahutubie ugenini? Si ungewahutubia pale pale walipo ili kuokoa fedha za wanachama na chama chao. AU ni ufisadi kila mahali?
 
Hii kasumba tumeitaka wenyewe waTZ. Tunaamini kuwa mfano mzuri wa chama chenye wafuasi wengi ni picha za wengi wa watu. Ndio maana CUF na CCM wanatumia hiyo style kuficha aibu. Ila ukweli ni kwamba hiyo style inaficha aibu na ni nzuri. We ona jinsi gani CUF walivyojipa moyo na V4C yao ingawa kule arusha walibeba watu kutoka dar!?. Siasa ni mchezo mchafu wa kitoto.
 
Wa kuwalaumu ni wanachi wenyewe wanaopenda kusombwa na Malori kama wanyama! TZ ya leo still kuna watu hawajui thamani ya utu wao! wamekuja duniani by Default ndio hao wanakubaliwa kusombwa kama wanyama. pia vyama vyenye tabia hiyo vikome mara mara moja.
 
Wanapenda kufanya maonyesho yasiyo na maana badala ya kuelimisha wananchi wa eneo husika. Mchezo huu ccm wanaupenda sana kutumia!
 
Hotuba inabaki kuwa ni kwa wenyeji ingawa wageni nao hupata,tatizo hapa si hotuba tatizo ni kusudio husika la mkutano,haiingii akilini kusomba watu toka sehemu moja kwenda nyingine eti kujaza watu,huu ni Ufisadi na ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.
 
cuf-crowd.jpg
Mbali ya hilo pia picha huchakachuliwa.
Hapa majjid mjengwa anatuambia kuwa picha hii ni cuf arusha majuzi.
Lakini ukiangalia hata matangazo ya Voda yanayoonekana pembeni barabarani ni ya mwaka 2010.
 
Hiyo inaitwa domo klasi - yaani tumbo kwanza! Iweje mtu mwenye akili timamu ukubali kubebwa kwenye lori kama mfu ili mradi tu umepewa faranga. Yaani kunakujidharirisha kwingine kunapitiliza mipaka.
Wanahitaji elimu ya uraia, na wajibu huo ni wangu na wako. Tuzidi kuwaelimisha ili wajue haki zao za msingi. Yote hayo yatakuwa na mwisho wake.
 
Inanufaisha wote wenyeji na wageni. Tena inafaa sana maana hata wale ambao wasingefika kwenye mikutano na kupata ujumbe wakishaona malori tu wanatamani kupanda na hatimaye wanaenda kupewa elimu ya uraia bure. Nawapongeza sana waliochukua uamuzi huu mzuri.
 
Inanufaisha wote wenyeji na wageni. Tena inafaa sana maana hata wale ambao wasingefika kwenye mikutano na kupata ujumbe wakishaona malori tu wanatamani kupanda na hatimaye wanaenda kupewa elimu ya uraia bure. Nawapongeza sana waliochukua uamuzi huu mzuri.

Kaka, nimependa style yako ya kufiri!
 
Back
Top Bottom