Mawaiba
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 417
- 150
Najaribu kukumbuka jinsi Mwl. J.K. Nyerere alivyokuwa na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi magumu. Nina imani kabisa kutokana na uwezo mkubwa wa J.K. Nyerere katika kusoma alama za nyakati na kufanya maamuzi magumu accordingly, kama leo hii angekuwa hai Nyerere angeshauri muungano wa Bara na Visiwani uvunjwe. Miongoni mwa maamuzi magumu ambayo viongozi wetu wa sasa hawana uwezo wa kuyafanya kwa hiyari ni "kung'atuka" kutoka madarakani kama alivyofanya Nyerere. Hebu tukumbushane baadhi ya maamuzi magumu ambayo Mwalimu aliyafanya wakati wa uhai wake, ili liwe somo kwa viongozi wetu wa sasa. Karibuni....