Kuvamiwa kwa Ofisi za Mwanahalisi na Polisi

Kuna serikali mbili; inayoongozwa na JK na ile inayoongozwa na mafisadi, chini ya EL na RA .... hao askari wametumwa na serikali ya EL na RA

Kuna sirikali moja tu ya MAFISADI maana hatuoni tofauti yoyote kati ya serikali ya JK na hiyo ya mafisadi. Kinachotendeka sasa hivi ndicho ambacho mafisadi wanakitaka na JK kakaa kimya bila hata kutoa mguno
 
Nadhani mwanasheria wake anaweza kufanya hivyo..Ama kama nimekosea wanasheria wanirekebishe hapa.

So kama raia tu wa kawaida mwenye interest na wala sio mwanasheria siwezi pewa na mahakana siyo? that means hii information siyo public then?
 
Mkuu Kasheshe,

Heshima mbele, hapa nimekusikia sasa naomba tena kukuuliza one more question, una maana kuwa haya unayosema yamefanyika je ni within sheria na katiba ya Jamhuri yetu?

Meaning mahakama kumauru wananchi wapekulwe majumbani mwao au kwenye makazi yao, kwa amri ya mahakama bila kujua sababu na kwamba sababu wataambiwa baadye huko mahakamani kwenyewe, unasema hii ni within sheria na katiba ya Jamhuri yetu?

Na hakuna kosa la kisheria lililofanyika hapa? au?

Mkuu wangu definition ya "within the framework of our constitution" ni ngumu sana. Kuna vipengele vingi vya kijinga sana Rais, RC, DC wanaweza kutoa decree yoyote ambayo ni unconstitutional na inayokwenda kinyume na sheria lakini ikakubalika. Kwa hiyo weather Mahakama inatoa search warrant au hapana that is not the question, kwa hiyo la muhimu hapa ni kuangalia ni nini kimewapeleka kuwa harass kina kubenea. Kungekuwa na legak system nzuri hata polisi wanaweza kushitakiwa, lakini sijui kama kina kubenea wanaweza kufanya hili.
 
Makachero wavamia MwanaHalisi

na Martin Malera
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MAKACHERO wa polisi jana walivamia ofisi za gazeti la kila wiki la MwanaHalisi na kisha wakafanya upekuzi mkali nyumbani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea.

Hatua hiyo ya kushtukiza na isiyotarajiwa ilifanywa jana jioni na makachero hao wa polisi waliokuwa wamevaa nguo za kiraia na ambao walidai kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Tukio hilo linakuja miezi michache tu baada ya kundi la watu wasiojulikana kuvamia ofisi za gazeti hilo na kumjeruhi kwa mapanga, Mhariri Mshauri wa gazeti hilo, Ndimara Tegambwage na kuwamwagia kitu kinachoaminika kuwa tindikali yeye na Kubenea.

Tukio hilo lilisababisha wanahabari hao wawili kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na siku chache baadaye, Kubenea akapelekwa India ambako alifanyiwa upasuaji wa macho kwa nyakati mbili tofauti katika hospitali maarufu ya Apollo iliyoko Delhi.

Katika tukio la jana, makachero hao wakiwa na gari lao, walianza kuvamia ofisi ya MwanaHalisi iliyoko Kinondoni, nyumba namba 51/37A, Mtaa wa Kasaba, majira ya saa 9:00 alasiri na kuanza kupekua nyaraka mbalimbali na kisha kuwasha kompyuta moja baada ya nyingine wakitafuta taarifa ambazo hadi sasa hazijulikani ni za nini.

Hata hivyo, kazi ya kuanza kupekua nyaraka hizo ilichelewa baada ya Kubenea mwenyewe kuwataka polisi kufanya kazi hiyo wakati mwanasheria wa MwanaHalisi, Godfrey Mapunda akiwapo.

Katika tukio hilo lililovuta hisia za majirani, hata kusababisha mfanyakazi mmoja wa gazeti hilo la MwanaHalisi aliyejulikana kwa jina moja la Jaffari kupandwa na shinikizo la damu, na hivyo kusababisha akimbizwe katika zahanati moja Kinondoni.

Baada ya upekuzi huo, askari hao walikwenda nyumbani kwa Kubenea anayeishi Temeke wakiwa wamebeba moja ya kompyuta za Kampuni ya Hali Halisi Publishers.

Akizungumza na Tanzania Daima, Kubenea alisema makachero hao ambao hawakusema malengo yao, pamoja na kuonyesha kuwa na hati ya kufanya upekuzi, walisema wamefika kutafuta nyaraka moja ya siri ambayo hata hivyo hawakuitaja.

"Hawajasema ni nini hasa wanatafuta, lakini niliwazuia hadi mwanasheria wetu alipofika, ndipo kazi ya upekuzi ilipoanza.

"Mimi ni mpambanaji, siogopi kitu, na siamini kama nina nyaraka ya siri. Hii ni aina nyingine ya vitisho ili tuache kuandika yale ambayo serikali inafikiri ni mabaya," alisema Kubenea wakati akihojiwa na Tanzania Daima mbele ya polisi hao.

Alisema baada ya kushindwa kupata kile walichokuwa wakikitafuta, makachero hao walichukua maandishi yaliyokuwa katika kompyuta waliyoichukua ofisini, wakitumia kinyonyeo ‘flash', wakisema walikuwa wakitaka kwenda kuyatumia katika uchunguzi wao.

Tanzania Daima ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kuzungumzia tukio hilo kupitia simu yake ya mkononi, hakuweza kupatikana licha ya simu hiyo kuita muda mrefu bila kupokelewa, kabla ya kuzimwa kabisa muda mfupi baadaye.

Tangu kuanzishwa kwake zaidi ya miaka miwili iliyopita, MwanaHalisi limejipambanua kama gazeti linalofichua masuala ya ufisadi, utawala bora ndani ya serikali na hususan katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kutokana na habari na makala zake, mara kadhaa Kubenea amepata kukaririwa akisema kwamba amekuwa akipokea vitisho vya namna mbalimbali dhidi yake vinavyofanywa na watu wasiojulikana kupitia ujumbe wa simu ya mkononi.

Akizungumza na Tanzania Daima kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datoo alilaani upekuzi huo na akauelezea kuwa mfano wa matukio yanayotishia ustawi na uhuru wa habari hapa nchini.

"Nikiwa ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, nimesikitishwa sana na tukio hili la kupekua chumba cha habari cha MwanaHalisi na nyumbani kwa mkurugenzi wake, ambaye ni mmoja wa wanachama wetu," alisema Datoo.

Alisema kwa kuwa Kubenea hafahamu sababu ya upekuzi huo, ambao kimsingi unatishia uhuru wa habari, Jukwaa la Wahariri litahakikisha vitisho vya namna hii vinakomeshwa, si kwa MwanaHalisi tu, bali kwa vyombo vyote vya habari.
 
Mkuu wangu definition ya "within the framework of our constitution" ni ngumu sana. Kuna vipengele vingi vya kijinga sana Rais, RC, DC wanaweza kutoa decree yoyote ambayo ni unconstitutional na inayokwenda kinyume na sheria lakini ikakubalika.

Naomba kutofautina na wewe hapa mkuu, hizi ni sheria ambazo tumetoka nazo uhuru, mpaka leo zimetutunza sisi wengine mpaka tumekuwa watu wazima na sasa hivi tuna-function kama bina-adam wengine wote dunaini,

ukweli ni kwamba hizi zilikuwa sheria za utawala wa chama kimoja, sasa tulipoingia utawala wa vyama vingi ulikuwa ni wajibu wa waasisi wa upinzani, kudai zibadilishwe, kwa sababu tunaingiaje kwenye siasa za vyama vingi na sheria za chama kimoja kwenye taifa?, lakini kuziita kuwa ni sheria za kijinga hulitendei hakia taifa na sisi wananchi wengine tunaoheshimu uzalendo wetu,

Sheria zimepitwa na wakati hilo halna mjadala, lakini kuziita kuwa ni za kijinga ni way much over the line!

Kwa hiyo weather Mahakama inatoa search warrant au hapana that is not the question,

Hapana it is a question tena a valid one, kwa sababu mahakama imeandika warrant basi ni valid kwa mujibu wa katiba, huko US zamani ilikuwa hivyo hivyo kwa polisi mpaka wakapate warrant kutoka kwa mahakama, siku hizi wamebadili hiyo, polisi wanayo haki ya kukusimamisha barabarani na wakiamini kuwa wana probable course, wanakusachi na watakachopata ni valid as legal evidence against a criminal,

Zamani huko US, kama polisi wamepwaa warrant ya kukupekua kama una bangi na mahakama, wakikukuta na cocaine, haiwezi kukubaliwa na mahakama kama ushahidi, lakini hayo yote siku hizi yamebadilishwa baada ya September 11, sasa na sisi bongo tunahitaji mabadiliko ya katiba, lakini until then bado sheria zetu ni valid kwenye mkono wa sheria!

kwa hiyo la muhimu hapa ni kuangalia ni nini kimewapeleka kuwa harass kina kubenea. Kungekuwa na legak system nzuri hata polisi wanaweza kushitakiwa, lakini sijui kama kina kubenea wanaweza kufanya hili.

Polisi hawawezi kushitakiwa kwa prosecute a valid search warrant, tatizo so far ni sababu ipi iliyowafanya wawapekue, lakini as far as kitendo cha kuwapekua, kiko valid kabisa under sheria zetu, kwa sababu kibali kimetolewa na mahakama, na hiyo inairidhisha katiba yetu, Imean wakati tunajaribu kuwa pamoja na ndugu zetu kina Kubenea, tusije tukawaponza na maneno yasiyokuwa na uhakika!
 
Akizungumza na Tanzania Daima, Kubenea alisema makachero hao ambao hawakusema malengo yao, pamoja na kuonyesha kuwa na hati ya kufanya upekuzi, walisema wamefika kutafuta nyaraka moja ya siri ambayo hata hivyo hawakuitaja.

Maneno ni mazito sana haya, lakini bado tunahitaji kujua ukweli wa sababu.
 
Naomba kutofautina na wewe hapa mkuu, hizi ni sheria ambazo tumetoka nazo uhuru, mpaka leo zimetutunza sisi wengine mpaka tumekuwa watu wazima na sasa hivi tuna-function kama bina-adam wengine wote dunaini,

ukweli ni kwamba hizi zilikuwa sheria za utawala wa chama kimoja, sasa tulipoingia utawala wa vyama vingi ulikuwa ni wajibu wa waasisi wa upinzani, kudai zibadilishwe, kwa sababu tunaingiaje kwenye siasa za vyama vingi na sheria za chama kimoja kwenye taifa?, lakini kuziita kuwa ni sheria za kijinga hulitendei hakia taifa na sisi wananchi wengine tunaoheshimu uzalendo wetu,

Sheria zimepitwa na wakati hilo halna mjadala, lakini kuziita kuwa ni za kijinga ni way much over the line!

Hapana it is a question tena a valid one, kwa sababu mahakama imeandika warrant basi ni valid kwa mujibu wa katiba, huko US zamani ilikuwa hivyo hivyo kwa polisi mpaka wakapate warrant kutoka kwa mahakama, siku hizi wamebadili hiyo, polisi wanayo haki ya kukusimamisha barabarani na wakiamini kuwa wana probable course, wanakusachi na watakachopata ni valid as legal evidence against a criminal,

Zamani huko US, kama polisi wamepwaa warrant ya kukupekua kama una bangi na mahakama, wakikukuta na cocaine, haiwezi kukubaliwa na mahakama kama ushahidi, lakini hayo yote siku hizi yamebadilishwa baada ya September 11, sasa na sisi bongo tunahitaji mabadiliko ya katiba, lakini until then bado sheria zetu ni valid kwenye mkono wa sheria!

Polisi hawawezi kushitakiwa kwa prosecute a valid search warrant, tatizo so far ni sababu ipi iliyowafanya wawapekue, lakini as far as kitendo cha kuwapekua, kiko valid kabisa under sheria zetu, kwa sababu kibali kimetolewa na mahakama, na hiyo inairidhisha katiba yetu, Imean wakati tunajaribu kuwa pamoja na ndugu zetu kina Kubenea, tusije tukawaponza na maneno yasiyokuwa na uhakika!

Nakubaliana na wewe mkuu labda nimevuka mstari. Lakini naweza kukurudisha kidogo nyuma kuwa sheria zilizopo in principal sio za chama kimoja ila ni za kikoloni. Lengo lilikuwa ku-serve the purpose of a governor. Wakati wa kutoa uhuru kama utakumbuka kule Lancaster house walibadilisha majina tu governor kuwa waziri mkuu, na vipengele vingine vidogo vodogo lakini kimsingi contents za katiba mpaka leo zimebaki zile zile za mkoloni na zina-serve the same purspose, japokuwa vimewekwa viraka vingi ambavyo wakati fulani vinakinzana . Kama kun genuine ground within legal framework ya kutoa warrant na kwenda kum-search mtu hilo halina tatizo. Lakini what if fisadi anamsukuma Hakimu kutoa search warrant, what if the search is arbitrary serikali/polisi haiwezi kufikishwa mahakamani?
Au inapofika wakati serikali inafanya uhalifu kwa kisingizio fulani yenyewe haiwezi kufikishwa mahakamani?
Nakubaliana na wewe kuhusu kuwa waangalifu tusiwaponze waandishi makini wanaotusaidia kuifahamu nchi yetu vizuri.
 
Watanzania sasa tushaamka zile zama za kufuta watetea haki zinayeyuka.Mwanahalisi tuko nyuma yenu, mafisadi mtake msitake mwisho wenu umewadia
 
Nakubaliana na wewe mkuu labda nimevuka mstari. Lakini naweza kukurudisha kidogo nyuma kuwa sheria zilizopo in principal sio za chama kimoja ila ni za kikoloni. Lengo lilikuwa ku-serve the purpose of a governor. Wakati wa kutoa uhuru kama utakumbuka kule Lancaster house walibadilisha majina tu governor kuwa waziri mkuu, na vipengele vingine vidogo vodogo lakini kimsingi contents za katiba mpaka leo zimebaki zile zile za mkoloni na zina-serve the same purspose, japokuwa vimewekwa viraka vingi ambavyo wakati fulani vinakinzana . Kama kun genuine ground within legal framework ya kutoa warrant na kwenda kum-search mtu hilo halina tatizo. Lakini what if fisadi anamsukuma Hakimu kutoa search warrant, what if the search is arbitrary serikali/polisi haiwezi kufikishwa mahakamani?
Au inapofika wakati serikali inafanya uhalifu kwa kisingizio fulani yenyewe haiwezi kufikishwa mahakamani?
Nakubaliana na wewe kuhusu kuwa waangalifu tusiwaponze waandishi makini wanaotusaidia kuifahamu nchi yetu vizuri.

BongoLander hapo mzizi wa fitina umeukatilia mbali.
 
Katiba ndio kitu cha kwanza kabisa kinachotakiwa kufanyiwa marekebisho, tatizo serikali itasimama kidete kuhakikisha kuwa katiba haibadilishwi. Mambo mengi yanafanyika utaona ni interest za watu wachaceh na wala sio kwamba maslahi ya nchi au wananchi yanawekwa mbele. Kama hili la serikali kwenda mahakama ya rufaa kupinga uamuzi wa mgombea binafsi, hapa utajiuliza serikali inaenda kupinga kwa maslahi ya nani?
 
Mahakama za nchi zote daima ni neutral. Mahakama haiwezi kuamua kuwa nyumba ya Kishoka ipekuliwe mpaka kuwepo na mlalamikaji atakayetoa ushahidi kuwa anaamini Kisura wa Jasusi kafichwa nyumbani kwa Rev. Kishoka. Ukishatolewa ushahidi huo au sababu zinazopelekea kuamini hivyo ndipo mahakama inapoweza kutoa search warrant. So there must be someone high up who wanted Mwanahalisi offices searched.
 
Hivi mahakama zetu zinatoa search warranties au basi tuu police wanaexcute kutokana na mapenzi ya boss wao?
 
Wananchi inabidi kuwa makini kwa sababu polisi nao wanajichukuliaga sheria na kuanza kusearch. ishu zingine zinaudhi ni pale airport, mtu umeishaonga passport kisha unakaribia kutoka eti jamaa wa TRA wanakuja wanataka kuona passport yako.
 
Mahakama za nchi zote daima ni neutral. Mahakama haiwezi kuamua kuwa nyumba ya Kishoka ipekuliwe mpaka kuwepo na mlalamikaji atakayetoa ushahidi kuwa anaamini Kisura wa Jasusi kafichwa nyumbani kwa Rev. Kishoka. Ukishatolewa ushahidi huo au sababu zinazopelekea kuamini hivyo ndipo mahakama inapoweza kutoa search warrant. So there must be someone high up who wanted Mwanahalisi offices searched.

Jasusi ni lazima kuwe na uchunguzi unaoendelea ama kesi.
Na ni prosecuters wanaokwenda kuomba hiyo warrant kutoka mahakamani.
Na kabla hawajakubaliwa ni lazima waje na sababu za kutosha kwamba kuna ushahidi muhimu ambao wanahatari ya kuupoteza endapo hawata execute hiyo warrant.
Kwa hiyo hata kama there was someone high haina maana kuwa hakuna prosecuters ama hata sababu za warrant yao.
Tatizo pia bado liko kwasabau hata warrant yenyewe haikuwa na jina la kubenea bali mtu mwingine kabisa.
Hivyo kina Kubenea na mwanahalisi wanaweza kuwageuzia kibao.
 
Jmushi,

Nakubaliana na wewe kuwa kuna kesi au uchunguzi unaoendelea. Nafikiri by Monday tunaweza jua sheshe zima lilianzia wapi.
 
Hivi mahakama zetu zinatoa search warranties au basi tuu police wanaexcute kutokana na mapenzi ya boss wao?

Mkuu Icadon,

Umewezaje ku guess hicho kitu? Kama wewe sio Mwanasheria basi una gift ya ku guess.

Yani sheria inasema hivyo hivyo. Polisi wafuate mapenzi ya mabosi wao kupata search warrant.

Ni kituko!

Tatizo, Icadon, ni kwamba tumekataa kubadilisha sheria tulizorithi kwa watu ambao hata wenyewe wamesha zibadilisha. Wa Europe walipoenda kuanzisha America walikwenda na Sheria za Ufalme wa Uingereza, lakini siku hizi wanasema sheria karibu zote za Marekani zimeandikwa upya, statutory law, na sio tena common law ya Mwingereza. Sisi bado tunazo!

Hicho kitu ulichokisema hapo juu hiki hapa:

CRIMINAL PROCEDURE ACT 1985-9
Procudure Relating to Criminal Investigation

Power to issue Search Warrant

38.-(1) If a police officer in charge of a police station is satisfied that there is reasonable ground for suspecting that there is in any building, vessel, carriage, box, receptacle or place:
(i) anything with respect to which any offence has been committed;
(ii) anything in respect of which there are reasonable grounds to believe that it will afford evidence as to the commission of any offence;
(iii) anything in respect of which there are reasonable grounds to believe that it is intended to be used for the purpose of committing any offence, and the officer is satisfied that any delay would result in the removal or destruction of that thing, or would endanger life or property,

he may search or issue a written authority to any police officer under him to search the building, vessel, carriage, box, receptacle or place as the case may be.
 
Kuhani ndio maana tunasema hapa ni kweli sheria ni za kikoloni...Hilo tumeshakubali.

However..Bado tuna haki ya kuuliza sababu hizo ambazo huyo mkuu wa kituo alizitumia licha ya kwamba bado hatujajua kama thats the case.

Mg hapo juu amedai kuwa ni kweli kuna kesi kama nilivyokuwa niki guess.

Si unasema wanatakiwa wawe satisfied kuwa kuna resonable ground ya ku execute warrant?

Hiyo ndiyo tunaitaka...Kuwa ni kipi hicho kilichowapeleka kwa Kubenea na mwanahalisi headquaters huku wakiwa na warrant ya mtu anayeitwa Peter Msangi.

Tunataka kujuwa ni grounds gani hizo ambazo ni resonable kwenda kusachi kwa mtu mwingine ukiwa na warrant ya mtu mwingine.

Hata kama polisi akija kukusachi una haki ya kumuuliza anachotafuta.

Halafu pia naomba usipingane na kauli za wahusika wenyewe kuwa walionyeshwa warrant kutoka mahakama ya Kisutu.

Kwa hiyo hapa ni kuwapa moyo wafuatilie na haki itapatikana.
 
Back
Top Bottom