Kuuliza si ujinga

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Nimesikia maneno haya lakini bado sijajua ni vyombo au taasisi gani na vinafanya nini
MKUKUTA na MKURABITA
Naomba mwenye kufahamu zaidi wanijuze nijue masahi na faida zake kwa raia wa kawaida
 
mkukuta ni mpango wa kukuza na kuongeza umaskini tanzania na mkurubita ni mpango wa kupunguza rasilimali ufahamu bila idhini tanzania
 
Kuna nyingine sasa hivi imeongezeka inaitwa "MKUMABI", yaani MKAKATI WA KUONGEZA MASLAHI BINAFSI, ingawa hii haitangazwi sana
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Mi pia nimesikia maana ya mkurabita ila ni mbaya. Ngoja nisikilize wadau kwanza.
 
Nimesikia maneno haya lakini bado sijajua ni vyombo au taasisi gani na vinafanya nini
MKUKUTA na MKURABITA
Naomba mwenye kufahamu zaidi wanijuze nijue masahi na faida zake kwa raia wa kawaida

wakati mwingine kuuliza huwa ujinga. Hebu cheki alivyokujibu kitalolo, kakuona wewe mjinga sana. Hiyo siyo maana ya maneno hayo. Cheki kwenye google kama alivyokuambia mj
 
unajua ukijua unajua wakati hujui inakuwa hatari..
bora ya mjinga atakaye kujifunza kuliko mjanja asiyetaka kujua
ukirudia kusoma utaelewa kitalolo katoa jibu sahihi sana kama hujatambua
 
Nimesikia maneno haya lakini bado sijajua ni vyombo au taasisi gani na vinafanya nini
MKUKUTA na MKURABITA
Naomba mwenye kufahamu zaidi wanijuze nijue masahi na faida zake kwa raia wa kawaida
Kweli bana....
 
unajua ukijua unajua wakati hujui inakuwa hatari..
bora ya mjinga atakaye kujifunza kuliko mjanja asiyetaka kujua
ukirudia kusoma utaelewa kitalolo katoa jibu sahihi sana kama hujatambua

ok. Mi nilidhani uko serious
 
Pole sana inaonekana hata redio husilizi,kama wewe hujui maana ya mkukuta,hao wa vijijini itakuwaje? basi subiri mpaka utakapo kukuta ndipo utakapojuta.
 
mkukuta ni mpango wa kukuza na kuongeza umaskini tanzania na mkurubita ni mpango wa kupunguza rasilimali ufahamu bila idhini tanzania

Kitalolo kama hujui maana usimpotoshe mwenzako.

MKUKUTA - Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (National Strategy for Growth and Reduction of Poverty in Tanzania)

Ama MKURABITA naisikia lakini siifahamu, najua inahusiana na kuratibisha Biashara ndogo ndogo Tanzania.
 
kwa nyongeza MKURABITA ni mkakati wa kurasilimisha biashara za wanyonge Tanzania.hadi leo mradii huu haueleweki kama umefikia malengo au wanajinufaidisha hela za ufadhili kutoka NOrway na serikali.Upo chini ya ofisi ya rais.wao wanapima pima viwanja na kutafuta hati za kimila kwa watu mikoani humo kama Kigoma,Mtwara,mbeya.Lushoto nk lakini sijaona walipoweza kumsaidia mnyonge kama wanavodai.Machinga hadi leo wanahangaika, mabenki hayakubali hati za kimila mtu kukopea ili mtu aweze kujiendeleza nk. lengo lao kubadili sheria za biashara,TRA,nk eti iwe moja ili mtu aweze kuanza biashara na kusajili makampuni fasta kitu ambacho hakiwezekani, tafiti zao nyingi wanazofanya hazijazaa matunda na hazina uthibitisho.Mfano wao walisema sababu ya kesi kuchelewa mahakamani ni kwa sababu ya uhaba wa majaji bila kujua hata majaji waliopo wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii kama sheria zilizopo zikibadilika kuendana na mazingira na wakati huu.Pili hata mtu akipewa hati ya kimila au hata hati ya kawaida ya umiliki wa ardhi hataweza kupata mkopo kama ardhi yake ipo mbali na mji thamani yake huwa ni ndogo nk.Yapo mengi tu walipendekeza lakni sio rahisi kutekelezwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004 wkt wa MH MKapa..Sasa angalia mishahara wanayyolipana na kazi inayonfanywa utashangaa sana huko MKurabita na MKUKUTA,tuongeze na TASAF vikao vingi vya kupeana siting alowance,trip za kumwaga kila wakati nk nk.Mnyonge atabaki kuwa mnyonge tu siku zote.
 
Kitalolo kama hujui maana usimpotoshe mwenzako.

MKUKUTA - Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (National Strategy for Growth and Reduction of Poverty in Tanzania)

Ama MKURABITA naisikia lakini siifahamu, najua inahusiana na kuratibisha Biashara ndogo ndogo Tanzania.

KITALOLO yuko sawa, wew umedanganya bana! Hamna kitu ya kuleta utajiri hapa Bongo. Hii Ni MKUKUTA inayoongeza umaskini tanzania,hasa vijijini... Nashukuru elimu imenitoa huko hadi hapa mujini!
 
Pole sana inaonekana hata redio husilizi,kama wewe hujui maana ya mkukuta,hao wa vijijini itakuwaje? basi subiri mpaka utakapo kukuta ndipo utakapojuta.

kirefu chake nakijua ila kazi yake ndio inanitatiza...
ndo maana nikamsapoti kitalolo
something is wrong kwenye reality
 
Back
Top Bottom