Tatizo la kutokwa na damu kwenye fizi: Fahamu chanzo na namna ya kutatua tatizo hili

hadi sasa hivi naona bado kidude cha thnx.kama vipi nipe ya s.l.p yaaani ya kuandika
 
Jamani wataalamu habarini za kazi?

Jamani mimi nna tatizo la kuvimba fizi za meno kwa mda flani na baadae zinapona, zinakaa mda kama miezi miwili then zinauma na zinapona tena bila kutumia dawa yoyote.
wadau sababu ni nini?

MSAADA.......
Mbarikiwe wote
 
Jamani hapa ndani hakuna wataalamu wa kinywa (watu wa ent clinics) no answer up to now?
 
nadhani ni ukosefu wa vitamin c. tumia sour fruits (machachu nadhani) kama machungwa, malimao zaidi.
angalia pia kama unaumizwa na mswaki unaotumia,kama brush ni ngumu. kumbuka pia kubadili mswaki kila baada ya miezi walau miwili.
nb: meno wanahusika dentists, sio ent
 
Mkuu kuvimba kwa fizi ni kutokana na mpaka wako kati ya meno na fizi kujaa vyakula na kufanya fizi zako zishindwe kupumua. Ukiacha mda mrefu bacteria wanazaliana na kuanza kushambulia meno yako. Na mara nyingi ukiwa katika hali hio pia damu inaweza au huwa inatoka wakati wa kupigwa mswaki.

Muhimu kwa sasa nenda kwa daktari wa meno wasafishe meno yako na baada hapo piga mswaki mara mbili au kila baada mlo na pia toa vyakula vilivyonasa kwenye meno kila siku baada kupiga mswaki au kabla. Kuna mashine nzuri sana za kutoa mabaki ya vyakula ambavyo mara nyingi huwezi kutoa kwa kupiga mswaki peke yake zinaitwa water pik unaweza ku-google ukasoma zaidi. Sugua fizi zako taratibu kama unakanda kila siku wakati wa kupiga mswaki kwa kutumia mswaki laini.

Ukiacha hivyo baadae meno yako yanaweza kuanza kulegea na kung'oka. Baada kupiga mswaki pia sukutua maji ya chumvi( husaidia fizi kurudi kwenye hali ya kawaida) ya vugu vugu na kama damu inatoka wakati wakupiga mswaki sukutua kwa kutumia Hydrogen Peroxide hili uweze kuua bacteria.

Kumbuka kuskutua kwa maji ya chumvi peke yake haitasaidia kama huto endelea kupiga mswaki vizuri na ku-floss(kutoa mabaki ya vyakula) kila siku.

Kwa sasa nenda kwa daktari wa meno wasafishe na ukirudi fuatisha hayo maelezo na jenga tabia ya kwenda kusafisha meno yako kwa daktari kila baada miezi sita.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Wanajamvi naomba msaada wa haraka,maana mtoto wa dada yangu anaumwa amevimba fizi na zinatoa damu,mimi cjui tatizo ni nini,na yeye yupo chalinze vijijini sasa cjui nitoe kauli gani,tafadhali wana Jf doctor,mnisaidie kwa hili.
 
Usafi wa kinywa ni muhimu sana lakini pia msipoteze muda mkawaone wataalamu haraka sana. Na pia ajitahidi sana kula vyakula vyenye Vitamin C kama vile machungwa. Pia hali hii inaweza kusababishwa na upungufu wa damu.
 
Pole sana, mpeleke hospital watajua tatizo na atapata matibabu angekuwa dar ningekuelekeza pale mtaa wa jamuhuri karibu na kituo cha polisi kuna klinik nzuri sana ya wahindi nimeisahau jina lakini ukiulizia utaelekezwa, nilishapata tatizo hilo nikapata matibabu pale kuna dawa ya meno inaitwa protector utaipata hapo ni ghali kidogo na adimu lakini nzuri sana kwa vizi zinazo vimba na kutoa damu
 
Umri wa mtoto ni mdogo, probably ana ukosefu wa vitamin c. Mpeleke hospital then mpatie vyakula vyenye vitamic c, jamii ya machungwa, machenza,zabibu, nk. Pia kuna vitamin c supplements.
 
kwa muda sasa nimekua nikitoka damu kwenye fizi za meno kila ninapokua napiga mswaki, leo asubuhi wakati nakunywa chai ile nang'ata mkate nikaona damu kwenye mkate nadhani tatizo limekua kubwa. naombeni ushauri wenu kama kuna mtu mwenye idea ya hili tatizo na namna ya kulitatua.
 
Kuna dawa inaitwa Chlorhexamed, ni nzuri sana. Mimi pia nilikuwa na tatizo hilo nikaenda kwa dentist akaniandikia dawa hiyo. Nimeitumia mara mbili tu tatizo limeisha. iko kwenye tube ndogo kama zile za dawa za macho, na una massage ufizi kwa kutumia mswaki.

Ila pia kuna masharti: kila ukimaliza kula upige mswaki, na kabla ya kwenda kulala pia upige mswaki. Ukiweza kwenda kusafishwa meno kwa dentist pia itakuwa vizuri.

Ukiweza kupata dawa ya mswaki Parodontomax, ukaitumia pamoja na hiyo chlorhexamed basi utamaliza kabisa tatizo hilo.

Kila la heri.
 
Mkuu nenda kwa daktari wa meno ukasafishe meno.

Unauogonjwa wa fizi ambao unatoka na kutosafisha meno vizuri.hata ukitumia dawa ya meno hipi haitosaidia kwa sasa mpaka uende kwa daktari wa meno wakasafishe meno alafu ndio uanze kufuata njia sahihi za kusafisha meno.
 
Kasafishe meno hospitali. kwa kawaida tunatakiwa kukagua meno yetu kila baada ya miezi 6.
 
Back
Top Bottom