Wote wanafunzi,waalimu na wasimamizi.
Si walishasema kuwa watamlinda Ndalichako kwa nguvu zote?Hao wahusika wakuu hawataki tu, kudhibiti hiyo hali. Serikali kama ikitaka jambo lake lifanyike litafanyika tu bila mizengwe wala kupoteza muda.
Hao watayarishaji wa mitihani wanajulikana, wanaoingiza Data kwenye Computer wanajulikana, wachapishaji wanajulikana, wanao hifadhi hiyo mitihani pia wanajulikana. Sasa tatizo liko wapi?
Mbona hatujawahi kusikia kuwa PESA mpya zinazo chapishwa zimepotea?
Siku Serikali itakapo amuwa kuwaadhibu wale wote wanao husika na UFISADI huu, tena kwa adhabu ya kupigiwa mfano, watakao fuwata watatia akili.
Angalieni mfano wa nchi ya China, mafisadi wanawafanya nini. Serikali ijifunze kutoka kwao.
Hivi jamani na tujiulize huku kuvuja kwa mitihani ni kosa la nani ?
Na inakuwaje wanafunzi ndio wanaobebeshwa lawama hadi kufika kufutiwa mitihani yao na kutelekezwa ?
Je mwananfunzi anapobahatika kuona mtihani ambao ataufanya siku mbili tatu zijazo ,ataupuuza au ataona
hii ni bahati ya mwaka ? Hata mwanafunzi alie na akili za kufaulu pindipo akisogezewa mtihani uliovuja basi hata wacha kuuangalia na kuufanyia kweli.
Baraza la mitihani linapokaa kwenye vyombo vya habari na kuanza kuonyesha madudu ya wanafunzi na kuuhakikishia umma kuwa wanafunzi hao waliiba mtihani ? Hivi walimuibia nani ? Walivunja ofisi za wizara ? Walitekagari inayobeba mitihani ? Naona baraza hili na utitiri mzima hadi kwa Waziri wanajificha na kufinya uzembe uliotokea ndani ya Vyombo vyao kwa kushindwa kuudhibiti mtihani huo usivuje.
Ikiwa mtihani umevuja hivi ni sawa kuwabana wanafunzi na kuwazuia kufanya tena mtihani yaani nionavyo huku ni kuwapotezea muelekeo wa maisha yao kwa kosa ambalo sio lao.
Hivi Wizara imeshindwa kuchunguza au kutuma vyombo vya uchunguzi kubaini ni nani aliehusika na uvujaji wa mitihani ? Na badala yake kuwakaba wanafunzi kwa kuwakatishia masomo yao ? Kuna nchi moja huko uarabuni imebaini kuwa mtihani umeibiwa ,tangazo la mwanzo ni kuwa result imefutwa na wanafunzi watafanya tena mtihani na uchunguzi unafanyika kujua ni nani alihusika kwa kuvuja kwa mitihani na sheria kuchukuliwa ,wanafunzi hawakuguswa wala kuadhiriwa zaidi ni kuwa watatajiwa tarehe ingine ya kufanya mitihani ,Hapa Tz sipo ni kulinda wizara na wafanyakazi wake kwa kuwatelekeza wanafunzi. Je ni haki ?