EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
- Thread starter
- #41
68. Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha
uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini
Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla
hajaapishwa.
UFAFANUZI
1. Kwanza elewa kuwa amesha itwa Mbunge si Mteule hata kabla ya kuapa na sifa ya kuitwa Mbunge ndio inatakiwa ili mtu awe Waziri
2. Inasema kabla ya kushiriki shughuli za Bunge si shughuli za Serikali (Waziri ni sehemu ya Utendaji wa Serikali (Executive).
Hitimisho: Hao ni Mawaziri na wanawajibika kwa aliyewateuwa (Rais) kwa kusimamiwa na Waziri Mkuu.
Vipi wakiapishwa kuwa mawaziri hiyo tarehe 7 halafu wakitinga wizarani wanakuta barua kutoka Kamati ya Bunge ikimtaka Waziri aijibu yeye mwenyewe kabla ya kikao kijacho cha bunge? Au vipi kamati ya bunge ikimzukia wizarani tarehe 8 kutaka maelezo/ufafanuzi wa kitu fulani? Atajibu hiyo barua/kukutana na hiyo kamati au atasepa na kusema bado hajaapishwa kuwa mbunge ili aweze kushikiri katika shughuli za bunge?