Kutumia gas Kwenye gari

Nyikanavome

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
482
176
Habarini za leo wana JF

Nina kagari kangu nataka nikageuze kaweze kutumia gesi na petrol ila ningependa nipate uzoefu kama kuna mtu ana gari yake inatumia gesi anipe uzoefu wake hasa wa gharama za uendeshaji. Pale sabasaba mwaka huu kuna jamaa waliokuwa wanatangaza hiyo product wanasema inaweza kupunguza gharama za uendeshaji hadi kwa asilimia 50%, ila bei yao ya ufungaji kwa gari ndogo ni kama 1,600,000/=

Naombeni uzoefu jamani
 
nenda dar es salaam instute of education (DIT) pale kuna wataalamu wanafanya shughuli hiyo ya kuwezesha magari ya petroli kutumia gas watakuelewesha vizuri na kwa kitaalamu zaidi
 
Ahsanteni
Hakuna kabisa mtu mwenye kagari kanakotumia gesi Kweli!

Go green go> pengine vyama viingize hii kwenye kampeni zao, watalalam waliniambia vifaa viko bei juu kutokana na kodi kubwa ndio sababu bei ya ubadilishaji ni kubwa
 
naona magari mengi yanayoagizwa kutoka UK yana hizo pipe za gas sasa wenye kujua huduma hiyo inapatikana wapi watujulishe ili tuweze kujua kama hiyo teknolojia imeshatufikia hapa nchini
 
Habarini za leo wana JF

Nina kagari kangu nataka nikageuze kaweze kutumia gesi na petrol ila ningependa nipate uzoefu kama kuna mtu ana gari yake inatumia gesi anipe uzoefu wake hasa wa gharama za uendeshaji. Pale sabasaba mwaka huu kuna jamaa waliokuwa wanatangaza hiyo product wanasema inaweza kupunguza gharama za uendeshaji hadi kwa asilimia 50%, ila bei yao ya ufungaji kwa gari ndogo ni kama 1,600,000/=

Naombeni uzoefu jamani

Mkuu inategemea na ukubwa wa gari lako maana ule mtungi huchukua sehemu kubwa ya buti na pia ni vyema ukapima faida na hasara zake. Mimi binafsi kama matumizi yako ya mafuta ni chini ya lita 20 kwa kila kilometa 100 sioni haja ya kuwa na LPG. Pia zingatia ya kwamba huu mfumo ni after market na sio oem factory install hivyo ufungaji wake na maintenance ni lazima iwe ya hli ya juu.

Kuna mijadala mingi tu kuhusiana na faida na hasara za LPG na hizi zipi kwenye mtandao na kwa wale purists tuna mashaka ya jinsi gani nishati hii maradufu inavyoongeza msukumo wa ziada katika engine kutokana na near perfect combustion katika ignition system.

Kwa kawaida watu hufunga LPG katika magari ya engine za Petroli zenye displacement ya angalau 4000cc
 
Ahsanteni Kwa michango ya mawazo

Ahsante PatPending kwa kunipa mtazamo wa jicho la pili kuhusu kulibadili gari kutumia gesi. Nitaambatanisha kipeperushu ambacho nilkipata sabasaba kuhusu ubadilishaji wa magari ili yaweze kutumia gesi.
Preta kama kuna mtu ana gari ina mfumo wa kutumia gesi, teknologia hiyo ipo hapa Tanzania na kuna kituo kiomoja pale Ubungo maziwa ambapo mtu unaweza kujaza gari yako gesi
 

Attachments

  • CNG Tanzania.pdf
    1.8 MB · Views: 235
Back
Top Bottom