Kwa hiyo mnataka kusema nchi kama Namibia na Afrika Kusini nao wanyakue ardhi kutoka kwa wazungu? Hilo ndilo mnalotetea hapa? Nadhani watu wamesahau hapa kwamba ardhi sio ishu kwa Zimbabwe sasa. Ni Mugabe ametumia kisingizio hicho ili kubaki madarakani na kutafuta ushawishi wa nchi za kiafrika kumuunga mkono.
Hivi kaka Mkandara una habari kwamba sasa hivi kuna makampuni makubwa ya kichina, Saudi Arabia na canada yananunua mashamba makubwa dunia kote a na kuwekeza kwenye kilimo cha mazao ya chakula? Mfano mmoja ni Madagascar ambao hekari zaidi ya milioni 1 zimeshanunuliwa. Wakati watu wanafikiria kuwekeza katika kilimo sisi wengine na viongozi wetu (akina Mugabe) tunaongelea kuirudisha thamani ya ardhi katika enzi za ujima. Kwamba heri ibaki bure kuliko mzungu aitumie kuzalisha!
Sioni busara ya kumnyang'anya raia ardhi kutokana na rangi ya ngozi yake na kumpa raia mwingine asiye na rasilimali wala mtaji wa kuiendeleza, eti kwa sababu tu ni mweusi. Suala la ardhi kwa sasa ni la kiuchumi zaidi kuliko hapo awali tulipokuwa tunapigania uhuru ambapo lilikuwa ni la kisiasa. Huko tumeshatoka jamani. Watu wanataka ajira, nyumba bora, elimu bora na hospitali bora. Ardhi isiyo na tija sio lengo kwa sasa. It is just another white elephant!
Angalia Zimbabwe sasa, baada ya kupewa ardhi eti ndio wanakufa njaa! What a shame!