Kuuma masikio kwenye ndege

kussy

JF-Expert Member
Jun 15, 2010
400
121
Wadau naomba msaada mara nyingi nasafiri na ndege na mara zote masikio huuma sana, inasababishwa na nini na njia gani naweza kuzuia hali hii, mara zote hizo abiria wengine huwa wako normal.
 
Utofauti wa mkandamizo kati ya hewa iliyopo ndani ya sikio na hewa ya nje ndio sababu, hii
ni kutokana na utofauti wa mwinuko.
Jaribu kufungua na kufunga mdomo mithili ya kupiga mwayo.
Kama una "chewing gum", jaribu kutafuna.
Tumia vidole kuziba matundu ya sikio, huku ukiwa umebanua mdomo.
 
Nadhani wewe unapanda vile vindege vya TANAPA vya watu wa nne, nina imani kama unapanda ndege kubwa kubwa tatitizo hili halipo ama lipo kwa kiasi kidogo sana
 
Nadhani wewe unapanda vile vindege vya TANAPA vya watu wa nne, nina imani kama unapanda ndege kubwa kubwa tatitizo hili halipo ama lipo kwa kiasi kidogo sana

Nowadays naingia humu sana sio kwa kupata nyuzi only, ila kupunguza stress kwa wingi. Thank you mkuu bornagain
 
Last edited by a moderator:
Hata mimi nkipandaga Ngorika napata shida hii hivi tatizo nini jamanieeee, teh teh teh teh.
 
ndege ninazopanda mara nyingi ni caravan za watu 12
 
Utofauti wa mkandamizo kati ya hewa iliyopo ndani ya sikio na hewa ya nje ndio sababu, hii
ni kutokana na utofauti wa mwinuko.
Jaribu kufungua na kufunga mdomo mithili ya kupiga mwayo.
Kama una "chewing gum", jaribu kutafuna.
Tumia vidole kuziba matundu ya sikio, huku ukiwa umebanua mdomo.

Mtoa mada, fuata ushauri huu hapa, ndizo mbinu ninazotumia ninapokuwa na shida kama hiyo. Kadhia hiyo inatokea sana hasa kwa ndege ndogo. Kwenye ndege za masafa marefu zimekuwa pressurised kuondoa tatizo hilo
 
Kwenye seat ya mbele yako, back pocket inakuwa na karatasi ya maelekezo. Njia nzuri ya kuondoa ears popping ni kufunga mdomo na kuujaza hewa as much as u can (kama unapuliza puto). Utasikia jaws zinaachia. Endelea hadi utakapoona kitu kimeachia kwenye masikio. Ukizoea kusafiri na ndege itaacha hii hali,lol!
 
Kunakokuwa na pressurized air ndani ya chumba, masikio na mdomo maeneo ya koromeo kwa juu huwa kuna mawasiliano.
Mawasiliano haya yanawezeshwa kwa kufunguka kwa njia iliyo kama aina ya tube inayoitwa Eustachian tube, inapofunguka uweza kuequalize a pressurized air entering through ear with mouth.
Sasa kama hii njia haiwezi kufunguka, a pressurized air entering in the ear exert a pressure in ear and cause a painfull experience. In a flight there is a pressurized air.

Advace: Go to see an Ear, Nose and Throat (ENT-surgions.) watakusaidia tatizo lako.
 
Kwenye seat ya mbele yako, back pocket inakuwa na karatasi ya maelekezo. Njia nzuri ya kuondoa ears popping ni kufunga mdomo na kuujaza hewa as much as u can (kama unapuliza puto). Utasikia jaws zinaachia. Endelea hadi utakapoona kitu kimeachia kwenye masikio. Ukizoea kusafiri na ndege itaacha hii hali,lol!

ameshasema mara nyingi anapanda ndege, bado kuna kuzoea tu? King'asti.
 
Last edited by a moderator:
kussy, unajuaje kama abiria wengine huwa wanakuwa normal? usiusemee moyo.
 
Last edited by a moderator:
Mwezi May nilikuwa Dar na jamaa zangu ambao ni wafanyakazi wa kwenye ndege.

Niliwaambia kuwa dalili ya kuwa tumekaribia Dar ni watoto kulia kwa sababu ya maumivu masikioni.

Na kweli tulitua Zurich, kimya. Tukatua Nairobi hamna makelele. Tumeipita tu Zanzibar nikaanza kusikia makelele ndani ya watoto na nikwaambia, mnasikia hiyo habari?

Hili tatizo pia linakuzwa na Dar kuwa usawa wa bahari na joto la Dar. Ndiyo maana Nairobi ni dogo.

Njia zilizoandikwa ni kweli kabisa zinatumika. Ila hawa jamaa zangu wafanyakazi wa kwenye ndege waliniambia kuwa niwe nakunywa maji muda wote wakati masikio yakianza kuuma. Hivyo nikikaribia Dar, nachukua kichupa kabisa cha maji na kunywa kila baada ya sekunde kadhaa nameza funda moja.

Kuziba masikio haisaidii sana kwani nafikiri ni mishipa ya kichwani inabanwa na Pressure na si kuwa pressure inapitia masikioni. Nilishaambiwa kuwa ukitumia vikomve ukaziba masikio inasaidia. Nikakusanya vikombe vyangu na nikatumia. Baadaya ya dakika moja nikaviondoa maana nilikuwa kama nazidisha tu maumivu kwa kukandamiza masikio.
 
Nadhani wewe unapanda vile vindege vya TANAPA vya watu wa nne, nina imani kama unapanda ndege kubwa kubwa tatitizo hili halipo ama lipo kwa kiasi kidogo sana

Siyo kweli hata kwenye ndege kubwa hili tatizo lipo. Pipi na kufanya kama unapiga miayo husaidia sana
 
Wadau naomba msaada mara nyingi nasafiri na ndege na mara zote masikio huuma sana, inasababishwa na nini na njia gani naweza kuzuia hali hii, mara zote hizo abiria wengine huwa wako normal.
kussy, ni tatizo la kawaida hata kwa regular travellers depending on Pressure Changes ndani ya ndege.

Achana na kupiga miayo, kutafuna big G au kuzibua masikio nk . . . do the following kila hali hiyo inapotokea . . .

Funga poa zako kwa Mkono (ina maana Minya Nostrils), jifanye kama unapenga makamasi lakini bila kufungua pua. Utaona tu Pressure inabalance. Unaweza kujaribu hata sasa si lazima uwe kwenye ndege.

Good luck!
 
Back
Top Bottom