kuunga mkono Hoja kwa 100% bungeni inamaanisha nini?

Bebrn

Senior Member
Mar 20, 2008
103
23
ndugu zangu naomba mniambie maana halisi ya mbunge anaposema ameonga mkono hoja kwa 100% alafu baadae analalamika kuwa jimbo lake linamatatizo mengi na hayatatuliwi!! sasa hapa mm ndio sielewi maana ya kuunga mkono hoja kwa 100%
 
Yaani hawa wabunge wanakwenda kwa business as ussual kwa kweli wanaboa... sentensi zilezile miaka yote ili mradi posho imeingia mfukoni... nawachukia sana hawa nyinyiem:A S 13:
 
Sawli kama hili ndilo aliombea mwongozo mchungaji Peter Msingwa mbunge wa Iringa mjini, lakini kwa unazi wake yule mwenyekiti wa mbunge Jenista muhagana akampotezea!
 
Kuunga mkono hoja kwa wabunge wa sisiem ni kukubali kila itu ili usimuudhi mkuu......
ila kwa vyama vingine ni kukubaliana na hoja kama inakidhi matakwa ya yule aliyewatuma bungeni
 
kitu hiki ndio kinapoteza umuhimu wa bunge maana hakuna no ni yes yes hata kama unaumia!!!!!
 
Huwezi kuwa unaoppose kitu then mwisho unamalizia nasupport.
You can not be the opposser and at the same time supporter huo ni WOGA na USALITI kwa waliokutuma
 
ndugu zangu naomba mniambie maana halisi ya mbunge anaposema ameonga mkono hoja kwa 100% alafu baadae analalamika kuwa jimbo lake linamatatizo mengi na hayatatuliwi!! sasa hapa mm ndio sielewi maana ya kuunga mkono hoja kwa 100%

Huo ndio udhaifu wenyewe..Maana wanaanza kwa kulalamika sana, uku wakiikosoa bajeti yenyewe, mwisho wa siku unasikia naunga mkono....mie nadhani ni maelekezo waliyopewa na viongozi wao wa chama
 
Kuunga mkono 100% kwa 100% kwa wabunge CCM wakiwa Bungeni na baadaye kulalama majimbo yao hayana huduma maana yake ni kwamba tunakutii Bwana mkubwa mwenye shati la Kijani pamoja na chama chetu lakini waliotuchagua kutuleta Mjengoni tutawaridhisha kwa kugonga Meza na Vijembe kisha tutawapa fulana Khanga na kofia maisha bora kwa kila mtanzania, na sisi bila kujiuliza tuanawachagua kila ifakapo siku ya uchaguzi,Wabunge wenye tamaa ya maisha wasiowajali wenzao wanakula nini watoto wao wanasoma vipi shule wanapataje huduma za Hosptali????? yote haya wamesahau kabisa Kijana wetu Mchemba mtoto wa juzi anasema uchumi na bajeti ni nzuri.Kikubwa kinachotuponza ni Wtz wenzetu wanapokosea kukipa ridhaa ya kutawala chama Dhalimu. Mujwahuzia
 
Mi huwa nashangaa unakuta mbunge anapoonda bajeti alafu mwishoni anamalizia naunga mkono hoja mia kwa mia
 
Bunge linaangaliwa/kuzilizwa na watu wengi wakiwemo watoto wa shule, hivyo ni vema wabunge wakisaidiwa na Spika kurekebisha huu upofu wa kuunga hoja 100% na hapo hapo unaanza kukosoa! Inatufanya watanzania tuonekane kama hatuna elimu hata kidogo. Hivi unaweza kusema kwa mfano nyumba imekamilika 100% na hapo hapo ukasema bado vyumba kadhaa havijakamilika? Bado CCM wanaishi kwenye fikra za chama kimoja.
 
Wabunge wanaounga mkono bajeti kwa 100% kisha wanatoa matatizo yaliyo jimboni mwao au kuonesha kuwa bajeti imesahau wakulima na wavuvi wa jimboni kwa bwana Presha inapanda na kushuka ni wehu. Kimsingi kuikubali ni kutokuwa na dosari na kwa hivo inatakiwa waseme "naunga mkono hoja kwa 100% bila marekebisho yeyote au siiungi hoja kwa vile ina mapungufu haya na haya"
Wabunge wa upinzani wanafanya vizuri sana kama inavotakiwa.
 
Bora hiyo ya 100%. Jamani leo nimemsikia mbunge wa Kishapu akisema anaunga mkono kwa 300% nikabadilisha na station
 
Bora hiyo ya 100%. Jamani leo nimemsikia mbunge wa Kishapu akisema anaunga mkono kwa 300% nikabadilisha na station

teh teh teh sasa mtu kama huyo ni mzima kweli? mungu tuepushe na kama hao kuwa wabunge wetu tena
 
Ni hivi, moja ya theories za logic inasema "if one of the premises (not PROMISES) is negative, the conclusion must be negative. Nasema hivi kwa kuwa hawa WaBonge wa CCM wengi wao wanapinga mambo mengi ambayo yako katika budget, halafu wanaishia kuunga mkono hoja (ambayo ni conclusion). This is another silly action that the guys are doing. Kweli tumeruhusu ujinga (kutojua) utawale maarifa (akili)
 
ndugu zangu naomba mniambie maana halisi ya mbunge anaposema ameonga mkono hoja kwa 100% alafu baadae analalamika kuwa jimbo lake linamatatizo mengi na hayatatuliwi!! sasa hapa mm ndio sielewi maana ya kuunga mkono hoja kwa 100%

Another sill seson,bungeni wabunge Wa ccm ni mzigo kwa taifa hili kuthibitisha Hilo yupo mmoja leo kasimama na kabla ya kuchangia aliunga hoja kwa 300% na papo hapo akaanza kuelezea matatizo ya jimbo lake na matumizi mabaya ya fedha za umma.Vichwa lazima vituume watanzania kwa kusikilza pumba Kama hizo.
 
....wanaepuka kupinga sana bajeti coz wao wakipinga itapelekea mabadiliko makubwa ya kisiasa ikiwemo nchi kuingia katika uchaguzi before 2015 kitu ambacho wanachichiem wanogopa ukizingatia chadema imeshika hatamu sana sahv....huo ni udhaifu mkubwa ni lazma wajikubali na kubadilika sema ndo hivo uchu wa madaraka umewajaa wanaunga mkono hoja hovyohovyo tu...aagghhh
 
Back
Top Bottom