Kutumia marehemu kisiasa ni zaidi ya kufilisika kisiasa

Hivi Nape bado yuko na katuni huku??? hajui kama yeye na wenzake wanamagamba ndio wamefilisika hadi kufikia kuiba maiti mochuari
 
Jeshi kutumiwa na chama tawala kuua watu wake ambao ndio wanawalipa mishahara ni sawa na kubaka siasa.na polisi kuua raia na kuwaambia wafiwa serikali itagharimia mazishi ni sana na kuhaini wananchi.
Jeshi kutumiwa kulinda majambazi wa madini yetu imekaa sawa.
Polisi kuiba miili ya marehemu usiku ni sawa?
 
Join Date : 14th September 2008
Posts : 65
Thanks 0
Thanked 38 Times in 22 Posts

Rep Power : 23

Yaani huyu dogo tangu ajiunge JF miaka mitatu hajaona posti hata moja ya kutolea 'THANKS'???!!!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Kutumia marehemu kisiasa ni sawa na kufirisika. Hapa nilivutika kusoma ajenda hii nipate ukweli ni je Polisi waliiba mwili wa marehemu au kuuchukua kwa namna ambayo si ya kawaida na je hawakuta ndugu wauzike na yote kwa sababu gani. Lakini analaumu na yeye anatoa maelezo ya kisiasa hivyo hivyo. Hapa wasomaji nje ya Tarime wanabaki hawajui nani anapotosha.

Tatizo baadhi ya watanzania ni watu wenye kutumia akili yao vibaya sawa na watu wenye akili finyu ni kwamba hawaangalii na kuzungumzia mada objectively kwa hoja. Ushauri wangu kwao, ukitoa wazo lolote hadharani basi jiweke nafasi ya mwanafunzi anayeeleza jambo kwa joho la walimu wake ambao hapa ni ulimwengu wa Tanzania na dunia. Halafu utazungumza points.

Mtu hazuiwi kuwa na mawazo yake kwa ajili yake mwenyewe na ya aina hiyo akae nayo mwenyewe. Tunapotoa mawazo yetu hadharani tuachane na mawazo binafsi au porojo za kudhani ndiyo siasa katika mambo serious. Hizi siyo enzi za kupakia katika kichwa cha mtu kile unataka wewe ukifikiri yeye hafikiri au hana elimu hiyo. Hiyo ni zamani, sasa watu wengi wamesoma na wanajua. Acheni hizo!
 
Nimeona kikatuni mahali mtu mmoja kavaa kombati akiwaambia wafiwa subirini msizike msubiri maandamano yetu hapa.......hii ni dhihaka au kweli?

Kikatui kilikuwa na magwanda ya CCJ au!!? tuhabarishe mkuu tukitafute:A S 103:
 
Naona mtoa hoja ni Nauye Jr na picha ni ya Nape Nauye, je huyu ni Nape Nauye kabisa au mtu mwingine. Kama ndiye asilete habari za magazeti ya uhuru hapa. Yeye atwambie mkakati wa siku 90 kwa watuhumiwa ............., aeleze kwa nini alisema hawezi kujiunga CDM kwa kuwa ni cha wachaga
 
Ni kweli kabisa ,si vizuri kumtumia marehemu kisiasa. However, by reading your post I don't know what are you exactly trying to insuniate. As a serious politician you should look at it critically and analytically
Mkuu huo ndo uwezo wa katibu mwenezi wa MAGAMBA ulipoishia, Ndo mawazo yake bora angekuwa ni Marelia Sugu!
 
Hembu tulia wewe siasa msibani sisi ndio tunaujua uchungu kwani ndio wafiwa kama kwenu ni siasa mbona mliwauwa nyie na ccm na mlikimbilia kutaka kuzika mapema ili kupoteza ushahidi subirini ngoma inogile.
 
Nimeona kikatuni mahali mtu mmoja kavaa kombati akiwaambia wafiwa subirini msizike msubiri maandamano yetu hapa.......hii ni dhihaka au kweli?

Nimekuwa na wasiwasi sana na uwezo wako kiuongozi. Namna unavyokabiliana na majukumu yako mapya ni tofauti sana na jinsi ulivyokuwa umetuaminisha vision yako huko nyuma.

Ulitufanya tukuamini kuwa unajua udhaifu cha chama chako na unataka kupambana na udhaifu huo. Sasa hivi inaonekana kuwa kazi yako imekuwa ni kupambana na CHADEMA badala ya kupambana na udhaifu ulipo ndani ya chama chako cha CCM ili CHADEMA ikose udhaifu wa kukosoa ndani ya chama chako.
 
Hakukuwa na mtu Serikalini ambaye angeweza kumuwakilisha Kikwete katika kutoa rambi rambi kwa familia ya Sheikh Yahya ili aweze kushughulikia matatizo mbali mbali ndani ya nchi yetu ambayo yanapigiwa kelele na Watanzania katika kila kona ya nchi yetu!? Au naye anatumia marehemu kisiasa zaidi? Mbona wale Watanzania waliouawa kule Arusha na hivi karibuni kule Tarime hatujamuona Kikwete kwenda kutoa rambi rambi kwa familia za wafiwa!?


Heshima kwako BAK

Umesahau lazima arejeshe fadhila za ulinzi usionekana.
 
Nape... Hivi hatari zaidi ni kuua (yaani kuchukua uhai mtu mwingine bila matakwa yake) au kumtumia marehemu kuwasaidia ndugu wa marehemu kupata haki??
 
Kwa hali ya kawaida wacha hicho kikatuni,nenda katika picha kamili huko Tarime, ni kuwa CHADEMA wameipiga bao CCM na moto wake ni mbaya kwa hawa wajamaa ukiangalia historia ni watu wa shari tangu enzi hizo katika majeshi ndiyo wenyewe wakubwa n.k.2015 kuna uwezekano wa kukosa mbunge wa CCM kanda ya ziwa wasipojipanga sasa.
 
Nape... Hivi hatari zaidi ni kuua (yaani kuchukua uhai mtu mwingine bila matakwa yake) au kumtumia marehemu kuwasaidia ndugu wa marehemu kupata haki??

Mkuu hapo umeharibu kabisa huyu Dogo atakimbia moja kwa moja.
 
Nimeona kikatuni mahali mtu mmoja kavaa kombati akiwaambia wafiwa subirini msizike msubiri maandamano yetu hapa.......hii ni dhihaka au kweli?

Mara tu ulipoteuliwa kushika wadhaifa ulionao ndani ya chama cha Magamba ulianza na gia kali na kuwataja mafisadi kwa majina, mbona hatukusikii tena umebakia kudakia vijikatuni? Mafisadi wamekushinda nini?
 
Back
Top Bottom