Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja husababishwa na tamaa. Ndio sababu wasichana wengi wadogo wana simu za bei kubwa ukilinganisha na watoto wa kiume hata kuliko sisi wazazi. Wakiume pia wapo kwani wapo wachache ambao wanamilikiwa na mashuga mami, ambao huwaita Serengeti boys. Utakuta mtu ana rafiki kwa ajili ya lift, mwingine kwa ajili ya chips na vinywaji, yupo wa kwenda nae beach na kadhalika. Sisi kama wazazi inabidi tubadili mwelekeo na mtazamo, tuache kushabikia tunapoona mtoto wa jirani au ndugu anapotoka.

Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja ni tatizo kubwa sana, linahitaji ujasiri wa hali ya juu. Na elimu ya ziada inatakiwa kutolewa. Kwani kuna wingi wa demokrasia ya vyombo vya habari ambavyo vinachochea mtu kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja. Pia heshima ya woga ndani ya wapenzi ni sababu kubwa ya tatizo hilo. Mmoja anaogopa kumwambia mwenzake abadili staili ya mapenzi kwani anaogopa kuonekana mhuni. Na pia anafikiria iwapo ataniktalia nitajisikiaje? Vibanda vinavyoonyesha mikanda au video usiku navyo ni chanzo kikubwa sana, kwani ufikapo usiku mnene mikanda yenye vishawishi vya ngono huonyeshwa. Fungakazi ni kwenye internet na kwenye simu. Kwani watu wanatumiana move za kutisha za kimapenzi kwenye simu. Nyumba za wageni nazo hazichagui, ili mradi ulipie. Uingie na mtoto wa sekondari, wa shule ya msingi, wa chuo na kadalika hakuna wakukuuliza, je tutafika?

Elimu na ushirikiano vinatakiwa. Femina wana kazi nzito ya kufikisha ujumbe kwa walio wengi hasa vijijini. ONE LOVE IS A SOLUTION.

Kipindi cha Fema wiki hii kililenga panapostahili, pale kijana kutoka Mtwara alipokiri kuwa na rafiki zaidi ya mmoja wa kingono. Kitendo hicho kilimpelekea kijana huyo kupata gonjwa la ngono. Cha kushangaza ni kwamba kijana huyo hakujua gonjwa hilo alilipata kutoka kwa mwanamke yupi? Nilichojifunza ni kwamba, vijana tulio wengi hatutaki kutumia kinga na tunachukulia magonjwa ya ngono ukiwepo UKIMWI kama ajali kazini. Mahusiao ya kingono kwa mpenzi zaidi ya mmoja ni hatari sana.
 
hii thread tangu 2008 mpaka mwaka huu haikupata koment hata moja

Watu hawakutoa coment kwa sababu inagusa wengi tuna wapenzi zaidi ya mmoja.na jambo hili halikuanza leo ni tangu zamani ola limepata changamoto (Challenge) Sababu ya magonjwa .Ingawa watu bado haachi hiyo dawa!
 
Ni tatízo sugu linachagizwa na mengi hasa na maadui wetu wawili. Ujínga. Umaskini.
 
Yaani mtoa Mada umenikosha dear. Nilipokuwa Bongo recently nilishangazwa na wakina Dada sana sana na misemo yao mpaka ndugu zangu wakawa wananicheka honestly. Niliwasikia wakina Dada wengi wakiongelea Visadolini walivyo navyo. Honestly akili na mawazo yangu iliniambia ni visadolini vya mafuta ya kula au taa kumbe I was wrong, very wrong . Siku Mdogo wangu akaniambia kuwa sister Sweet wenzio hawamaanishi hivyo , visadolini ni wanaume. Yaani sikuamini nikafikiri mdogo wangu ananitania since huwa tunataniana sana. Haikuishia hapo siku moja wakati natoa huduma ya Afya , nikiwa hapo nikaufuatilia tena hii msemo , nikaja kugundua Mdogo wangu was right . Kuna baadhi ya wadada Wana wanaume zaidi ya watatu . Mmoja Wa kulipa rent, Wa pili kununua mavazi, Wa tatu ndio huyo ambae huenda ndio Wa ukweli aka mchumba. Wa NNE ni Wa mizinga tuu, Jamani nilichoka . Sasa najiuliza hivi Kweli Huku Ukimwi utaisha Tz kwetu.? Jamani tujitahidi sio tuu wanawake hata wakaka lakini haswa wanawake mwenzangu hebu tujitunze huu mwili , kwa kuwa ina thamani sana kuliko hata hivyo Visadolini . Mungu atusaidie kwa Kweli . Thanks.
 
Kwa haraka haraka malaya wana ladha tofauti tofauti

Leo utataka mnene kesho mwembamba kesho kutwa model

Kazi kwako
 
Kwa haraka haraka malaya wana ladha tofauti tofauti

Leo utataka mnene kesho mwembamba kesho kutwa model

Kazi kwako
Hii kitu ndio naona inafanya malaya kuwa na deal sehem zote af pia hakuna gharama ya kupoteza muda zaid hii pia ni faida nyingine
 
Hamna gharama mkuu.... Piga hesabu ukiwa na dem wako ana cost kias gan kwa mwezi af rudi kwa hawa watu hiyo cost utabeba wangap..... Otherwise uwe na dem mwepes asiekua na karaha kwa wallet yako
Nazani ni vyema kubadilisha chakula mkuu japo ni expensive
 
Hamna gharama mkuu.... Piga hesabu ukiwa na dem wako ana cost kias gan kwa mwezi af rudi kwa hawa watu hiyo cost utabeba wangap..... Otherwise uwe na dem mwepes asiekua na karaha kwa wallet yako
Anya tukija kwenye suala la calculations inategemeana kwa mwezi unachukua Malaya wangapi, na je unamwachia shilingi ngapi za baada ya show?
 
Back
Top Bottom