Kuuchukia Ufisadi na Kuwapenda Mafisadi

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Hii tabia ya kuhudhuria hafla zilizoandaliwa na mafisadi. Huu utamaduni wa kuwasiliana na mafisadi. Hizo hulka za kuchekacheka na mafisadi. Huo utaratibu wa kupiga picha na mafisadi. Hayo mahusiano ya kuishi kwa amani na upendo na mafisadi. Haya yote ndiyo yanayolea ufisadi nchini!

Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
- Mfalme Daudi
 
Nimependa sana quotation yako Mkuu!

Ni ngumu sana Ndugu yangu Companero kuwaepuka kwa 100% hawa manyang`au!...Utawakimbia kumoja, kwingine utakuta unanunua bidhaa zao, ambapo ni kuwapromoti!

Wewe mwenyewe ulipata kusema kwamba umechoka na inji hii na hivyo unaenda ukabebe maboxi, lakini hata sasa bado upo nchini, unaendelea kupita katika barabara zilizojengwa na CASPIAN CONSTRUCTION COMPANY LTD...!

Mambo haya magumu bana....Tuombe MUNGU.
 
KAMA HATUWEZI KUWAFUNGA, WALA KUWAKAMATA, WALA KUFILISI MALI WALIZOTUIBIA, japo tuwazomee basi, inatia kinyaa sana kuwahekea chekea...
asante for the useful post.
 
mmh.....hapa umewachoma sana wale wapambe na makuwadi wa mafisadi
 
scan0032.jpg
 
Kama kuwazomea nako hatuwezi basi tuonyeshe kukerwa kwa kutojihusisha nao...kwani madhara yao ndio yanayoua ndugu zetu kwa kukosa dawa mahospitalini, huduma za maji safi na elimu bora.
 
Kama kuwazomea nako hatuwezi basi tuonyeshe kukerwa kwa kutojihusisha nao...kwani madhara yao ndio yanayoua ndugu zetu kwa kukosa dawa mahospitalini, huduma za maji safi na elimu bora.
ni kweli, kusema kua RA,Lowasa ni mafisadi hakutoshi, ni lazima tujitenge nao, kusema kua watendaji wa Serikali hasa Mawaziri ni Wachafu ila aliewateua ni msafi ni kucheka cheka nao kwa mtindo mwingine,
kweli inawezekanaje alie wateua kina Sofia, karamagi , msabaha kuwa mawaziri akabaki msafi, mbona hataki kuwapeleka selo.
ndo maana nawapenda wananchi wanaozomea zomea viongozi wa ngazi ya juukatika sekta ya UMMA, wanawachukia kivitendo sema tu hawana uwezo wakukabilizna nao na kuwapora mali zetu walizo chuma, ole wako Chenge, RA, Lowasa , Karamagi, Sophia Simba, na mafisadi wa kariba hiyo. ipo siku wananchi watapata moto zaidi watawatoa kwenye viringe vyenu, watakula nyama zenu....Nawachukia sana.
 
wanatuzadharau kwa maana tunachekacheka nao. ila ipo siku tutanyonya damu yao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom