Kutumia face book kama photo album

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,512
4,129
Wadau wa Jf book,
Jana nikiwa kwenye Lunch nilikuta mjadala ambao ulinivutia nikaona nishirikishe wadau wangu wa JF;

Watu wengi hasa walioko kwenye mahusiano walionesha kukerwa sana, na wapenzi wao kujaza picha kwenye FC, walikuwa wakilalama kuwa, mtu kujaza picha zake kwenye fc ni aina flani ya kujiachia au kutoweza kumiliki hisia zake.
Nilisikia mmoja akilalamikia ujio wa hizi simu za kichina ambao mtu anaweza kupiga picha wakatiwowote na ku upload imefanya hali iwe mbaya zaidi, aliongeza kuwa wengine wanajisahau na kuweka picha ambazo kimsingi hazipendezi ku display. Mbaya zaidi ni wengine kuweka picha kwa ajili ya kumkomoa mwenzake na kusahau kuwa hizo picha zinaonekana na public???
Wengine walichangia kuwa, hili limesababishwa na utandawazi, ila wanasahau kuwa ukifuatiia profile za wazungu walio jaza picha zao karibia wote wanasababu za msingi; Utakuta ni muingizaji hivyo anavutia fun wake, wengine ni wana mitindo hivyo wanahitaji sponsor, wanamuziki hujaza picha kwa kuvutia wapenzi wao nk
Hapa nyumbani mtu anaweka picha za namna kama hiyo ya hapo juu wakati yeye hahusika kabisa na hao, sisemi wasiweke ila ninacho jaribu kusema ni waaweke picha gani? Kwa makusudio gani? na Idadi gani? Tahadhari yangu ni kuwa isiwe copy paste kwa wazungu kwani sio kila cha wazungu ni kizuri!!!!
Utakuta mtu alifunga ndoa miaka kumi iliyopita bado picha amejaza kwenye fc?? Just for your information kama unaenda na wakati, Picha kama hizo unatakiwa uziweke wakati wa wedding anivessary baada ya hapo unazitoa!!!
Mimi binafsi nina hobby ya kupiga picha hivyo nina picha zaidi ya 1000 za kwangu na za matukio mbalimbali niliohudhuria ila nimeziacha kwenye pc yangu….huwa nawaonesha wanaohusika kama ni za matukio ila zile ambazo hazina effect kwa public kama safari za kwenye wildlife parks huwa nawaonesha marafiki ambao wengi huzipenda na kuomba copy.
Wadau wengine mnaonaje kufanya face book kuwa photo album?
 
watanzania walio wengi hawana uelewa wa ICT....hata FB kuna customization kibao za privacy sema ushamba wetu ndio kikwazo
 
Facebook ni pana sana, na mapokeo yake kwetu ni tofauti, lakini cha msingi kila mtu ana uhuru wa kufanya atakacho kwenye akaunti yake kama anaona kinamfurahisha.
 
Naunga mkono hoja, si busara kudisplay picha kwenye public wakati hazifahi kuonyeshwa huko.
 
Mimi binafsi sikubaliani kuwa ni uhuru wa mtu kufanya apendavyo kwani...ndio sababu ku kawa na nafasi ya kukumbushana na kuelimishana...
 
2napo2pia picha fb weng 2nategemea gud coments kama, a girl aambiwe ur cute,attractv mzuri gud luking na vingenevyo ukifatilia picha yenyew kila k2 kaonyesh nje tunajidhalilisha sana mostly wadada cjawah ona mkaka kapiga na chupi mjirekebishe mnao2pia picha fb za kujianika
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom