Kuwa ugenini mateso

Imekuwa ikisemwa hivyo mara kwa mara. Mimi niliamini huu usemi mwaka 2002., nakumbuka nilikuja Dar kufatilia uhamisho wangu wa shule, nilikaa kwa baba yangu mdogo kwa takribani wiki moja. Huyo mama niliyemkuta hapo alikuwa hapiki mpaka mumewe awepo. Wiki niliiona kama mwaka, hata nilipoaga nilipewa nauli kimanati. Najua wengi tumepitia kwa ndugu kutokana na sababu mbalimbali, kuna walioishi vizuri lakini wengi wanalalamika. Je tatizo hasa nini? Ukiwa ni miongoni mwa uliyetendewa mabaya, umejifunza nini?

Hata marafiki wengine sio watu kabsa....nakumbuka long back nikiwa chuo nliwahi kukaa kwa a friend of mine for just a week nikijipanga kupata my own accomodation.
Yan ilikua nikitumia hata sukari, majani ya chai, jam & blue bland, sabuni etc. (vitu vidogo vidogo tu)....ilikua ni shida sanaa.
Kelele na majungu kibao....ni mengi tu alifanya na kuongea. Ilinifungua akili sana kuhusu tha type of people i call friends. Nkajiuliza sana, ivi siku nimeanguka nashida huyu ni mtu wa kutegemea kweli ??
Siku naondoka nikamnunulia kila kitu chake nlichotumia in that week. Alikua mshkaj wang sanaaa but since then ikawa ni salamu tu....after like 3 months jamaa alinifata akaniomba msamaha...nlimsamehe but it has never been the same....achilia mbali ugeni wa kindugu nao ni shida sanaaa.
 
Haya mambo yako pande zote zote. Sisi mama yetu alikuwa anatuambia tulale kwenye makochi wageni wakija nyumbani ambao most of them ni ndugu upande wa baba. Kuna waliokuwa wanakuja bila hata malengo; si wa kuondoka leo au kesho lakini tulikuwa tunabanana tu. Wengine wakaja ku win maisha tukawa tunawasikia bombani wala shukurani hawana.

Wengine ni ndugu wa mbali. Wanatangaziana tu huko kijijini; ukienda dar fikia kwa mzee fulani ana nyumba kubwa. Tena wanakuja kwa kushtukiza maana those days hakukuwa na simu za viganjani ni za kukoroga tu. Mnashtukia mtu katia timu. Sisi tulikuwa tuna mind kweli maana tulikuwa hatuko comfortable lakini mama alikuwa mkali kweli yani priority kwake ni wageni. Mama alipoachana na baba walikuwa wa kwanza kushangilia wala hawakuwa wanakumbuka fadhila zake. Binadamu ni wagumu sana kuishi nao.

Umesema kweri kabisa, ndugu wengi lawama tu. Ukiwa nazo wanamiminika kama hawana akili nzuri, siku ukipata matatizo hujikata mmoja mmoja na masimango kibao. Na sio siri wengi wanaopenda kusaidiwa sana wao huwa wagumu kusaidia wanapopata na hata kidogo ulichowasaidia husahau na kujidai kuwa kama usingewasaidia wewe wangesaidiwa na wengine
 
mmh....watu wengine tukisimulia masaibu yaliyotukuta......tutajaza kitabu......ila cha muhimu....ni kumuombea adui yako aishi siku nyingi.....ili unapofanikiwa ajionee kwa macho yake mawili

Ukifatilia matajiri wengi hii ndio sabab wanatafuta hela na mafanikio kwa nguvu zote. Kuna kitu au watu kwa namna moja au nyingine anajaribu kuwa prove wrong hence anaweka a lot of effort. Dat mimi ninaweza na nitawaonyesha kwamba ninaweza.
 
Haya mambo yako pande zote zote. Sisi mama yetu alikuwa anatuambia tulale kwenye makochi wageni wakija nyumbani ambao most of them ni ndugu upande wa baba. Kuna waliokuwa wanakuja bila hata malengo; si wa kuondoka leo au kesho lakini tulikuwa tunabanana tu. Wengine wakaja ku win maisha tukawa tunawasikia bombani wala shukurani hawana.

Wengine ni ndugu wa mbali. Wanatangaziana tu huko kijijini; ukienda dar fikia kwa mzee fulani ana nyumba kubwa. Tena wanakuja kwa kushtukiza maana those days hakukuwa na simu za viganjani ni za kukoroga tu. Mnashtukia mtu katia timu. Sisi tulikuwa tuna mind kweli maana tulikuwa hatuko comfortable lakini mama alikuwa mkali kweli yani priority kwake ni wageni. Mama alipoachana na baba walikuwa wa kwanza kushangilia wala hawakuwa wanakumbuka fadhila zake. Binadamu ni wagumu sana kuishi nao.

Story yako iko similar na yangu kwa 90% hapo kwenye mama weka baba nd bado wanaishi pamoja.
 
naona mmeongea saana. kila mmoja kateswa vipi nyie kama mnafamilia ndugu zenu wakiwatembelea wanaenjoy au mnaendeleaza yalayale
 
Siku hizi boarding schools tu ni mateso tosha kwa watoto haina haja ya kuwapeleka kwa ndugu

ni bora kila likizo umpeleke mtoto kwa ndugu ili akajifunze maisha, ukimuacha wiki mbili au tatu akirudi kanyookaaaaaaa. lazima appreciate unachompa. kila akikuangalia anaomba mungu usife leo.

hakikisha unampeleka mbali kidogo ili asiweze hata kudandia gari kurudi home.
 
Nyumbani kwetu tulifundishwa kufanya kila kitu, kila aina ya kazi za nyumbani mpaka kazi za bustani na kutunza mifugo. Tulikuwa tunapiga kazi mpaka mtu unatamani shule zifunguliwe urudi. Na hapo palikuwa kwetu kabisa. Ndugu ndio walikuwa wanatanua, tulikuwa tunaambiwa hapa ni kwenu unategemea nani akutengenezee kwako kama sio wewe.

Mi nadhani wazazi ndio wanaokosea wanaona kuwafundisha watoto wao kazi za kila aina ni kuwatesa. Hata mimi nilikuwa naona nakosewa haki na kuonewa wakati huo nikiwa mdogo. Namshukuru mama yangu may the Good Lord rest her soul in eternal peace, nikiwa na miaka 18 niliweza kuendesha nyumba na kutunza familia na wadogo zangu watano. Ninaimagine kama ningekuwa legelege ingekuwaje.

Mh. Kaizer unachokiuliza nami nimeshajiuliza sana, mimi nimelelewa kwa mjomba baada ya Baba kutangulia kwenye HAKI.
Na kwa vile tulizaliwa 7 hivyo nduguze Mama na ndugu wa Baba (the late) wakatugawana sisi watoto kumwondolea Mama task work ya maisha, huko kwa Uncle ndipo nilipoyajua haya mnayoyasema, aidha Uncle hakua na tatizo, Mkewe ndiye alikua mwiba wa Nungunungu! Pamoja na yote maisha ya hivyo yana advantage na disadv kwani kwa upande mmoja utapata faida ya kujua Njaa inavumiliwaje utajua Branget linafuliwaje, vyombo vinaoshwaje, deki inapigwaje, utajua kupika n.k.
Watoto wanaokulia kwa wazazi wao wa kibayolojia wenye umri sawa na wanaokulia kwa ndugu walezi hawawezi kua sawa katika kumudu mazingira yanayowazunguka, wale walioko kwa walezi wanakua more active kuliko wanaokulia kwa wazazi halisi.
 
kuna watoto wengine sio kwamba wananyanyaswa ugenini ila kutokana na malezi waliyoyapata nyumbani kwao yakudekezwa,anakuwa hawezi kufanya kazi,hata kama ukimwambia aoshe vyombo kwa nia njema kabisa yeye ataona unamwonea na unamnyanyasa kwa sababu kwao hajazoea kufanya kazi na ndio anatakiwa awe hapo ugenini kwa miaka minne au mitatu ya masomo yake, na msosi anapata apendavyo.Hapo vipi ?
 
Huwa najitahidi sana kuishi kwa kanuni ya usimtendee mwingine usichopenda kutendewa wewe, sio rahisi lakini inawezekana.

Inaelekea kila mtu kayapitia haya. Sasa cha kunuia hapa c kwamba mtoto wako asiende kwa mtu, bali usije mtendea hivyo mtoto wa mtu mwingine. Kwa maana hii dunia tunategemeana, ina wezekana ukawa umejidhatiti vya kujitosheleza, lakini kunamatukio yanatokea mtoto anajikuta yupo kwa watu bila kupenda. kila mtu akimjali mtoto wa Mwingine kama wakwake, hakuna mtoto atakaye nyanyasika.
 
Ukifatilia matajiri wengi hii ndio sabab wanatafuta hela na mafanikio kwa nguvu zote. Kuna kitu au watu kwa namna moja au nyingine anajaribu kuwa prove wrong hence anaweka a lot of effort. Dat mimi ninaweza na nitawaonyesha kwamba ninaweza.

Ni kweli mkuu, ukinyanyasika sana utatia akili tu!!
 
Ni kweli mkuu, ukinyanyasika sana utatia akili tu!!

Mara nyingi such people wanawapenda sanaa watoto wao....hawataki kabsa wakose mahitaji ya msingi....it reaches a point umenyanyasika na kudharauliwa sanaaa. Ile hasira na uchungu from within inakua converted to efforts...ndio unakuja ona watu wa kawaida sanaa wasio na elimu kubwa wanafanya wonders....75% ya matajiri wanaofanya biashara kariakoo....hata hyo form 1 hawajawahi kuiona....ukipiga nao hadithi utagundua nlicho kueleza hapo juu.
 
Hayo yapo mijini kwa sana na kama ndo mara ya kwanza umefika mjini utajuta. Kijijini watu wana upendo na wanajali utu.
 
Hii thread inaweza kukusisimua ka uwoga au hasira kwa ile hisia unayopata ktk post za watu. Mie nmekaa mahali kwingi na mmeona mengi na kuexperience mengi. Wanasema mtu hawi mbaya kwa yote kna mema lazma anatenda ila ndio binadamu tunaona negatives kuliko wema. I hv bn through hell ila had leo ukiniuliza ntasema i miss the lyf niliyopitia mana it was happy in its own way japo cruel in all eyes.

Kikubwa ni kwamba my kids wataishi na mm tuu kama ktembea tunaenda wote tunarudi wote na nikiwaacha basi ni 7b i know the bondage na mwenyeji ni kubwa na atawalinda kama wake.
 
Ila kuna wazazi wengine wanakosea pia, kuna familia ninaijuwa walithubutu kumruhusu mtoto wao aje asomee dar eti tu kwa sababu mtoto wao anapenda kuja dar kwa sababu zake binafsi,akafikia kwa watu, bahati mbaya wenyeji hao walikuwa na nafasi ndogo sn, ndipo wakamwomba baba mtu kama itawezekana wasaidiane kifedha wampeleke mtoto boarding,baba wa mtoto alikataa na kusema hana pesa ya boarding na kuwaambia wenyeji hao ndo watoe pesa hizo, wakati baba huyo uwezo anao.
 
Back
Top Bottom