Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,119
- 9,049
Wakuu ninaomba kuelimishwa kwa wale ambao wanajua zaidi, tofauti iliyopo katika uvaaji kofia kwa wanajeshi.Kwa mfano wakati wa mazishi ya Mzee Kawawa, kuna wanajeshi waliokuwa wana kofia za kijani sawa na sare zao za kijeshi na wengine walivaa kofia nyekundu na sare za kijani.Je uvaaji huo wa kofia tofauti una maana yoyote au ni basi tu imetokea kuwa na mchanganyiko wa aina hiyo? Kama ndivyo nini tofauti kati ya wenye kofia za kijani na nyekundu?