Kutumia watoto wadogo kwenye maigizo ya kutisha:haki za watoto zikowapi?

kulwa12

Senior Member
Jun 30, 2009
103
28
Wadau nakuja na kiti kinachonisikitisha sana,kuna tabia sasa inakua kwa kasi ya baadhi ya wasanii wa maigizo na filimu hapa tanzania kushirikisha watoto wadogo katika matukio ya maigizo/picha,cha kusikitisha zaidi watoto hawa ni wa kati ya miaka 2-5

nitatoa mifano kadhaa nimeangalia kanda mmoja katika tukio moja watu wazima wawili wana rushiana mtoto wa miaka sio zaidi ya mitano kama mpira.

Na wengine mama anapigwa na mmewe huku kabeba mtoto mchanag mgongoni na kibaya zaidi mtoto yule haelewi kinachoendelea akalia kwa mshituko mkubwa sana.je haki za watoto zikowapi? Na matukio haya ya kutisha hayawezi kuwaasili watoto hawa kiakili?
 
Hiyo ya kumrusha sijaifurahia ila kumpiga mama kwa kuigiza sioni kama kuna ubaya maana haumii. Na mtoto pengine walimchokoza tu ili kuongeza uhalisia.
 
Huwezi kumshirikisha mtoto bila wazazi kusign ruhusa. Hivyo mzazi mwenyewe anatakiwa akubaliane na scene ambazo mtoto atakuwa anaplay au anakuwa exposed!
 
Huwezi kumshirikisha mtoto bila wazazi kusign ruhusa. Hivyo mzazi mwenyewe anatakiwa akubaliane na scene ambazo mtoto atakuwa anaplay au anakuwa exposed!

Bongo kuna kusign kweli?
Au wanaambiana tu "mama 'nanii' nataka nimweke 'nanii' kwenye movie yangu ijayo" mama 'nanii' nae anachekelea tu mwanae kuwa kwenye movie.
 
Bongo kuna kusign kweli?
Au wanaambiana tu "mama 'nanii' nataka nimweke 'nanii' kwenye movie yangu ijayo" mama 'nanii' nae anachekelea tu mwanae kuwa kwenye movie.

Hilo nalo neno! Come to think of it, hata waandishi wa habari sidhani kama wanapata ruhusa kwa wazazi/walezi pale wanapowainterview watoto!
 
Mimi naona haina shida ila wawe makini. Tena watoto wakiendelezwa vizuri katika sanaa baadaye watakuwa waigizaji wazuri. Mfano Lulu anayetembea nusu uchi alianza sanaa tokea mdogo na anaigiza vizuri ila alikosa uangalizi wa kimaadili.
 
Back
Top Bottom