Kuuza nyumba za Serikali ‘noma’

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Kama sikosei katika lile gazeti la THIS DAY mwaka juzi waliandika kwamba uamuzi wa kuuza nyumba za Serikali umeitia hasara Serikali za shilingi bilioni 200 and counting kutokana na gharama kubwa za kuwaweka mahotelini "eligible officers" pamoja na familia zao katika mahoteli mbali mbali nchini tena kwa kipindi kirefu.

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*
Kuuza nyumba za Serikali ‘noma’
Monday, 04 July 2011 20:56


Leon Bahati, Dodoma
Mwananchi

UAMUZI wa Serikali wa kuuza nyumba zake kwa ajili ya watumishi wake wakati wa awamu ya tatu sasa umegundulika kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuwagharamia viongozi wa juu kuishi hotelini.

Hayo yalibainika bungeni jana wakati Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Susan Lyimo akitoa hutuma yake kuhusiana na utendaji wa ofisi ya Rais.

Alisema kwamba Kambi ya Upinzani imechunguza na kubaini kuwa mmoja wa Mawaziri wa Serikali ya awamu ya nne ambaye alikuwa anaishi hotelini kwa miezi saba tangu aapishwe, ametumia Sh110.2 milioni za umma.

Hakumtaja waziri huyo, lakini hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsa Vuai Nahodha aliripotiwa kupatiwa nyumba baada ya kuishi hotelini kutokana na kukosa nyumba ya Serikali ya kuishi.

Susan alisema hayo akizingatia kuwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya kwanza na ya pili zilijengwa nyumba maalumu kwa ajili ya kuishi viongozi wa Serikali na watendaji wengine, lakini katika Serikali ya awamu ya tatu, iliamuliwa baadhi ya nyumba kuuzwa hivyo kuwafanya baadhi ya viongozi kukosa sehemu ya kuishi.

Susan alisisitiza, “wakati nyumba za Serikali zilijengwa na kuuzwa baadhi ya mawaziri kwa sasa wanakaa mahotelini. Kwa siku gharama ya hoteli ni Sh560,000”.

Aliendelea, “tukipiga hesabu ya kiongozi mmoja aliyekaa hotelini kwa miezi saba tangu aapishwe ni dhahiri Sh110.2 milioni zilitumika.”

Hivyo akahoji, “Je ni viongozi wangapi wanaokaa hotelini na mpaka sasa wameliingizia taifa hasara kiasi gani? Je Serikali imechukua hatua gani dhidi ya viongozi waliouza nyumba hizo?”

Maswali ya Susan ambaye aliyawasilisha kwa niaba ya kambi ya upinzani aliyauliza akitazamia kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia atayajibu wakati akifanya majumuisho ya hotuba yake ya kuomba bunge limuidhinishie Sh33.4 bilioni kwa ajili ya matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2011/12.

Susan hakuishia hapo bali aliendelea kuilaumu Ofisi hiyo ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma akisema imekuwa na uzembe unaosababisha matumizi mengi mabaya ya fedha za umma.

Akitumia ripoti ya Mdhibiti na Makaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali(CAG) alisema katika mwaka 2009/10 fedha za walipa kodi zipatazo Sh1.8 trilioni zilitumika kulipa mishahara kwa watumishi wa Serikali kuu waliostaafu, waliokufa na watoro kazini.

Kama hiyo haitoshi, akasema mwaka huo huo Sh583.2 milioni zilitumika kuwalipa wafanyakazi hewa, yaani waliostaafu, waliokufa na watoro wa Serikali za mitaa.

Wakati fedha hizo za umma zikitumika vibaya, Susan alisema kulikuwa na mishahara ya watumishi wa Serikali za mitaa ambayo haikulipwa na hazikurudishwa hazina inayofikia Sh1.1 bilioni.

Lawama nyingine ni Ofisi hiyo ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kushindwa kuweka kumbukumbu za wafanyakazi wake waliopo kazini, wanaoacha kazi na wanaofukuzwa.

Uzembe huo, akasema unasababisha matatizo hata katika kuwalipa wafanyakazi mafao yao pindi wanapostaafu au kufariki

Awali, naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana alisema ukosefu wa maadili kwa watumishi wa umma ni changamoto kubwa kwa Serikali hivi sasa, lakini akasema hilo linachangiwa na ukosefu wa elimu ya kizalendo.

 
ufisadi @ its best! wameuziana nyumba,na wanaendelea kuchakachua fedha! hata kama hakuna nyumba,kuna haja ya kuishi hotel for all that money and time? si wangepangisha way b4 kuteuliwa kwa mawaziri?hivi planners wanasomaga nn shule,manake hao mawaziri sio kama walikuja by surprise!
 
ufisadi @ its best! wameuziana nyumba,na wanaendelea kuchakachua fedha! hata kama hakuna nyumba,kuna haja ya kuishi hotel for all that money and time? si wangepangisha way b4 kuteuliwa kwa mawaziri?hivi planners wanasomaga nn shule,manake hao mawaziri sio kama walikuja by surprise!

King'asty ndio maamuzi ya nchi yetu ambayo yamejaa madudu kila kukicha na huku nchi ikizidi kudidimia. Haya ni matokeo ya fisadi Mkapa aliyetaka kukwapua nyumba za Serikali na hivyo kuona kwamba asipate pingamizi kali kutoka baraza la Mawaziri basi ikaamuliwa nyumba zile ziuzwe kwa bei ya kutupa na kuahidi kujenga mpya hadi hii leo hakuna nyumba mpya zilizojengwa na Serikali inazidi kuingia gharama kubwa za kuwaweka maofisa mbali mbali na familia zao mahotelini kwa gharama kubwa sana.
 
Unaweza kuacha kazi serikali na kwenda private sector, kumbe kuna mtu anaendelea kukinga mshahara wako kama vile bado upo.
 
shida yetu hatuhoji, na hata tukihoji tunapuuzwa! why nt build them houses b4 selling out? ni wazi ilikuwa kwa manufaa yao binafsi! why cant we handle the present situation ka kutumia akili? naona jinsi tutakavyopata shida kuwasimulia watoto wetu hadithi hizi, u hav to see to understand aisee!
King'asty ndio maamuzi ya nchi yetu ambayo yamejaa madudu kila kukicha na huku nchi ikizidi kudidimia. Haya ni matokeo ya fisadi Mkapa aliyetaka kukwapua nyumba za Serikali na hivyo kuona kwamba asipate pingamizi kali kutoka baraza la Mawaziri basi ikaamuliwa nyumba zile ziuzwe kwa bei ya kutupa na kuahidi kujenga mpya hadi hii leo hakuna nyumba mpya zilizojengwa na Serikali inazidi kuingia gharama kubwa za kuwaweka maofisa mbali mbali na familia zao mahotelini kwa gharama kubwa sana.
 
Nchi ya wendawazimu huongozwa na wendawazimu pia; sisi ni nchi ya wendawazimu. Mie bado ninatafuta mganga wa kunionodlea wendawazimu wangu unaonifanya niongozwe na wendawazimu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom