Kutokwa na damu ukeni wakati wa mimba changa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,111
Hii ni hali inayoweza kujitokeza kwa mama mjamzito hasa katika kipindi cha umri wa mimba chini ya wiki ya 28. Baadhi ya sababu zinazoweza sababisha ni

i) Kutoka kwa mimba\

ii) Mimba nje ya mji wa uzazi

iii) Uvimbe ktk kondo la nyuma(placenta)

iv) Sababu za kienyeji

Leo ningependa tuiongelee kidogo maada ya utokaji wa mimba (Abortion) ikiwa ni moja ya sababu ya utokaji damu kwa mwanamke kwenye mimba changa.

Kutoka/kutolewa mimba (Abortion)

Hiki ni kitendo cha kutoa mimba kabla haijafikisha wiki ya 28 kutokana na sababu mbalimbali. Ikumbukwe kuwa katik anchi yetu kitendo cha kutoa mimba kwa makusudi ni kosa la jinai.

Ili kuzitambua sababu za kutoka kwa mimba ni vyema tukajua kwanza aina za utokaji wa mimba na ndipo tutajua na sababu zake.

Aina

Mimba inayotishia kutoka (Threatened abortion)

Hii ni mimba inayotihia tu kutoka ila haitatoka kama tahadhari zitachukuliwa mapema. Hii huwa na sifa zifuatazo;kutoka damu kidogo ukeeni na maumivu ya tumbo lakini njia (cervix) inakuwa haijafunguka.

Aina hii mara baada ya kuigundua inatakiwa mama huyu awe na mapumziko (bed rest) atumie dawa ya kutuliza maumivu na asifanye mapenzi.

Mimba ambayo ni lazima itoke( Inevitable abortion)

Hii ni mimba ambayo kwa namna yoyote ni lazima itatoka kwani njia ya kizazi huwa tayari imekwisha funguka na hivyo inaweza pelekea masalia ya mimba kutoka yote au kubakiza baadhi.


Mimba iliyotoka lakini imebakiza masalia yake (Incomplete abortion)

Huwa na sifa zifuatazo kwasababu ya yale masalia yaliyobakia;kutoka damu ya mabonge ukeni,maumivu ya tumbo,njia huwa imefunguka na mfuko wa uzazi huwa ni mdogo kuliko umri wa mimba

Mimba iliyotoka yote (Complete abortion)

Hii huwa imetoka yote bila kubakiza kitu

Mimba iliyotoka na kubaki uchafu ambayo imeshambuliwa na wadudu hususani bakteria (Septic abortion)

Hii inaweza tokana na mabaki ya mimba ambayo hajatolewa kitaalamu au kufanyika katika mazingira machafu na hivyo mama huyu atakuwa na homa, kutokwa damu kwa wingi, njia ya kizazi itakuwa wazi na atakuwa anatokwa na uchafu wenye harufu sehemu za siri.

Mimba kutoka mara kwa mara zenyewe ( Arbitual abortion)

Aina hii mara nyingi mimba zinakuwa zinatoka zenyewe na ni lazima iwe imejirudia zaidi ya mara 3 ktk historia ya mama.Ni muhimu sana kwa kila mama mjamzito kuhudhuria kliniki bila kujali hadhi yako.

Mimba ambayo imepoteza dalili zake ( missed abortion)

Inatokea kwa mama mjamzito kupoteza dalili za mimba wakati alikuwa mjamzito na tumbo lake la uzazi likawa dogo kuliko umri wa mimba.

Mimba inayotolewa kwa utaratibu wa kitiba ( therapeutic arbotion)

Hizi ni mimba ambazo zinatolewa kwa kitiba ili kunusuru maisha ya mama ama kutokana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaonekana kuhatarisha maisha ya mama. Hii inategemea sana maamuzi ya daktari na jinsi alivyoona.

Utoaji mimba usio salama/jinai/ (Unsafe/criminal abortion)

Utoji mimba hauruhusiwi katika nchi yetu na ndo maana unaitwa jinai lkini kitaalamu tunaita utoaji usio salama. Aina hii hufanyika kwa njia mbalimbali ambazo sitazitaja hapa kwasababu za kimaadili.

Makundi makubwa wanao fanya aina hii ambayo ni hatari kwa mtoaji na mtolewaji huwa ni wake za watu wasio waaminifu kwa ndoa zao, wanafunzi, wanaotumia vibaya uzazi wa mpango, waajiriwa wapya kama masharti ya kazi yamekataa, wanaotoka familia zenye misimamo mikali ya kidini lakini wao wamekiuka imani zao na wale wa mimbba zisizotarajiwa.

Hatari za utoaji mimba

zinazofahamika ikiwa ni pamoja na kupasua tumbo la uzazi, kutokwa damu nyingi na kupata maambukizi

Matibabu

Ni muhimu sana kumwona daktari hospitali au kliniki inayofahamika kisheria na utaratibu na si maduka ya madawa
 

Attachments

  • pre1.jpg
    pre1.jpg
    19.8 KB · Views: 1,253
Back
Top Bottom