Kutoroka familia: Ni busara, kulogwa au tatizo la kisaikolojia??

Hata mimi nina kaka yangu yalimkuta hayo hayo sasa ni mwaka wa 8 hatujui aliko yaani hataki kabisa kujulikana amesusa mpaka familia nzima kisa mkewe, jamani wamama tuwe na kiasi

Ple sana Maty, unajua mimi hadi nilitamani kulia. Niliwahi kukaa naye takribani masaa 6 tunaongea, nikimshauri asiondoke lakini wapi. Je, familia yenu imefanya juhudi zipi za kumtafuta nduguyo???
 
Hatujui ugomvi ulikuwa ni nini kiundani.

So ngumu sana kushauri

Dena, matatizo ya huyo jamaa ni ugomvi kati yake na mkewe. Eti mke si mwaminifu na mume si mwaminifu katika ndoa yao. Kelele kila siku, kila mara wakutanapo. Ni kweli mwanaume aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti fulani mkewe kajua, lakini alimwacha nami najua hivyo, lakini mkewe ni ugomvi tu kila mara. Hatahivyo, ugomvi haukuanzia hapo, ulikuwepo hata kabla ya hapo. Hilo ndilo tatizo lao kubwa.
 
mie sijui kama ni busara au la kutoroka familia...ila nampongeza kwa kumuacha huyo mwanamke aliyekuwa anamuabuse psychologically and physically .....jambo ambalo angepaswa kuweka kny consideration ni watoto wake, future yao na yake mwenyewe.......nahisi amekuwa abused sana mpk amesuufer low self esteem kiasi na anafeel worthless yeye kama baba ndio maana kakimbia..........mie ningekushauri mumtafute anaweza kujiua,mumpe ushauri aachane na mkewe ila wapange future na jinsi ya kulea watoto wao..........msisitizo mumuonyesha kuwa watoto wake bado wanamuhitaji,na mmpoint yale mazuri aliyoyafanya anayoweza kufanya kwake na familia yake ili arebuild up his lost confidence.

roselyne1, asante kwa ushauri. Tatizo lililopo kwa huyu bwana aliniaga kuwa ataacha ameandika wosia. Kwamba hatohangaika kuwatafuta watoto kwani -."... nami sikulelewa na wazazi wangu, nao wanangu Mungu atawalinda na kuwatunza..." Aliniambia kwa masikitiko. Kwa hiyo, nilijaribu kumshauri lakini akasema, kwa sasa hajaona haja ya kurudi tena make hataki hata kuona sura ya mke wake huyo!!!
 
Hata mimi nina kaka yangu yalimkuta hayo hayo sasa ni mwaka wa 8 hatujui aliko yaani hataki kabisa kujulikana amesusa mpaka familia nzima kisa mkewe, jamani wamama tuwe na kiasi

...huu ni thibitisho matendo haya yanahitaji ufumbuzi kwenye jamii yetu. Inasikitisha.

Mkuu, asante kwa ushauri. Nakubaliana na wewe kabisa. Huyu mama bila shaka naye anataka kurithi mali za mwanaume. Aliwahi kuniambia kuwa".... hadi nifike hapa, nilimtoa mwanaume kwao, amenijengea hapa karibu na kwetu, siwezi kutoka hapa, labda yeye aondoke." Kabila lake ni Mhaya. Sijui ni target group yako???

...ama kweli "there is a thin line between love and hate!"

Ungemwambia jamaa yako watoto hawana makosa. kama yeye hakubahatika kulelewa na baba na mama, isiwe sababu ya kuwakomoa watoto. "What goes around comes around."
 
Inasikitisha bw Edson,...labda nikuulize? wewe binafsi umemtafuta? na
umetumia njia gani kumtafuta? Familia yake wanaendeleaje bila yeye?

mkuu mpaka leo hatuji aliko familia yote...... tulishatafuta hadi tumechoka....
familia yake ipo ..watoto wapo katika famila yetu tumewasomesha na wanaendelea vizuri.....mama wa watoto wale alikaa kwa mwaka mmoja lakini alifariki baadae 2008 june kwa malaria.......watoto wawili wapo hai na tumewainclude katika familia yetu...mali zao zipo na wakikua watapewa kwa sasa famia yangu ndo inasimania.....na hizo ndizo zinasomesha watot wale
 
Duh hii issue ni serious sana bana. sikiza andika tangazo hata facebook huko uwaulize marafiki mbalimbali usikute alienda kujificha mahala akafariki huko.sasa mke keshafariki anahitaji arudi home kutunza familia yake.
 
Back
Top Bottom