Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH) Featured

Saratani ya Tezi Dume - Chanzo na Tiba

Tatizo jingine linaloathiri tezi dume ni saratani ya tezi dume. Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na saratani kwa wanaume wa umri mbalimbali duniani. Aidha ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wa umri miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, ni nadra sana kwa saratani hii kuwapata wanaume chini ya miaka 40.
Nani yupo katika hatari ya kupata saratani ya tezi dume?

Watu walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na:

  • Wanaume wenye asili ya Afrika (weusi) ikilinganishwa na wazungu
  • Wanaume kuanzia miaka 60 na kuendelea
  • Wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba amewahi kuugua ugonjwa huu.
  • Wanaume wanaokunywa pombe kupindukia
  • Wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi
  • Wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali
  • Wanaofanya kazi katika viwanda vya utengenezaji matairi
  • Wachimbaji wa madini hususani aina ya cadmium
  • Walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama
Pamoja na kwamba, tatizo la kukua na kuongezeka kwa tezi dume yaani BPH hutokea kwa wanaume wengi, hali hiyo haiongezi uwezekano/hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
Dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?

Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na

  • Kupata shida unapoanza kukojoa
  • Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa
  • Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  • Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  • Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
  • Kutoa mkojo uliochanganyika na damu
  • Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu za jirani ya mwili, mgonjwa anaweza kuwa na

  • Maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni
  • Uume kushindwa kusimama (uhanithi)
  • Aidha, mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu n.k
Vipimo gani vitathibitisha kuwa nina saratani ya tezi dume?
Utambuzi wa saratani ya tezi dume hujumuisha kufahamu historia ya mgonjwa pamoja na familia yake, kufahamu dalili alizo nazo mgonjwa pamoja na kufanya vipimo kadhaa. Vipimo vinavyoweza kufanywa ni pamoja na

  • Digital rectal exam: Daktari ataingiza kidole cha shahada katika puru (rectum) ili kuhisi tezi dume kupitia ukuta wa puru. Aidha atahisi pia sehemu zote zinazozunguka tezi dume kutambua iwapo tezi ni ngumu au kama ina uvimbe wowote.
  • Kipimo cha damu kuchunguza Prostate Specific Antigen (PSA): PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume. Uzalishaji wake huongezeka wakati wa BPH, tezi dume inapopata uambukizi (prostitis) , na saratani ya tezi dume.
DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au BPH. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa.

  • Prostate biopsy: Kipimo hiki hufanywa kwa kuchukua kipande cha nyama (tishu) kutoka tezi dume kwa ajili ya uchunguzi maabara.
Kipimo kingine huitwa transrectal ultrasound ambacho husaidia kuonesha ukubwa na sura ya tezi dume lilivyo.
Ili kutambua kama saratani imesambaa sehemu nyingine za mwili vipimo vya CT scan, MRI pamoja na PET navyo vyaweza kufanyika pia.
Saratani ya tezi dume inatibika?
Ndiyo! Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika.
Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi, wakati kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri kumfuatilia mgonjwa kwa ukaribu bila kumfanyia upasuaji au bila kumpatia tiba ya mionzi.
Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu (hormonal therapy), au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).
Upasuaji

Upasuaji hufanyika kwa wagonjwa walio katika hatua za awali za ugonjwa (stage I na stage II) ingawa pia hufanywa kwa baadhi ya wagonjwa walio katika hatua za mwisho za ugonjwa huu yaani stage III na stage IV. Upasuaji unaofanywa ni ule wa kuondoa tezi dume pamoja na baadhi ya tishu zinazozunguka tezi hiyo.
Tiba ya Mionzi

Hii ni aina ya tiba inayotumia mionzi kuua seli zenye saratani. Tiba ya mionzi hutumika kutibu saratani ya tezi dume ambayo haijasambaa kwenye sehemu nyingine za mwili. Aidha inaweza pia kutumika kuua masalia ya tishu zenye saratani mara baada ya kufanyika kwa upasuaji.
Kwa wagonjwa walio katika hatua ya mwisho ya saratani yaani wale ambao saratani tayari imeshasambaa mwilini, mionzi hutumika kupunguza maumivu makali ya mifupa.
Madhara anayoweza kupata mgonjwa kutokana na aina hii ya tiba ni pamoja na kushindwa kusimamisha uume au uhanithi, kukosa hamu ya kula, uchovu, ngozi kubabuka, kuharisha na kutoa mkojo uliochanganyika na damu.
Tiba ya Homoni

Hii ni aina ya tiba inayotumia dawa zinazopunguza kiwango au ufanyakazi wa homoni ya testosterone mwilini. Testosterone ni homoni ya kiume inayochochea ukuaji wa tezi dume, hivyo basi matumizi ya dawa hizi husaidia kupunguza ukuaji huu na kusambaa kwa seli za saratani.
Tiba ya homoni hutolewa kwa wanaume walio katika hatua za mwisho za ugonjwa huu kwa nia ya kupunguza maumivu na kutibu dalili za ugonjwa. Dawa zinazotumika kwa tiba ya aina hii zimegawanyika katika makundi mawili, zile zinazochagiza uzalishaji wa homoni ya luteinizing (luteinizing hormone-releasing hormones, LH-RH) kwa mfano goserelin, nafarelin na leprolide; na zile zinazozuia ufanyaji kazi wa homoni yaandrogen kwa mfano flutamide, bicalutamide na nilutamide.Madhara yanayoweza kusababishwa na utumiaji wa dawa hizi ni pamoja na kichefuchefu na kutapika, upungufu wa damu, kuongezeka uzito, uhanithi na kukosa hamu ya tendo la ngono, matatizo katika ini na matiti kuwa makubwa.
Baadhi ya madaktari hutumia upasuaji wa kuondoa korodani kama njia ya kupunguza kiwango cha homoni za kiume mwilini kwa kigezo kwamba kiwango kikubwa cha homoni hizi huzalishwa kwenye korodani. Hata hivyo tiba hii haifanyiki mara kwa mara.
Baada ya matibabu?

Baada ya matibabu, mgonjwa wa saratani ya tezi dume hufuatiliwa kwa ukaribu kuhakikisha kuwa saratani haisambai sehemu nyingine za mwili. Ufuatiliaji hujumuisha mgonjwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara pamoja na kupima PSA kwa kipindi cha miezi mitatu mitatu mpaka mwaka mmoja.

Saratani ya Tezi Dume - Chanzo na Tiba
 
MAAMBUKIZI YA TEZI DUME (PROSTATITIS) SEHEMU YA PILI

Maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria (Chronic non-bacterial prostatitis)

Kama jina lake linavyoeleza, maambukizi ya aina hii kwenye tezi dume husababishwa na msongo wa mawazo, matatizo katika vichocheo vya mwili (homoni) na hata matatizo katika mfumo mzima wa neva.Pia kumekuwepo na dhana ya kwamba maambukizi ya aina hii huchangiwa na kuwepo kwa

maumivu ya kibofu cha mkojo yanayotokana na maambukizi katika kibofu hicho (Cystitis)au hali ya hewa hususan baridi ambayo huongeza maumivu ya tezi dume na hali ya joto ambayo hupunguza maumivu hayo. Baridi pia huchangia kujirudia kwa dalili na viashria vya maambukizi haya.

Katika utafiti uliofanyika kaskazini mwa nchi ya Finland (nchi ambayo ina majira ya baridi kali sana),umeonyesha ya kuwepo kwa maambukizi ya aina hii yanayoambatana na dalili na viashiria vyake kali sana kuliko sehemu yoyote duniani.
Maambukizi haya ya tezi dume bila uwepo wa bakteria hutokea kwa wanaume walio katika umri wa miaka 35-45 na inakisiwa kutokea kwa asilimia 90-95 ya maambukizi yote ya tezi dume .

Kuna aina mbili kuu za maambukizi haya ambazo ni:
1.Maambukizi haya yanayoambatana na mcharuko (Inflammatory Chronic Prostatitis/Chronic Pelvic Pain Syndrome)
2.Maambukizi yasiyokuwa na mcharuko (Non-infalmmatory chronic prostatitis, CP/Chronic Pelvic Pain Syndrome au CPPS)

Nini hasa hutokea wakati wa maambukizi haya?

Kukosekana kwa udhibiti wa mfumo wa neva mwilini kutokana na kuwepo kumbukumbu za maumivu yoyote (past trauma), maambukizi kwenye tezi dume, mrundikano wa kemikali tofauti tofauti na kuwepo kwa hali ya kuvutika kwa neva za kwenye nyonga husababisha mcharuko (inflammation)

katika tezi dume unaosababishwa na kutolewa kwa wingi kwa kemikali aina ya substance P(kutoka kwenye msihipa ya neva) ambayo ndio husababishwa kutolewa chembechembe zinazosababisha mcharuko mwili (mast cells) kwa wingi na matokeo yake ni kuathiri tezi dume pamoja na viungo vilivyokaribu yake kama kibofu cha mkojo, mpira wa kupitisha mkojo (urethra),korodani nk.

Dalili na viashiria vya maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria
•Maumivu makali ya kwenye sehemu za siri au kwenye nyonga kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu bila kuwepo kwa maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI)
•Maumivu haya makali yanaweza kuenea hadi kwenye mgongo kwa chini, kwenye puru (rectum) na kumfanya mgonjwa kushindwa kukaa chini/ kwenye kiti.

•Maumivu wakati wa kukojoa
•Maumivu katika jointi za mifupa
•Maumivu ya misuli (myalgia)
•Maumivu ya tumbo
•Uchovu usioelezeka
•Kichomi kwenye uume/dhakari (constant burning pain in the penis)
•Maumivu ya mara kwa mara kwenye nyonga, korodani au kwenye puru (rectum) bila uwepo wa maambukizi kwenye kibofu cha mkojo

•Maumivu wakati wa kutoa shahawa (wakati wa kujamiana)
•Kukojoa mara kwa mara
•Maumivu baada ya kutoa shahawa (baada ya kujamiana) ni dalili kubwa ya maambukizi haya
•Kupungua hamu ya kufanya mapenzi
•Kushindwa kujamiana vizuri (sexual dysfunction)
•Kushindwa kusimika/kudisa (jogoo kushindwa kupanda mtungi)- Erectile dysfuction

Vipimo vya uchunguzi
Hakuna kipimo maalum cha kuchunguza maambukizi haya ya tezi dume.

Vipimo vinavyoweza kusaidia katika uchunguzi wa maambukizi haya ni pamoja na
•kipimo cha kuangalia shahawa (semen analysis)
•kipimo cha kuangalia wingi wa cytokines kutoka kwenye majimaji ya tezi dume
•Vipimo vya kuangalia viashiria vya mcharuko(inflammation) kama cytokines,myeloperoxidases na chemokines
Inflammatory CP/CPPS huambatana na kuwepo kwa seli za usaha (pus cells) kwenye mkojo, shahawa na kwenye majimaji ya tezi dume wakati Non inflammatory CP/CPPS haina seli hizi za usaha kwenye mkojo, shahawa na majimaji ya tezi dume.Kielezo hiki si kigezo cha kutumika kama kipimo cha kuchunguza maambukizi haya.

Seli za usaha (pus cells) huwa ni chembechembe za damu nyeupe zilizokufa.

Matibabu ya maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria
Maambukizi haya sio rahisi kutibu kwani hakuna tiba maalum inayokubalika na wataalamu wa afya.
Lengo kuu la matibabu ya maambukizi haya ni kupunguza mvutano unaosababishwa na kuvutika kwa misuli ya nyonga na ya kwenye puru ,

kupunguza msongo wa mawazo na vichangizi vya msongo huu wa mawazo.
Miongoni wa matibabu yanaweza kusaidia ni pamoja na:
•Kujua chanzo cha msongo wa mawazo/wasiwasi(panic disorder) au taharuki na kumsaidia mgonjwa kuepuka vichagizi hivi
•Ushauri nasaha pamoja na kumhakikishia mgonjwa ya kwamba hali yake itatengemaa
•Kumuona daktari wa magonjwa ya akili
•Kufanya mazoezi ya yoga ili kufanya nyoga pamoja na mishipa ya neva ya nyoga na misuli kuwa katika hali tulivu(relaxation)
•Massage ya tezi dume (Digital prostate massage)
•Mazoezi ya viungo kwa wale ambao bado hawajafikia hatua ya kupata maumivu makali (Chronic Fatigue Syndrome)

•Dawa za kupunguza msongo wa mawazo kama antidepressants, benzodiazipines nk.
•Dawa za antibiotiki na alpha blockers hazijatoa matokeo ya kuridhisha katika uponyaji wa maambukizi haya
•Tiba ya acupuncture imeonyesha kuwapa unafuu baadhi ya wagonjwa

Wanaume wenye maambukizi haya ya tezi dume wako kwenye hatari ya kupata tatizo la maumivu makali sana (Chronic fatigue syndrome) na ugonjwa wa Irritable Bowel Syndrome( unaoambatana na maumivu ya tumbo, tumbo kuwa kubwa, kuharisha mara kwa mara au kutopata haja kubwa, msongo wa mawazo, wasiwasi, kuharisha damu na nk).

Prostate glands(matatzo ya kibofu cha mkojo) imekuwa ikisumbua wanaume wengi sana.Baadhi ya tiba zake ni TIBA YA HOMONI,UPASUAJI N.K.Madhara yanayo mpata mtu kwa upasuaji ni,kupoteza damu nyingisana,mwili kuwa dhaifu kwa mda,kutolewa tezi,kupungua kwa nguvu za kiume,pia husababisha kifo kwa watu walio na presha.Kiukweli unapofanyiwa upasuaji wa tezi unakuwa unapoteza kiungo mhimu katika mwili,maana kazi ya tezi ni kutengeneza majamaji yanayobeba shahawa.je tezi zikitolewa mtu huyo anakuwa na haligani kwa upande wa kizaz???Nina dawa inayotibu matatzo hayo ya tezi,ni dawa nzurisana ya mitishamba kwa aliye na tatyo hili anitafuta kama anaitaji tiba.iwe mkojo unatoka kidogokidogo,mfululizo,hata kama mgonjwa anacatheta miaka mingapi atapona.kama kuna mtu alisha fanyiwa upasuaji na tatzo likajirudia tena mwambie askate tamaa dawa zipo na zinatibu.kwa meng zaid ntafute.0759217720
 
Wadau !
Habari zenyu .
Kiukweli kiswahili cha kibaolojia hakijawahi kuwa na urafiki nami .
Sielewi TEZI DUME ni tezi gani .

Aidha sielewi linahusika kuwepo pande ipi ya mwili wa Binadamu .
Naomba kuelimishwa.

===========================================================
Mengi yamesemwa kuhusu saratani za aina mbalimbali katika jamii na athari zake kwa maisha ya binadamu.
Pia, zimekuwa zikitajwa aina mbalimbali za saratani ambazo zinawasumbua wengi katika jamii yetu.

Miongoni mwake ni ile ya tezi dume ambayo wanataalam wanaeleza kuwa inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vingi nchini.
Pia, wanaume wanaokunywa pombe kupita kiasi na wale wanaofanya kazi viwandani wakitajwa kuwa katika hatari zaidi ya saratani hii.

Imeelezwa kuwa wanaume wanaofanya kazi katika viwanda vya rangi au wanaofanya kazi za kupaka rangi wamo hatarini zaidi.
Hata hivyo, saratani ya aina hii kwa wanaume inashika nafasi ya kwanza kwa kusababisha vifo vingi hapa nchini.

Aidha,saratani ya tezi dume ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wa umri miaka 70 na kuendelea.

Hata hivyo, ni nadra kwa saratani hii kuwapata wanaume chini ya umri wa miaka 40.
Mwathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume ya ‘50 Plus Campaign' Dk Emmanuel Kandusi anasema saratani hii ikitambuliwa mapema huweza kutibika.

Anasema "Kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari hapa Tanzania, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20,"

Kwa kawaida saratani ya aina hii hukua taratibu ingawa baadhi hukua kwa kasi. Seli za saratani wakati mwingine husambaa katika maeneo mengine ya mwili hasa katika mifupa na tezi za limfu.

Saratani hii inasababisha maumivu makali hasa wakati wa kukojoa.
Wengi hushindwa kushiriki tendo la ndoa, au kukosa kabisa nguvu za kiume.

Watu walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na:

• Wanaume wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na Wazungu
• Wanaume kuanzia miaka 60 na kuendelea.
• Wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani, wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba amewahi kuugua ugonjwa huu.
• Wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali.
• Wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi.
• Wachimbaji wa madini, hususan aina ya cadmium.
• Walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama.

Mtandao wa Wikipedia unaeleza kuwa tafiti ziliwahi kufanyika na kubaini kuwa watu waliowahi kufanya mapenzi katika umri mdogo wapo katika hatari ya kupata saratani hii.

Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa magonjwa ya zinaa huweza kusababisha baadhi ya kesi za saratani hii.

Dalili za saratani ya tezi dume:

Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na;

• Kupata shida unapoanza kukojoa
• Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.
• Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
• Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
• Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
• Kutoa mkojo uliochanganyika na damu
• Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu

Vipimo vya saratani ya tezi dume:

Utambuzi wa saratani ya tezi dume hujumuisha kufahamu dalili alizo nazo mgonjwa pamoja na vipimo

Digital Rectal Exam: Daktari ataingiza kidole cha shahada katika puru (rectum) ili kuhisi tezi dume kupitia ukuta wa puru. Aidha, atahisi pia sehemu zote zinazozunguka tezi dume kutambua iwapo tezi ni ngumu au kama ina uvimbe wowote.

Aidha, kipimo hiki ni rahisi na kisicho na gharama kuweza kugundua tatizo mapema lakini kimekuwa kikipata upinzani mkubwa toka kwa wagonjwa kutokana na imani potofu na kutokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu kipimo hiki wakidhani ni cha udhalilishaji wa uanaume wao.

•Kipimo cha damu kuchunguza Prostate Specific Antigen (PSA): PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume. Uzalishaji wake huongezeka wakati wa BPH, tezi dume inapopata uambukizi (prostitis) , na saratani ya tezi dume.

DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume, lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au BPH. Hivyo, basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa.

• Prostate biopsy: Kipimo hiki hufanywa kwa kuchukua kipande cha nyama (tishu) kutoka tezi dume kwa ajili ya uchunguzi maabara.

Kipimo kingine huitwa ‘trans-rectal ultrasound' ambacho husaidia kuonyesha ukubwa na sura ya tezi dume lilivyo.

Ili kutambua kama saratani imesambaa sehemu nyingine za mwili vipimo vya CT scan, MRI pamoja na PET navyo vyaweza kufanyika pia.

Chanzo: Mwananchi
 
Wadau !
Habari zenyu .
Kiukweli kiswahili cha kibaolojia hakijawahi kuwa na urafiki nami .
Sielewi TEZI DUME ni tezi gani .

Aidha sielewi linahusika kuwepo pande ipi ya mwili wa Binadamu .
Naomba kuelimishwa .

Wanalazimisha lugha kwa kuipeleka kwa kasi bila utafiti wa kisayansi. What are the etimological origin of these words. nami huwa sipati ladha yake hata kidogo
 
Wewe hujui tezi dume? Ni litezi linatokea mkono wa kulia halafu linavimba sana na maumivu makali.

Tezi jike hutokea mkono wa kushoto, uvimbe huwa mdogo na maumivu kidogo.

Hayo ndo matezi dume na jike. Usikonsoe.....
 
Kiongozi mwanawao , asante kwa elimisho .
But hujanikidhisha kuelewa.
Tezi mkono wa kushoto (kama usemavyo)
Sasa mkono wa kushoto kwapani? Kiwikoni ?
Kiganjani ?
Vidoleni ?
 
Last edited by a moderator:
jamani mbona waoga waoga hivi kulijibu hili swali, leteni majibu maana tupo wengi hapa tusiofahamu hii tezi dume
 
- Tezi la uzazi la kiume (Prostate)- ni moja ya tezi la uzazi, lilopo chini ya kibofu cha mkojo, mbele ya utumbo.- Inauzunguka mpira unaootoa mkojo toka kwenye kibofu kwenda kwenye uume.
- Inatengeneza majimaji meupe yanayotengeneza asilimia kubwa ya shahawa (haitengenezi shahawa)

Pia, zimekuwa zikitajwa aina mbalimbali za saratani ambazo zinawasumbua wengi katika jamii yetu.Miongoni mwake ni ile ya tezi dume ambayo wanataalam wanaeleza kuwa inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vingi nchini.

Pia, wanaume wanaokunywa pombe kupita kiasi na wale wanaofanya kazi viwandani wakitajwa kuwa katika hatari zaidi ya saratani hii.

Imeelezwa kuwa wanaume wanaofanya kazi katika viwanda vya rangi au wanaofanya kazi za kupaka rangi wamo hatarini zaidi.

Hata hivyo, saratani ya aina hii kwa wanaume inashika nafasi ya kwanza kwa kusababisha vifo vingi hapa nchini.

Aidha,saratani ya tezi dume ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wa umri miaka 70 na kuendelea.

Hata hivyo, ni nadra kwa saratani hii kuwapata wanaume chini ya umri wa miaka 40.
Mwathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume ya ‘50 Plus Campaign' Dk Emmanuel Kandusi anasema saratani hii ikitambuliwa mapema huweza kutibika.

Anasema "Kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari hapa Tanzania, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20,"

Kwa kawaida saratani ya aina hii hukua taratibu ingawa baadhi hukua kwa kasi. Seli za saratani wakati mwingine husambaa katika maeneo mengine ya mwili hasa katika mifupa na tezi za limfu.

Saratani hii inasababisha maumivu makali hasa wakati wa kukojoa.
Wengi hushindwa kushiriki tendo la ndoa, au kukosa kabisa nguvu za kiume.

Walioko hatarini kupata saratani ya tezi dume
Watu walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na:
• Wanaume wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na Wazungu
• Wanaume kuanzia miaka 60 na kuendelea.
• Wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani, wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba amewahi kuugua ugonjwa huu.
• Wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali.
• Wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi.
• Wachimbaji wa madini, hususan aina ya cadmium.
• Walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama.

Mtandao wa Wikipedia unaeleza kuwa tafiti ziliwahi kufanyika na kubaini kuwa watu waliowahi kufanya mapenzi katika umri mdogo wapo katika hatari ya kupata saratani hii.
Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa magonjwa ya zinaa huweza kusababisha baadhi ya kesi za saratani hii.

Dalili za saratani ya tezi dume

Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na
• Kupata shida unapoanza kukojoa
• Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.
• Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
• Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
• Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
• Kutoa mkojo uliochanganyika na damu
• Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu

Vipimo vya saratani ya tezi dume
Utambuzi wa saratani ya tezi dume hujumuisha kufahamu dalili alizo nazo mgonjwa pamoja na vipimo

Digital Rectal Exam: Daktari ataingiza kidole cha shahada katika puru (rectum) ili kuhisi tezi dume kupitia ukuta wa puru. Aidha, atahisi pia sehemu zote zinazozunguka tezi dume kutambua iwapo tezi ni ngumu au kama ina uvimbe wowote.
 
Wadau !
Habari zenyu .
Kiukweli kiswahili cha kibaolojia hakijawahi kuwa na urafiki nami .
Sielewi TEZI DUME ni tezi gani .

Aidha sielewi linahusika kuwepo pande ipi ya mwili wa Binadamu .
Naomba kuelimishwa .

Ni pumbu moja kuwa kubwa zaidi ya ingine, bila kuikata shipa linaota dizaini ya boga. Na mara nyingi haya matezi yanasababishwa na magonjwa ya zinaa haswa ngono zembe.
 
Back
Top Bottom