Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

Hilo mimi lilinifanya nijiulize ofisi ya raisi inafanyaje kazi, ina maana alikuwa hajui kuwa leo atamteua huyo kuwa naibu waziri wa fedha hadi akurupuke kumteua haraka haraka hivyo kuwa mbunge.

Mkuu bado una imani na utendaji wa huyu rais na ofisi yake?! Una moyo.
 
Naibu Spika hajui kwamba kuapishwa kwa mbunge ni formality tu, na mbunge anakuwa mbunge kabla ya kuapishwa.
The ignorant finality just oozes out of him with all pomp and confidence.
Kazi tunayo.
@Kiranga nina swali la kipuuzi. On the same note je, siku Tume ya Uchaguzi inamtangaza mshindi mpya wa kiti cha Uraisi anaweza kukabidhiwa ofisi kabla ya kuapishwa kama si incumbent?
 
Kwa ufupi NN katiba yote ni vurugu tu

Huko ndiyo hasa nilipokuwa naelekea! Katiba tuliyonayo ni mbovu sijapata kuona.

Kwa maoni yangu rais anapaswa asihusike kabisa na kuchagua wabunge kwa sababu bunge ndiyo chombo pekee ambacho wananchi wanausemi wa moja kwa moja juu ya wawakilishi wanaowapeleka huko.

Rais kuwa na mamlaka ya kuweza kuchagua wawakilishi 10 ni sawa na kujitwalia wajibu wa wananchi.

Natumaini katiba mpya itapunguza hayo mamlaka ya rais na kuondoa ulazima wa waziri kuwa mbunge.
 
Kwa hiyo wateuliwa ubunge na raisi wako beholden kwake yeye na si kwa wananchi?

Spinmasters wanaweza kukuambia serikali nzima inatumikia wananchi, kwa hiyo hata rais anatumikia wananchi, na hakuna conflict kati ya kumtumikia rais na kuwatumikia wananchi kwa maana ya kwamba hata rais anawatumikia wananchi.

Ndiyo maana nikasema hizi provisions zinataka rais aliye benevolent. You can't have a law that depends on an incumbent's benevolence. Vipi mwanajeshi mmoja chizi kama Idi Amin akichukua nchi kesho? Au kichaa mmoja anayejua kuficha makucha akipanda ngazi za CCM kwa kuonekana "mtoto mzuri" halafu akiwa rais afanye mambo ya ajabu?

Swala zima la rais kuteua wabunge, na la wabunge kuwa mawaziri yanazaa an inherent conflict of interest. Mbatia kesho kwenye mjadala wa kumuondoa Pinda kukibakia kura yake tu kuamua, wapinzani wa NCCR wakimtaka apige kura kumuondoa Pinda, Kikwete akionekana kutaka Pinda abaki, Mbatia atapiga kura vipi?

Ataamua kulipa shukrani kwa Kikwete au kwenda na consensus ya chama chake? Tayari Kikwete kwa kupewa uwezo wa kuchagua wabunge kasha compromise integrity ya bunge.
 
WRONG. RAIS amevunja Katiba, hakuna ubishi. Sifa ya kuteuliwa WAZIRI ni kuwa MBUNGE, na MBUNGE ni yule aliye (1) chaguliwa/teuliwa, na (2) kuapishwa. Na shughuli za BUNGE, siyo pale Bungeni pekee: kuna shughuli za kamati, kwa mfano sasa tunakwenda kwenye bajeti, nani atawasilisha mapendekezo ya wizara zao mbele ya kamati husika. Bila shaka watatumika mawaziri ambao ni wabunge kamili, hata ukweli una baki kuwa RAIS kavunja KATIBA kwa kuteua watu ambao si wabunge kamili kuwa mawaziri. MIMI ninashauri wanaharakati waingie mahakamani kutafuta tafsiri, au mawaziri hao wawekewe a quo warranto (injunction) watekeleze majukumu ya uwaziri hadi watakapo apishwa, wasishiriki vikao vya baraza la mawaziri nk!

Mkuu EMT wenzio tangia juzi tumelifanyia kazi hilo suala na tukapata jawabu. Anaweza akashika uwaziri bila kuapishwa ila.hawezi kushiriki shughuli za bunge kabla ya kuapishwa. hiyo wataapishwa june kabla ya kuanza sughuli za bunge
 
@Kiranga nina swali la kipuuzi. On the same note je, siku Tume ya Uchaguzi inamtangaza mshindi mpya wa kiti cha Uraisi anaweza kukabidhiwa ofisi kabla ya kuapishwa kama si incumbent?

Hawezi,

Lakini kama unataka ku draw parallel kati ya mbunge na rais analogy zitashindwa.

Kwa mfano, PM Pinda na January Makamba wamekuwa wabunge bila hata ya kupata kura moja. Kwa sababu "wamepita bila kupingwa" (ingawa ubunge huu hautambuliki kikatiba).

Ikitokea vyama vyote vya upinzani vikishindwa kutoa mgombea wa urais, mgombea wa CCM "atapita bila kupingwa"? Atapigiwa kura na wananchi au hatapigiwa?

Kama unataka kufananisha vitu, fananisha vinavyolingana.
 
Spinmasters wanaweza kukuambia serikali nzima inatumikia wananchi, kwa hiyo hata rais anatumikia wananchi, na hakuna conflict kati ya kumtumikia rais na kuwatumikia wananchi kwa maana ya kwamba hata rais anawatumikia wananchi.

Kwa msingi huo basi hata hakuna maana ya kuwa na mgawanyo wa madaraka!

Mimi bado siafiki rais kuwa na mamlaka ya uteuzi wa wabunge kwa sababu hii inampa mamlaka katika matawi yote matatu ya serikali.

Not good at all. Bungeni hatakiwi kabisa awe na mamlaka yoyote yale au kama ni lazima sana basi na yawe madogo sana.
 
WRONG. RAIS amevunja Katiba, hakuna ubishi. Sifa ya kuteuliwa WAZIRI ni kuwa MBUNGE, na MBUNGE ni yule aliye (1) chaguliwa/teuliwa, na (2) kuapishwa. Na shughuli za BUNGE, siyo pale Bungeni pekee: kuna shughuli za kamati, kwa mfano sasa tunakwenda kwenye bajeti, nani atawasilisha mapendekezo ya wizara zao mbele ya kamati husika. Bila shaka watatumika mawaziri ambao ni wabunge kamili, hata ukweli una baki kuwa RAIS kavunja KATIBA kwa kuteua watu ambao si wabunge kamili kuwa mawaziri. MIMI ninashauri wanaharakati waingie mahakamani kutafuta tafsiri, au mawaziri hao wawekewe a quo warranto (injunction) watekeleze majukumu ya uwaziri hadi watakapo apishwa, wasishiriki vikao vya baraza la mawaziri nk!

Kasome katiba vizuri, mbunge anapoapishwa anakuwa mbunge tayari. Mbunge anakuwa certiofied na Tume ya Uchaguzi, kwa hiyo kwa wabunge wanaoteuliwa na rais wanakuwa certified na rais I resume.

Kuapishwa ni formality ya kuonyesha utii kwa Spika na some such bs.

Ingekuwa kuwa mbunge mpaka uapishwe na Spika, Spika asingeweza kuwa Spika kwa sababu Spika inabidi achaguliwe na wabunge.
 
Mimi naona kiini macho maana sielewi nini maana ya kuapa! Je kiapo kipi kikubwa kuliko kingine? na Kipi kinatakiwa kianze kwa mujibu wa sheria? Je serikali kuteuwa watu na kuwapa mamalaka ya kutumikia wizara kabla ya kuapishwa ubunge akiharibu mapema tunasemaje kama akitolewa kabla ya kufika kuapa? Je chochotekinaweza kutokea mfano kifo je bunge linamtambua hali hajaapishwa kuwa mbunge au atakuwa ni waziri tu na je akina nani watahusika na msiba? Je bunge au wizara? Je ikitokea tatizo lolote je inawezekana kabisa huyu kuitisha kikao cha bajeti cha kamati za kudumu za bunge kuipitisha na kufanunua? Je kamati za kudumu za bunge zinatakiwa kupata maelezo ya wizara kutoka kwa nani kama anyesimama katika bunge, bunge bado halimtambui? Je atakapo aanza kuelezea hizi kamati kuwa wizara yangu inategemea kutumia kiasi kadhaa je uhali wake unakuwepo?

"KWA MTINDO TUNAOENDA NAO WAZIRI MKUU ATATEULIWA NA KUANZA KAZI MARA MOJA BAADAYE NDO BUNGE LIMUIDHINISHE NA HATA ASIPOIDHINISHWA NA BUNGE BADO ATAENDELEA KUPATA HAKI ZOTE KAMA ALIYEPITISHWA NA BUNGE KWASABABU MWENYE NCHI KASEMA MAANA NCHI HII HAINA KATIBA IMARA NA INAYOTOA MWONGOZO WA NINI KIANZE NA KWA HALI HII MTAJASHANGAA MAWAZIRI WANAWEZA KUJA KUAPA KWA SIMU BILA YEYE KUWEPO NA KIAPO KIKASWIHI MAANA NI ANAYETEUA NDO ANAJUA YOTE WENGINE MAMBUMBU"
 
Hawezi,

Lakini kama unataka ku draw parallel kati ya mbunge na rais analogy zitashindwa.

Kwa mfano, PM Pinda na January Makamba wamekuwa wabunge bila hata ya kupata kura moja. Kwa sababu "wamepita bila kupingwa" (ingawa ubunge huu hautambuliki kikatiba).

Ikitokea vyama vyote vya upinzani vikishindwa kutoa mgombea wa urais, mgombea wa CCM "atapita bila kupingwa"? Atapigiwa kura na wananchi au hatapigiwa?

Kama unataka kufananisha vitu, fananisha vinavyolingana.

The point I am trying to make ni kuwa, swala la kuapishwa si dogo kama tunavyotaka kuaminishwa...eti it is just a formality, no, hapana - that's all.
 
Kwa msingi huo basi hata hakuna maana ya kuwa na mgawanyo wa madaraka!

Mimi bado siafiki rais kuwa na mamlaka ya uteuzi wa wabunge kwa sababu hii inampa mamlaka katika matawi yote matatu ya serikali.

Not good at all. Bungeni hatakiwi kabisa awe na mamlaka yoyote yale au kama ni lazima sana basi na yawe madogo sana.

Yeah,

Mimi siafiki hata rais kuwa sehemu ya bunge, what's the logic? Kama una separation of powers kwa nini rais awe sehemu ya bunge?

Kwa sababu hawachelewi ku invoke some obscure sorcery na kusema rais kama sehemu ya bunge ana mamlaka ya kumteua mbunge na kumuapisha kuwa waziri na mbunge pamoja.

Inakuwa kama rais anataka kuwa na bunge lake ndani ya bunge vile.
 
The point I am trying to make ni kuwa, swala la kuapishwa si dogo kama tunavyotaka kuaminishwa...eti it is just a formality, no, hapana - that's all.

Kwa nini si dogo katika context hii ya mtu kuweza kuteuliwa na rais ubunge na kuapishwa uwaziri kabla ya kuapishwa ubunge?

Kile kiapo ni cha nini? Madhumuni yake ni nini? Swali hapa ni, je, mtu anakuwa mbunge kabla ya kiapo ama la?
 
Mantiki ya separation of powers ni checks and balances. Sasa unapokuwa na raisi ambaye ana watu wake ambao kawateua na wengine ambao wanamfanyia kazi moja kwa moja (mawaziri), in a sense defeats the purpose.

How can members of parliament who are also members of the executive branch check themselves?
 
Kwa nini si dogo katika context hii ya mtu kuweza kuteuliwa na rais ubunge na kuapishwa uwaziri kabla ya kuapishwa ubunge?
Kwa sababu Raisi hawezi kumteua mtu kuwa waziri mpaka awe mbunge. Swali, je kwa nini Raisi hamteui Waziri Mkuu mpaka awe ameapishwa kwanza kama mbunge if kuapishwa is just a formality?
 
Kwa maana hiyo ni batili kuwa waziri kwa sababu uwaziri ni kazi za bunge? nilidhani kuwa tafasiri yake ni kwamba hataingia bungeni kujibu maswali ama kuwasilisha chochote bungeni kabla ya kuapa.
Uwaziri ni kazi ya mbunge ndio maana kabla hujawa waziri sharti uwe mbunge kwanza. Ili uwe mbunge kamili lazima kwanza uwe umepata kiapo cha uaminifu toka kwa Spika. Ndio maana hata tume ya uchaguzi ikimtangaza mshindi inasema ni mbunge mteule, maana yake kuna kitu bado hakijakamilika. Mimi bado sijaelewa inakuwaje mtu ateuliwe kuwa mbunge, kabla hajaapa kwa nafasi hiyo ya kuwa mbunge anateuliwa tena kuwa waziri. Wataalam wa sheria watusaidie hapa.
 
Hapa ukweli ni kwamba JK inabidi atumie mabavu yako kama Rais kuwatandika viapo viwili hao mawazir wawili ambao walikuwa hawajaapishwa kama wabunge. Hawezi kuingia ofisini kufanya kazi za kiwaziri kwa sababu hawajaapishwa. Na pia Waziri anatakiwa awe ameapa viapo vyote anavyotakiwa kuwapa, that means ikiwamo ubunge. Vinginevyo wanaweza kutayarishiwa utaratibu spika akawaapisha ofisi ndogo ya bunge Dar es Salaam, maana sheria haisemi kwamba ni lazima waapishwe kwenye mkutano wa bunge...

Hapa ndo pale ambapo naona kuna umuhimu wa katiba kubadilishwa ili kwamba mawaziri wasiwe lazima kuwa wabunge. JK aliona vichwa ambavyo vinafaa, ila sheria ikambana, ikabidi awateue wawe wabunge fasta fasta. I don't think this is right. Tufanyie marekebisho katiba kuhusu hili.
 
Mantiki ya separation of powers ni checks and balances. Sasa unapokuwa na raisi ambaye ana watu wake ambao kawateua na wengine ambao wanamfanyia kazi moja kwa moja (mawaziri), in a sense defeats the purpose.

How can members of parliament who are also members of the executive branch check themselves?

Deeper down ukweli ni kwamba hizi systems si zetu, sie tumeziiga tu na sasa hivi naona tuna ape tu Westminster. Therefore aping apes.

Sie tulishazoea uchifuchifu, anachosema Chifu kinakubalika. Ndiyo maana hata tunapojidai kutumia mi concept mikubwa sijui democracy, sijui separation of powers, inakuwa kama mchezo wa Pwagu na Pwaguzi kwa sababu mwisho wa mchezo Chifu ana control kila kitu.

Anateua wabunge, mawaziri na majaji. Branches zote anateua watu wake. Mpaka mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, refree wa mechi yake mwenyewe, anamchagua yeye mwenyewe. Mabalozi, wakuu wa mikoa, viongozi wa Tume na mashirika ya umma etc.

Sasa separation of powers yetu ina integrity gani?

Huyu rais au Sultan-Papa Mtakatifu Khalifa Kikwete bin Harun Rashid ?
 
Back
Top Bottom