Kutolewa Nje ya Bunge Mh. Mnyika - Haki iko wapi?

Katika hali ya kawaida ya siasa katika bunge letu,baada ya kauli ile nilijua tu kwamba ana hatari ya kutolewa nje.Bunge ambalo spika na naibu wake woote wamewekwa kwa malengo flan flan.Lakini naamini wamemtoa nje mnyika ila fikra zake pevu zimebaki ndani na zitaendelea kusumbua humo.Gharama za haki ni kubwa mno ambazo watanzani wengi hawajawa tayari kuzibeba ingawaje uwezo wanao.Wanawatoa wabunge wa upinzani bungeni huku na wao wakisubiri kutolewa na wananchi majimboni. Leo acha washangilie kutolewa mnyika,kesho mimi nitashangilia watakapozomewa na kunyimwa majimbo.
 
NIMEAMINI KUWA UONGOZI UNAFAA KUWEKEWA KIWANGO CHA CHINI CHA UMRI!!!!!!!!!!!!!!!!!


Katiba yetu inamruhusu mtanzania kugombea ubunge akiwa na miaka 22 na kuendelea. ni jambo zuri kuwa na wabunge vijana lkn hali halisi ya kimaumbile inapingana na kanuni hii. wabunge wengi wa kiume bungeni waliyo vijana hawajaoa. zitto, mnyika, makamba, mkosamali, kafulila....... nk................


kuoa ni jambo la heshima. humkuza mtu kiakili na humfanya ajiheshimu ktk jamii na aheshimike na jamii. kuna vijana wamezua mtindo wa kuzungumza nungeni ipasavyo. madhali kila mbunge alisaini kutii kanuni za bunge, hapana budi anaevunja kanuni awajibishwe. mnyika amemetukana mh rais bungeni. ameombwa afute kauli yake amekataa. naibu spika amemtoa bungeni kwa kikao cha leo tu. wadau inaelekea umri mzuri wa ubunge ni miaka 30 na kuendelea.....
 
Peleka maoni yako kwenye tume ya katiba kwamba SIFA za MBUNGE ni
1. KUOA/KUOLEWA
2. Miaka 30 na kuendelea
3. Kuwa mnafiki (kama RAIS ni dhaifu lazima unafiki)

Sasa Mbona huyo SPIKA unayempigia chapuo atakosa SIFA maana HAJAOLEWA!
 
Back
Top Bottom