Kuwasha mitambo ya dowans ni kumsafisha lowassa na " maji ya mgao wa umeme"

saggy

Senior Member
Nov 12, 2008
153
70
Kweli wanasiasa wa Tanzania mnatupeleka wapi Watanzania?

1.Sio ninyi mliounda Tume ya Kuchunguza mchakato wa Zabuni ya Richmond na badaye mkamwajibisha na kumwangusha Waziri mkuu EL?

2.Sio ninyi baadaye mkusema Dowans imerithi mkata kutoka kwa Kampuni HEWA ya Richmond ?Leo mnasema Mitambo ya Dowans iwashwe?

3.Sio ninyi mliosema mkataba wa IPTL ulikuwa na Harufu ya Rushwa?Leo
mnawasha Mitambo ya IPTL?

4.Sio ninyi mliopigia kelele Dowans wasilipwe 96Bn. Leo mnasema Mitambo yao iwashwe kwa dharura?

5.Sio ninyi Mliopokea jana Milioni 90 kila mmoja wenu za kununulia Magari ya Kifahari katikati ya dhiki kubwa ya maisha inayotukabili Watanzania?

Naomba Majibu kutoka kwa wana jamii wenzangu.
 
Jamaa amenibonyeza anasema sasa zile pesa za kofia na vitenga sijui khanga zitarudi vipi? Mmeamua kumuweka kuwadi magogoni mnategemea nini? Yeye kaiba kura mmeridhika hamuoni wenzenu wa Misri na Tunisia.

Hivi wabunge baada ya hongo ya wazi wazi ya mamillioni bado mnafikiri watasema nini? Sijui Takukuru wako wapi?
 
Hii kitu imeratibiwa kwa muda mrefu. Iunganishe na kuondolewa kwenye uspika kwa Sitta, kuondolewa kwa mzee Shelukindo huko jimboni na kuandaliwa mtu ambaye angekuwa mrithi wake kwenye lie kamati nyeti ya madini na nishati, na hata kuwanunua baadhi ya wabunge wa upinzani tuliowaamini sana. Hata hivyo watanzania tutakuwa mabwege kupindukia kama tutakubali ushenzi huu. Serikali ilishindwaje kununua mitambo yake tangu Lowasa atemwe hadi leo ndiyo tuambiwe tena ukichaa wa dharura. Kama wanashindwa kuitaifisha hiyo mitambo waache tuendelee na hizo hasara za kukosa umeme hadi hapo umeme wa TANESCO utakapopatikana.
 
Kuna tetesi kwamba mitambo ya dowans inawashwa wiki ijayo kwa muda wa mwaka mmoja. Hii itakuwa kama malipo ya kushindwa kesi ICC. If this is true are they going to pay a lump sum of $60m or will their be extra charges which will include capacity charge and energy charge? What a joke
 
hivi hii serkali haina uwezo wa kufikiria alternative nyingine zaidi akili zao kuzunguka na dowans tu???.
ni aibu miaka 50 tangu tupate uhuru lakini hatujawa na chanzo mbadala cha kupata umeme zaidi ya kuimbiwa kilamwaka kuwa tunaomba mungu mvua zinyeshe bwawa la mtera?? AIBU!!!!!!
 
Back
Top Bottom