Kutolewa kafara kwa Mwandishi Daud Mwangosi, mpango ulikuwa Chadema ifutwe!

Kwa hiyo unataka hata Polisi wangeandikwa wana CCM badala ya Polisi sio?

Polisi waandikwe chochote haijalishi lakini anapouliwa "mpiganaji" wa chadema kwanini iwe mwandishi na si "mpiganaji" wa chadema? Mwandishi alikuwa pekee pale? mbona wengine hawajauliwa?
 
Maswali gani haya mkuu wangu? Hivi walipouawa watu 34 South Afrika unaweza kusema kwa nini wale wengine hawakuuawa?. Mo lazima kwao wafe watu wengi ndio ujue haikuwa dhulma ya roho ya mtu..
Again Mpiganaji ni neno linalotumiwa na wanaChadema kwa mwanaharakati yeyote yule. Kumbuka sii watu wote ni wanachama wa Chadema isipokuwa wanaungana nacho ktk kutafuta mageuzi nchini baada ya kuchoshwa na uongozi wa CCM. Hata wewe leo hii unaweza kuitwa Mpiganaji ikiwa utaanza kupigania haki za wananchi badala ya Udalali wa chama tawala, nina hakika mwaka baada ya uchaguzi 2015, akiondoka JK utarudi kuwa mpiganaji..
 
Maswali gani haya mkkuuu wangu? walipouawa watu 34 South Afrika unaweza kusema kwa nini wale wengine hawakuuawa?..Again Mpiganaji ni neno linalotumiwa na wanaChadema kwa mwanaharakati yeyote yule. Kumbuka sii watu wote ni wanachama wa Chadema isipokuwa wanaungana nacho ktk kutafuta mageuzi. Hata wewe leo hii unaweza kuitwa Mpiganaji ikiwa utaanza kupigania haki za wananchi badala ya Udalali wa chama tawala..

Chadema wanapigania haki ya nani? ya wakubwa kujikopesha kujenga majumba ya kifahari? changa la macho.

Ally muuza magazeti au alikuwa si mwandishi?

Kwanini isiwe "mpiganaji" na iwe mwandishi? publicity? hao 34 unaowataja waliouwa kuna hata mmoja anatajwa shughuli zake? au wanatajwa kuwa ni waandamanaji?

Mantiki ya chadema kutumia fursa na kumchombeza huyo mwandishi naona unaikwepa. Ukweli ni kwamba Slaa alijuwa kitakachootokea, kuna watu wamewekwa wafanye ukaidi. Ushahidi ni ujumbe wa Slaa kwa Mwema, pengine haa huyo polisi aliyemfyatuwa mwenzake yuko kwenye payroll na kaahidiwa utatoka na maisha yako yatakuwa mazuri. Ikiwa wameweza kumchombeza Daudi watashindwa kumchombeza huyo Polisi?

Chadema si chama cha kutafuta maslahi ya Watanzania. Wale ni opportunists na miifano tunaiona sasa hivi, kujikopesha fedha za chama, kuzuga hawapati misaada ya CDU, kuuzia chama fuso chakavu kwa bei inayozidi hata mpya, kujipangia safari za kwenda kujifunza kufagia mji. Ni balaa tupu.
 
Hao 34 waliouawa walikuwa wafanyakazi ktk migodi ya kuchimba madini na walihusika moja kwa moja na maandamano, lakini dunia nzima imelaani kitendo kile na HUKUMU ilotolewa dhidi ya viongozi wao. Tunacholaani ni kitendo cha kumuua mwandishi wa habari ambaye hakuna na silaha isipokuwa kamera yake na zaidi ya hapo alikuwa kazini haijalishi alikuwa Mkerewe, muislaam au Chadema. Tunachosema ni nkwamba Polisi walitumia nguvu ya ziada na kinyume cha UTU.

Kila mahala nakusoma ukisema yale yalikuwa maandamano.. maandamano gani?.. Kilichokuwepo pale kilikuwa MKUTANO wa Wanachama kufungua tawi jipya na haikutangazwa Curfew iringa nzima au nchini isipokuwa Chadema pekee ndio walikatazwa kutofanya ufunguzi wao. Watu walienda makazini na kulikuwa na vijiwe bingine sehemu tofauti.. Sasa kama bado huelewi itakuwa kazi kubwa sana kwangu kuendelea na mjadala huu..
 
umenena lililotakiwa kunenaw...MUNGU AKIAMUA KUIKOMBOA ISRAEL KUTOKA UTWANI, HAKUNA ATAKAE ZUIA!
Nashukuru na kujionea fahar JF inapokuwa na watu kama hawa wanoweza ku clarify mambo...na sio kucfia kila kitu hata kama ni kinaua..
 
Kuuliwa alijitakia mwenyewe, unakwendaje kmvaa mkubwa wa polisi wakati umeambiwa sambaratika.

Nasema hivi kwanini aandike mwandishi na asiandike mwana chadema, au lina impact na sympathy zaidi na ndiyo maana akachombezwa akafanye alichofanya? maana Slaa alikuwa anajuwa watakaidi, ushahidi ni ujumbe aliomtumia Mwema. Kama alijuwa watakaidi asijuwe na hao wakaidi waliowachombeza huko?

Ukweli ubaki kuwa ukweli.

Kwa hili la chaddema kuamrisha watu wavunje amani ili nchii isitawalike, hata wafanye nini, Watanzania walio wengi wanaelewa kinachiendelea na wala huu upuuzi hautoijenga chadema kama chama cha walio wengi.

Huyo alikuwa huko kwa kazi za chadema na alikuwa mmoja ya wailochombezwa na Slaa kufanya fujo.

Zomba hata ni ushabiki umepitiliza If you know the truth,truth will set you free;Utaendelea kuwa mtumwa wa fikra zako mwenyewe mpaka lini???
 
Tarik Aziz! bora huyu alikuwa anafanya cha maana kuliko hawa jamaa zetu
sijui wanafanya nini?
 
Nilidhani tatizo la mtindio wa ubongo huisha mtu akipata elimu, kumbe ndio inakuwa sawa na kamasi tupu kwenye ubongo.
 
.......................mkuu, nimeupenda huu uzi. Katika hao vikaragosi uliowataja najua zomba na Ritz lazima watajibu tu......Na yule aliyekuwa anafanya propaganda wakati ule wa utawala wa Saddam alikuwa ni Waziri wa Habari anaitwa Al-Sahaf a.k.a comical Ally
 
Zomba hata ni ushabiki umepitiliza If you know the truth,truth will set you free;Utaendelea kuwa mtumwa wa fikra zako mwenyewe mpaka lini???

Mimi naona nyinyi ndio mnaopotosha ukweli. Jee, Slaa kama alikuwa hajui kuwa watafanya ukaidi angetuma ule ujumbe kwa Mwema?

Jee, Daudi alikuwa na sababu ipi ya kwenda kumvaa mkubwa wa Polisi, hivyo ndivyo wanavyofanya kazi waandishi? mimi nna uhakika wafanyao hivyo ni wapiganaji, sijaona mwandishi akamvaa mtu mwilini kuandika habari zake, tena hata husogei karibu ya Polisi walioweka mabango ya wazi kuwa sambaratika la sivyo watatumia nguvu. Kama si kujitakia kifo ni nini?

Kuwa mkweli wa nafsi yako kwanza na msituletee poroja za kitoto. Huyo alichombezwa na ukauvaa mkenge, watu kama huyo mimi huwaita misukule.
 
Tarik Aziz! bora huyu alikuwa anafanya cha maana kuliko hawa jamaa zetu
sijui wanafanya nini?

yule talik Aziz namfananisha na Zomba,yule bwana nae alikuwa king'ang'anizi sana,lakini sasa kimya hata simkii tena
yaani alivyo kuwa akisema utadhani leo vita inaisha,kumbe propaganda bwana
 
Mimi naona nyinyi ndio mnaopotosha ukweli. Jee, Slaa kama alikuwa hajui kuwa watafanya ukaidi angetuma ule ujumbe kwa Mwema?

Jee, Daudi alikuwa na sababu ipi ya kwenda kumvaa mkubwa wa Polisi, hivyo ndivyo wanavyofanya kazi waandishi? mimi nna uhakika wafanyao hivyo ni wapiganaji, sijaona mwandishi akamvaa mtu mwilini kuandika habari zake, tena hata husogei karibu ya Polisi walioweka mabango ya wazi kuwa sambaratika la sivyo watatumia nguvu. Kama si kujitakia kifo ni nini?

Kuwa mkweli wa nafsi yako kwanza na msituletee poroja za kitoto. Huyo alichombezwa na ukauvaa mkenge, watu kama huyo mimi huwaita misukule.
natamani sana kile kifo kinge mtokea mmoja wa mzazi wako,sijui kama leo hii ungekuwa ktk kichalazo cha komputa na kubeza kifo cha mzazi wa mtu mwingine.
 
Mkuu Mag3, yule wa Saddam alikuwa anaitwa Alsahafu. Huyu Advera laiti ingekuwa nchi za wenzetu angesharudi kijijini siku nyingi sana. Lakini kazi ya mungu ni kubwa, unajua alimuumbua ili kuonyesha ulimwengu namna uongo unavyotungwa maabara, kwa bahati mbaya maabara za Polisi wa nchi yetu zina wataalamu vihiyo.

Damu ya Mwangosi (R.I.P) itawafuata tu na nakuhakikishia ipo siku mpango mzima utakuwa wazi.
Tartibu washaanza kuumbuana, wale kruta waliofyatua mabomu wanahoji kwanini mwenzao afunguliwe mashtaka 'kwa kufuata maagizo'

Naomba kufahamishwa kwanini hakuna Inquest kwa tukio hili? Nini utartibu wake
 
Wajue kuwa Mungu ndiye anayeweka watawala katika nchi. Kama Mungu ameamua kuwa CC,M basi inatosha na sasa chama kingine kichukuwe madaraka, hakuna awezaye kuzuia. Je nani awezaye kuzuia mafuriko kwa mkono? Hakika yatamsomba. Enzi za mwalimu aliyekuwa akiona mbali, alikuwa na uwezo wa kuongoza mabadiliko badala ya kuyapinga. Lakini hawa mafisadi wamefungwa akili kiasi kwamba wanaangalia maslahi yao tu. Mabadiliko ni lazima.
 
natamani sana kile kifo kinge mtokea mmoja wa mzazi wako,sijui kama leo hii ungekuwa ktk kichalazo cha komputa na kubeza kifo cha mzazi wa mtu mwingine.

Bahati nzuri wazazi wangu wamefariki zamani sana. Hakuna ataebaki duniani milele.

Habezwi mtu hapa, hapa kila mtu ana muono wake na mtaamo wake wa matukio.

Jibu haya maswali:

Jee, Daudi alikuwa na sababu ipi ya kwenda kumvaa mkubwa wa Polisi? hivyo ndivyo wanavyofanya kazi waandishi? mimi nna uhakika wafanyao hivyo ni wapiganaji, sijaona mwandishi akamvaa mtu mwilini kuandika habari zake, tena hata husogei karibu ya Polisi walioweka mabango ya wazi kuwa sambaratika la sivyo watatumia nguvu. Kama si kujitakia kifo ni nini?
 
Zomba,'
Ngoja nikusaidie. Daudi alienda kumuuliza mkuu wa polisi ni kwa nini mwandishi mwenzake amekamatwa. Taarifa zote hizi ziko hadharani. Kasome ripoti iliyoandikwa na mwandishi wa Tanzania Daima, ametoa chronology yote kuanzia press conference ya asubuhi ambapo Daudi "alimuudhi" mkuu wa polisi hadi mauti inamfikia.
 
Hivi wewe Polisi tena FFu wanapotawanya watu unawata kwenda kuwauliza kwanini wamemshika fulani? kama si kujitafutia kifo ni nini? ulliona wapi hiyo duniani? Mahali wanapoingia riot police unaondoka, kama mwenzako kashikwa mfate kituoni, siyo pale.

Sasa uzembe kama huo unachokitetea ni nini?
 
Kuuliwa alijitakia mwenyewe, unakwendaje kmvaa mkubwa wa polisi wakati umeambiwa sambaratika.

Nasema hivi kwanini aandike mwandishi na asiandike mwana chadema, au lina impact na sympathy zaidi na ndiyo maana akachombezwa akafanye alichofanya? maana Slaa alikuwa anajuwa watakaidi, ushahidi ni ujumbe aliomtumia Mwema. Kama alijuwa watakaidi asijuwe na hao wakaidi waliowachombeza huko?

Ukweli ubaki kuwa ukweli.

Kwa hili la chaddema kuamrisha watu wavunje amani ili nchii isitawalike, hata wafanye nini, Watanzania walio wengi wanaelewa kinachiendelea na wala huu upuuzi hautoijenga chadema kama chama cha walio wengi.

Huyo alikuwa huko kwa kazi za chadema na alikuwa mmoja ya wailochombezwa na Slaa kufanya fujo.

CCM mnakata tawi la mti mlilokaliwa wenyewe.
Mwanga wa tochi hauwezi kuunguza nyumba.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom