Tatizo la Muwasho Sehemu za Siri: Chanzo, Matibabu na Namna ya Kujikinga

Asanteni kwa hii mada, ni muhimu kwa afya ya watu. Asilimia kubwa ya maisha ya watu inategemea mapenzi.

Mapenzi ni muhimu sana kwa sababu inaongeza value of life, hata hivyo uaminifu na kuwa na mapenzi salama. Ukitaka kuwa na raha epuka usaliti katika mapenzi, kuwa mwaminifu na mkweli.

Baada ya hapo nina maswali yafuatayo:
- Nini umuhimu wa Condom? Nitajie faida za kutumia condom katika mapenzi?
- Kuna hasara au madhara gani katika kutumia condom kwa muda mrefu? mfano kufanya mapenzi kwa condom mfululizo kwa miezi mitatu
- Je mtu akiambukizwa VVU itapita muda gani hadi Damu yake ikipimwa ionekane kuwa ina VVU
- Je Msichana mwenye VVU akitoa mimba, afya yake itadhoofika?
- Mwanamke akioga kawaida bila kupitisha kidole kwenye uchi/**** (samahani jamani) yake atapata madhara baada ya muda gani?
 
shem nakula vitu classic bana.....hana STI yoyote maana ningejua si unajua kwa jinsia ya pili haichukui muda kujitokeza.....kawaona madktari kapewa vidonge kuweka huko chini bado nasikilizia kama muwasho utaendelea...aaaah shem kuna sehemu kuuza mechi hakukwepeki....

1. Kwenye magonjwa na maambukizi yanayohusiana na kujamiiana (Sexually Transmitted Infection or Disease) hakuna cha u classic ndugu!Tena unayewaona ni "classic" pengine ndo hao hao wenye maambukizi zaidi.Uliza madaktari watakuambia.

2. Huwezi kusema kwa uhakika kuwa mtu anayo au hana STI bila kufanya vipimo. Kuna tofauti ndogo baina ya STI ambayo ni uambukizo unaotokana na kujamiiana na STD ambayo ni magonjwa ya zinaa. Hicho alicho nacho huyo dada kinaweza kutokana na au kisitokane na zinaa/kujamiiana kama walivyokwisha elezea wengine. Wanawake wengi hupatikana na tatizo la mwasho katika nyakati mbalimbali za mzunguko wao wa mwezi na pia kutokana na mabadiliko mbalimbali katika sehemu za siri (matumizi ya sabuni, matumizi ya dawa za anti biotics vyote huingiliana na PH ya sehemu hizo).

Wengine hupata kuvu ( fungus) - candida au hata trichomonas vaginalis - hii hupatikana pia kwa njia ya zinaa/kujamiiana. So dont be too sure kuwa siyo STD/STI.Maambukizi haya ni tofauti na Syphilis, gonorhoea, chlamydia etc ambayo yatakupa dalili za moja kwa moja na kukufanya ujue au kuamnini kuwa huyo bibie anayo STI/STD.

3. Ni vema basi huyo mwana dada atafute ushauri wa kitabibu hasa kama tatizo linajirudiarudia badala ya kujitibu kwa kununua dawa kama daktarin, nystatin, etc ambazo huweza kupatikana kwa urahisi kwenye maduka ya dawa. Pia epuka kujamiiana kipindi cha kutibu hilo tatizo na muwe na mazoea ya kutumia condom.
 
Masa mm naona tiba yake hapo nikuachana kabisa na mademu wa bei chee wale wa Mwananyamala, buguruni, TMK n.k
 
Kuwashwa kwa mwanamke sehemu za ukeni kunatokana na yafuatayo:

1. Kuna baadhi ya wanawake wakitumia aina flani za condom huwashwa kutokana nayale mafuta mafuta ya condom.

2. Wengine wanapo kwenda haja ndogo hasa kwenye hivi vyoo vyetu vya jumuia utakuta ktk choo cha wanawake kuna ndoo ya maji na kopo, lile kopo halisafishwi vizuri na choo pia hakioshi vizuri na madawa ya usafi hivyo basi ule uchafu wa choo na kopo la maji ambapo huwa kuna vijidudu vya fungus huzaliana kwa wingi ndipo hapo mwanamke huambukizwa.

3. Kwenda haja ndogo na umalizapo kunawa na maji husababisha unyevyu nyevu ktk chupi.

4. Baadhi ya wanawake hufuwa chupi zao na kuzianika ndani, na kuzivaa bila kupiga pasi chupi huwa na unyevunyevu hazikauki ipasavyo.
 
Kuna members wamekuja wakisumbuliwa na medical conditions, ushauri umetelewa juu ya nini wafanye ili kuweka afya yao sawa.Cha kusikitisha ni kwamba hakuna feedback yoyote toka kwa members hao. Iwapo wangekuja kusema njia ipi imewasaidia au haijawasaidia, ingeweza kuwasaidia wengine ambao wana conditions kama hizo au wanaowafahamu wenye conditions kama hizo.

Lile tatizo lilisha kwa mujibu wa mhusika alikwenda hosp akapewa dawa fulani akatumia baada ya siku kadhaa liakwa limeisha, aliambiwa limetokana na maji aliokuwa akitumia. Nafikiri mnajua maji yetu ya Dar.

Pia kitu kignine nilimshauri ni kujiswafi kwa saana(pamoja ni msafi sana na anazingatia kanuni zote za afya) na atumie maji kila akienda hata haja ndogo. Toilet paper nazo hazifai zinaongeza fungus kwa wakina mama.
 
Habari waungwana,

Mie nina tatizo limenitokea hivi karibuni. Ninapofanya mapenzi na mke wangu,baada ya shahawa kutoka nasikia muwasho ndani ya mrija wa kukojolea.

Muwasho huo uendelea kwa siku mbili kisha upotea, niikifanya tena unarudi. Sasa sijui hilo ni tatizo gani.

Naomba ushauri wenu tafadhali.

kisonono.jpg
muwasho.jpeg
gonorea.jpeg


===================

Magonjwa (STI's)

Ni magonjwa yakuambukizana kupitia kufanya ngono - Haya kwa kimombo yanaitwa STI au Sexually Transmitted Infections. Mambukizo hutokea pale maji maji ya mwili kama vile mate, damu, manii majimaji ya ukeni nk ya mtu ambae tayari ameambukizwa, yatatangamana na ya mtu ambae hajaambukizwa.

Hii mara nyingi hufanyika wakati wa ngono ya kuingiliana kimwili, au ya kunyonyana sehemu za siri. Baadhi ya majonjwa hayo (lakini sio yote) yanatibika, lakini yasipotibiwa yanaweza kusababisha madhara ya kudumu.

Kumbuka maambukizi ya ukimwi na virusi vya HIV pia mara nyingi hufanyika kupitia kufanya ngono. Na kumbuka pia bado hakuna tiba ya Ukimwi, wala chanjo dhidi ya virusi vya HIV.

Kwa sasa hivi kinga bora dhidi ya magonjwa ya zinaa, ni kutofanya ngono kabisa au kutumia kondom kwa kufuata maagizo kikamilifu, na kufanya ngono iliyosalama.

Nitajua vipi kama nimeambukizwa magonjwa yanayoathiri afya ya uzazi?

Wanawake:


attachment.php


Maji maji au ute unaotoka kwenye uke ni sawa kabisa, lakini wanawake wanapaswa kutafuta usaidizi wa kimatibabu wakigundua lolote kati ya yafuatayo:-

Majimaji ya ukeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida na yenye rangi tofauti na wingi kuliko ilivyo kawaida.

Maumivu au kusikia kama unachomeka au mwasho wakati wa kwenda haja ndogo.

Maumivu na mwasho katika maeneo ya uke.

Maumivu ya ukeni wakati wa kufanya ngono.

Vidonda na malengelenge katika eneo la uke.

Kumbuka, baadhi ya maambukizi huenda yasiwe na dalili. Hii haimaanishi kwamba huwezi kumwambukiza mpenzi wako, au kwamba hayawezi kukudhuru kiafya.

Kama una wasi wasi, ni vyema kuchunguzwa na daktari haraka iwezekanavyo, ama katika kliniki.

Wanaume:

attachment.php
attachment.php



Mwanaume anapaswa kuenda kutafuta ushauri wa daktari kama atajipata na dalili zifuatazo:

Majimaji kutoka uumeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida, au yakiwa mengi.

Kuhisi mwasho ndani ya uume, wakati na baada tu ya kwenda haja ndogo

Vijidonda na sugu ama malengelenge juu au katika sehemu za kiume.

Vipele au uvimbe katika sehemu za siri.

Kwa mara nyingine tena, kumbuka maambukizo mengine kama ya virusi vya ukimwi yanaweza kuwemo mwilini kimya kimya kwa mda bila dalili zozote kujitokeza.

Unaweza kuwa hutaona dalili yoyote kwanza, lakini haimaanishi kwamba huwezi kuwaambukiza wengine. Kama umefanya mapenzi bila kutumia kinga na una wasi wasi huenda umeambukizwa, nenda ukafanyiwe uchunguzi na daktari.

Magonjwa ya kawaida yanayoambukiza sehemu za siri (viungo vya uzazi)

Cystitis Huu ni uvimbe mgumuHuambukiza kupitia bacteria ambazo huishi chini ya ngozi, eneo la sehemu za siri na hata kwenye utumbo mkubwa.

Dalili:
Dalili kubwa ni maumivu makali wakati wa haja ndogo, na kujisikia kutaka kwenda chooni mara kwa mara. Maumivu hayo yanaweza kuendelea kuwa makali kwa haraka sana.

Huwakumba zaidi wanawake hasa wakati wa hedhi na wakati wa hali fulani nyenginezo kama vile kuwa na uja uzito, au kuugua ugonjwa wa sukari.

Usipotibiwa kwa haraka unaweza kusambaa hadi kwenye figo na kusababisha madhara mabaya zaidi.

Matibabu:
Kunywa maji kwa wingi au vinywaji majimaji kama maji ya matunda (juisi hasa ile ya cranberry yafaa zaidi!) Unapoona tu dalili za kwanza kwanza, juisi hiyo inaweza kusaidia sana.

Hata hivyo ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi na atakupendekezea dawa zinazokufaa.

Thrush: Huu ni ugonjwa wa kuvimba vimba ndani kwa ndani mwilini. Kwa kawaida husababishwa na 'fungus'- kukua kupita kiasi kwa kitu kama hamira.

Ugonjwa huu unaweza kusambazwa kwa njia ya ngono lakini pia unaweza kutokea kutokana na sababu nyingine, kwa mfano kama kuvaa chupi, suruali iliyokubana zaidi, au kama unaugua ugonjwa wa sukari.

Ugonjwa huu unaweza kuwapata wanawake kwa wanaume.

Dalili:
Dalili kubwa kwa wanawake, ni kupata maumivu na kujikuna kwenye mashavu ya upenyo wa uke na sehemu ya kupitishia haja kubwa (mkunduni). Yaani kujihisi mfano wa kuanza vidonda katika eneo la sehemu za siri.

Hali hiyo huandamana na kutokwa na majimaji mazito meupe kutoka ukeni yenye harufu kama hamira. Sehemu hizo huenda zikawa nyekundu zaidi, wanaumenao, huenda wakahisi mwasho kwenye uume, hasa nchani (kichwa cha mboo) na kuhisi kama karaha ya kupata vidonda.

Pia wakati mwingine uume hutokwa na majimaji au ute mzito wa njano .

Matibabu:
Pindi ukigunduliwa ugonjwa wa Thrust hutibika kwa usahisi. Daktari hupendekeza vidonge au krimu maalum ambazo zinapatikana kwa wingi, kwenye maduka ya madawa.

Trichomonas vaginalis kwa kifupi (TV)- Hiki nacho ni kijidudu cha bacteria, kidogo kinachoambukiza kupitia ukeni na kwenye mrija wa kupitishia mkojo.

Dalili:
Dalili za ugonjwa huu ni vigumu kuzigundua hasa kwa wanaume. Dalili kwa mwanamke aliyeambukizwa ni kutokwa na majimaji au ute wa rangi ya kijani manjano hivi, ambao huenda ukawa na harufu kama ya samaki.

Matibabu:
Ugonjwa huu unaweza kutibiwa kwa urahisi, kwa madawa maalam ya kupambana na viini antibiotics. Ili kuepuka kuambukizwa upya, na kusambaa zaidi kwa ugonjwa huu inabidi mpenzio pia nae atibiwe.

Magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono Magonjwa yanayoambukizwa kupitia ngono ni baadhi ya maambukizi yanayotokea mara kwa mara kote ulimwenguni, na huwaathiri watu wa kila rika na asili, wanawake kwa wanaume.

Bora tu wenye kufanya ngono, iwe ya baina ya mke na mume, na wengine wote basi ni vyema kuchukua tahadhari. Njia moja ni kutumia vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi haya.

Kwa mfano kutumia kondom na mpenzio, kila mara mnapofanya ngono, hadi pale nyote wawili mtakapokuwa mna hakika kabisa kwamba hakuna uwezekano wowote wa ninyi wawili kuambukizana magonjwa ya ngono.

Hebu tuangalie orodha hii ya baadhi ya mengine yakuambukuzana kupitia ngono.

Chlamydia - Husababishwa na viini vya bacteria na waweza kuathiri uke, mrija wa kupitisha mkojo, uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.

Dalili:
Kwa wanawake dalili hazionekani kwa urahisi. Ubaya ni kuwa ugonjwa huo unaweza kuathiri fallopian tubes yaani mirija ya kupitia mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye nyumba ya uzazi hivyo basi kusababisha utasa.

Wakati mwengine dalili hii unaweza kuiona - kutokwa na majimaji ya ukeni yasiyo ya kawaida na kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.Kwa wanaume ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitishia mkojo, uzuri ni kwamba dalili huonekana wazi, kama vile uume kutokwa na ute na kusikia maumivu wakati wa kukojoa.

Matibabu:
Ni pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa mkojo au damu. Unapotambuliwa daktari hupendekzeza dawa maalum ya kumeza. Kama umefanya mapenzi hivi karibuni basi yafaa mpenzi huyo aarifiwe ili nae atibiwe pia.

Kisonono (Gonorrhoea)Huu husababishwa pia na bacteria. Unapofanya mapenzi na mtu mwenye kisonono unaweza kuaathiri viungo kama vile uke, uume, sehemu ya haja kubwa na ya haja ndogo, na hata koo au mdomo kama ukifanya mapenzi ya kunyonyana.

attachment.php

kisonono bakteria


Dalili:
Wanawake hutokwa na ute mwingi wa njano au kijani kutoka ukeni na kusikia maumivu wakati wa kukojoa. Kwa wanaume uume uliathirika hutoa ute wa njano au kijani, na kupata maumivu wakati wa kukojoa.

Pia kuna uwezekano wa kuwashwa ama kutokwa na maji maji katika sehemu ya kupitishia haja kubwa. Ingawa hivyo baadhi ya watu hawaoni dalili zozote kabisa lakini bado wanaweza kuwambukiza wanaofanya mapenzi nao.

Matibabu:
Iwapo matibabu hayatapatikana kwa haraka kuna hatari ya mirija ya kupitisha mayai (fallopian tubes) kuharibika na hivyo kusababisha utasa.Kama una kisonono usifanye tena mapenzi hadi utakapofanyiwa uchunguzi na kupewa madawa ya kutibu ugonjwa. Ni muhimu sana kumfahamisha mpenzio ili nae pia atibiwe.

Herpes: Huu husababishwa na aina fulani ya kirusi, kama kile kinachosababisha mafua na vidonda vya mdomoni. Mbali na kusambazwa kupitia ngono pia husambazwa kupitia kufanya mapenzi ya kunyonyana sehemu za siri.

Dalili:
Ni Kupata vidonda ukeni au uumeni mfano wa vile vinavyotokea mdomoni wakati wa homa kali ya mafua.Matibabu: Sasa kuna dawa na krimu za kupambana na virusi hivi.

Lakini kumbuka hata unapotibiwa virusi vya herpes bado hubaki mwilini mwako na vinaweza kuzusha tena vindonda. Pia kama umja mzito unaweza kumwambukiza mtoto wako, hivyo basi kama una vijidonda ni vyema kumjulisha mkunga wako ama daktari ili upate matibabu yafaayo.

Magonjwa mengine yanayoathiri njia ya mkojo (Non Specific Urethritis kwa kifupi NSU)NSU ni herufi zinazotumiwa kuelezea magonjwa ya bacteria yanayoathiri mfereji wa kupitisha mkojo yaani urethra.

Magonjwa hayo husambazwa kwa kupitia kufanya mapenzi.

Dalili:
Kwa wanaume dalili kubwa ni kutokwa na ute, kutoka kwenye tundu ya uume na huenda akahisi maumivu wakati wa kukojoa. Huenda ukasikia maumivu au kuwashwa-washwa.

Matibabu:
Majimaji yakitoka kwenye uume, isipokuwa mkojo au manii, ni lazima uchunguzwe na daktari, au nesi katika kliniki ya afya ya uzazi. Unaweza kutibiwa kwa kutumia vidonge vya anti-biotics.

Kaswende (Syphilis) Ugonjwa huu nao husababishwa na bacteria Treponema Pallidum

Dalili
Dalili zake hazionekani kwa urahisi. Huenda ukaanza kwa kijidonda au kipele kwenye uke au uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa. Kidonda hiki kinapopona usidhani ndio mwisho wa maambukizo la! Viini hivyo vinaweza kubaki mwilini kimya kimya kwa miaka mingi!

Matibabu:
Ni bora daktari kufanya uchunguzi wa damu kwani majimaji ya ukeni au uumeni huenda uchunguzi wake usionyeshe viini vya kaswende. Kaswende ni hatari, kama haitibiwi, inaweza kusababisha utasa au ugumba, na hata kuathiri moyo, mishipa ya damu, ngozi ya mwili, mifupa na hata ubongo na kurukwa na akili.

Hata hivyo matibabu yake ni rahisi Zipo dawa aina (antibiotics) zinazoweza kutibu kaswende kabisa. Ili kuzuia kuenea kwa maradhi hayo ni vyema mpenzio nae pia atibiwe.

Source:BBC

Matatizo katika sehemu za siri

Sehemu za siri ni zinazohusika na uzazi na mkojo kwa mwanaume na mwanamke. Kwa mwanaume, viungo vya uzazi vinatumika kwa malengo mawili. Kwanza ni utoaji wa mkojo na pili ni uzazi.

Mwanamke katika sehemu zake za siri kuna sehemu ya kutolea mkojo na uzazi ambazo ni sehemu tofauti.Matatizo yapo mengi kama utakavyokuja kuona.

Matatizo yapo kwa nje na kwa ndani, matatizo katika sehemu ya mkojo ya mwanaume yanaweza kuathiri uzazi na matatizo katika sehemu ya uzazi wa mwanamke yanaweza kuathiri sehemu ya mkojo.

Matatizo katika sehemu za siri yanaweza kuwa ni maumivu, muwasho na kusinyaa. Matatizo yote haya yanaweza kuwapata wanawake na wanaume.

Matatizo kwa wanaume

Matatizo katika sehemu za siri za mwanaume yanaweza kuwa yale yanayoathiri ngozi mfano muwasho sehemu za siri, upele, vidonda, maumivu wakati wa kukojoa, maumivu ya korodani mara kwa mara, kupungukiwa nguvu za kiume na matatizo ya uzazi kwa kushindwa kuzalisha mbegu za uzazi.

Chanzo cha tatizo

Vyanzo vya matatizo haya ni vingi, magonjwa ya ngono kama Kaswende, Kisonono, magonjwa ya ngozi mfano fangasi na ukurutu. Matatizo katika sehemu ya mkojo pia yanaweza kukusababishwa na vitu vingi mfano Yutiai, makovu ndani ya njia ya mkojo ambayo yanasababisha mkojo utoke kwa shida au kwa maumivu, uvimbe wa tezi dume (BPH) au saratani ya tezi dume.

Maumivu ya korodani yanaweza kuanzia hapo hapo kwenye korodani kwa kuumia au joto kali au kwa kuvaa nguo za kubana. Maambikizi kupitia njia ya mkojo pia yanaweza kujipenyeza na kuathiri mfumo wa uzazi kwa kuzorotesha uzalishaji wa mbegu za kiume.

Dalili za tatizo

Hakuna dalili moja au dalili maalum ya tatizo katika mfumo wa mkojo au mfumo wa uzazi. Hali ambayo si ya kawaida ambayo utaiona katika sehemu zako za siri ni dalili tosha ya matatizo haya katika sehemu za siri.

UchunguziVipimo mbalimbali vitafanyika kufuatana na hali inayojitokeza. Vipimo vya damu, mkojo au mbegu za kiume vitafanyika ili kuhakikisha tatizo ni nini.

Matatizo kwa wanawake

Matatizo kwa mwanamke ni kama vile yanavyojitokeza kwa mwanaume yaani inaweza kuwa muwasho kwa nje au ndani ukeni.Mwanamke naye anaweza kupatwa na maumivu ya njia ya mkojo, kutokwa na vipele au vidonda sehemu za siri.

Anaweza kutokwa na vioteo sehemu za siri hali ambayo pia inaweza kumtokea mwanaume. Mwanamke anaweza kutokwa na uchafu ukeni ukiambatana na muwasho na harufu, maumivu wakati wa tendo la ndoa na kupoteza raha na hamu ya tendo la ndoa.

Mwanamke pia anaweza kupatwa na tatizo la kutofika kilele cha tendo la ndoa, kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa, kutokwa na usaha ukeni. Hali nyingine ambayo pia inaweza kuathiri mwanamke ni kuhisi joto na ganzi sehemu za siri.

Uchunguzi

Uchunguzi wa tatizo hili hufanyika kutokana na jinsi mgonjwa anavyojihisi na kujiona katika maumbile yake ya siri.Vipimo vya mkojo, damu, HVS na vya kuangalia ukeni hufanyika.

Kipimo cha HVS ni cha kupima majimaji ya ukeni ili kujua chanzo halisi cha tatizo.

Athari za matatizo kwa mwanamke

Matatizo katika sehemu za nje ya uzazi yanaweza kusambaa hadi katika viungo vya uzazi vya ndani. Maambukizi haya yanapokuwa ukeni husambaa hadi katika mlango wa uzazi ambapo mwanamke hulalamika kupata maumivu baada ya kumaliza tendo la ndoa.Baada ya hapo maumivu hupenya hadi katika tabaka la ndani la kizazi.


Tiba fangas wanaoshambulia sirini

Kabla ya kueleza tiba tufafanue kwamba kuna baadhi ya mambo yanayosababisha watu kuwashwa sehemu hizo nyeti kama vile kuwa na fangasi tuliowataja hapo juu.

Wengine huwashwa kutokana na kutumia dawa za antibayotiki kwa muda mrefu. Kutumia dawa hizo husababisha fangasi kwani huua wadudu wote wanaolinda mwili na kuacha sehemu ya siri kukiwa hakuna kinga.

Dawa za antibayotiki ni kama, ampicillini amoxyclini, ciproflaxine, doxylline, erythromycine, gentamcycine na nyingine nyingi hivyo basi, jamii isitumie ovyo dawa hizi bila ushauri wa daktari.

Sababu nyingine ni unene kupita kiasi. Mtu akinenepa anaweza kupata fangasi kwa sababu unene husababisha jasho sehemu za siri na kuongeza unyevunyevu sehemu hizo pia michubuko kutokana na kubanwa na chupi.

Sababu zingine ni utumiaji wa dawa ya jamii ya steroid, dawa hizi ni kama prednisoline, hydrocortisone, dexameltasone na nyingine nyingi. Hizi nazo hupunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi kuzaliana kwa wingi sehemu nyeti.

Pia kuna magonjwa yanayosababisha kupungua kwa kinga nayo ni kisukari, Ukimwi na magonjwa mengine yanayopunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi.

Kuwepo na joto kupita kiasi na kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka pia husababisha fangasi sehemu za siri.

DaliliDalili kwa maradhi ya fangasi hutofautiana kati ya mtu na mtu ila dalili kubwa ni kutokwa na majimaji meupe wakati mwingine kama mgando wenye rangi ya njano ukiwa umeambatana na muwasho sehemu za ndani au kwenye mashavu ya sehemu za nje za siri za mwanamke.

Nje ya sehemu hizi za siri hutokea wekundu na maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa pia mgonjwa atajikuta akikojoa mara kwa mara.

Tiba na ushauri

Fangasi hutibika vizuri na mgonjwa kupona ila ni vizuri akaenda hospitali na kufanyiwa kipimo cha mkojo ambapo chembechembe za yeast huonwa vizuri kwenye darubini.

Daktari akigundua mgonjwa ana maradhi haya ataweza kumpa dawa zenye uhakika.Usinunue dawa hovyo na kutumia utasababisha usugu wa fangasi, hivyo kutopona.

Mgonjwa ahakikishe sehemu iliyoathirika inakuwa kavu masaa 24 na apake poda yoyote ya kutibu fangasi asubuhi na usiku kwa wiki 4 mfululizo.

Mgonjwa, kwa ushauri wa daktari atameza dawa za antibayotiki kama vile cloxacillin 250mg (2 x 3 siku 5) kama sehemu yenyewe imekuwa kama kidonda ili iweze kukausha haraka, anashauriwa asivae boxer/chupi bali avae bukta yenye kuruhusu hewa kupita na ajikaushe vizuri baada ya kuoga.

Ushauri pia unatolewa kwa mgonjwa asitumie sabuni zenye dawa kwani zitamsaidia kwa muda lakini zitafanya ngozi kupoteza uwezo wake wa asili wa kujilinda dhidi ya vijidudu na ahakikishe anabadili nguo ya ndani kila siku na iwe safi iliyopigwa pasi.

Kwa ushauri wa daktari mgonjwa anaweza kutumia cream iliyo kwenye tyubu inayoitwa Quadrimerm au fluocinonide cream kwa wiki mbili kwa kupaka sehemu iliyoathirika ikiwa kavu na akae dakika 30 kabla ya kuvaa nguo.


Source:Global Publishers
 
tumsubiri labda Riwa aweze toa maelezo ila me nakushauri uwahi hosptl kapate treatment mapema coz it might be STD.
 
hakuna umuhimu wa kuvaa kondom kama sijawahi kushiriki tendo hilo. ndio sababu nashangaa kama ni ugonjwa nimepata wapi?
 
hakuna umuhimu wa kuvaa kondom kama sijawahi kushiriki tendo hilo. ndio sababu nashangaa kama ni ugonjwa nimepata wapi?

Kama unatumia choo cha kukaa kuna uwezekano mkubwa umepata infection kutoka kwenye sinki la choo kama uume utakuwa unagusa sinki wakati ukiwa unajisaidia. Lakini kujua ni infection gani exactly ni vema kuenda hospitali kupima.
 
Nilishaanza kupoteza imani na baadhi ya thinkers baada ya kuona majibu mabovu kutokwa kwa baadhi yao. Asanteni sana mliochangia nitaenda hospitali.
 
It could probably be UTI (Urinary Tract Infection) kaka wahi haraka hospitali inatibika, the problem ni wanaume wengi wanaogopa kwenda hospital kwa kuogopa kuonekana wazinzi, afu another thing u should b concerned abt ni mpka maumivu hayo umeanza kuyasikia imeshakua something seious..pliz fasta hospitali.

**Usisahau kurudi kutupa feedback ya diagnosis, itasaidia kuongeza to our knowledge!
 
Am sure its not UTI as that i know how it feels niliwahi kupata kipindi fulani kupitia kwa chooo cha kukalia kama ulivyosema. ila nitacheki natawapatia majibu worryless great thinkers.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom