KUTOKA VIKINDU: Polisi wapambana na majambazi, askari mmoja adaiwa kuuawa

Soma kwa za hii post ya MshanaJe bado unahitaji maelezo mengine?
Zaidi ya kukuhurumia hakuna kingine.
hivi akili yako haifanyi kazi kujiuliza
hao polisi waende apo wafanye kazi ya kupambana na hewa na kutupa risasi bure eti kwa lengo la kudanganya wananchi isitoshe mpaka mmoja anauawa hivi watakuwa machizi ama wendawazimu??
we hujifikili kazi ya kushangilia ujinga tu aya ndugu nikuache undelee kuburudika na hiyo move kama mwenye unavo iita.
 
Ndo uhuru wenyewe huo. Maana kuna watu mpaka leo hawajui kufa kupo au Mungu yupo mapka waone mwenyewe.
Hiyo Mimi naona Ni scene ya kutengeneza, sidhani kama hao majambazi kama watakuwepo,wahusika watakuwa wamesha tokomea kitambo sana.
 
Hawanaga
Mkuu umefikiria mbali sana, aliyeleta wazo la dini amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwa fool wengi,

mimi naongezea pia walioandika Biblia na Qur'an walitumia akili kubwa sana kwavile yaliyoandikwa mle ni story kama story zingine, lakini watu wapo tayari kuzifia story zile pindi unapo wa-challenge.
Wanakosaga cha kujibu zaidi watakutisha tu na mwisho wa siku wanakuambia ngoja ufe utaona hahahaha hua nacheka sana nikifikaga hapo wanashida sana hawa
 
Inasikitisha sana, nahisi hawa polisi walipewa taarifa na raia mwema kuwa hiyo nyumba kuna watu waalifu, wakaamua kuwazukia. Ila nachoshindwa kuelewa imekuwaje ndani ni hao waliokuta na hizo risasi walisopiga walikuwa wanajibishana na nani haswa. Sijui yaliyotokea ni woga na kiwewe cha mauaji ya wenzao, achene jamani wenzentu ni kazi tu kila mtu anaogopa kifo
 
Risasi zarindima kwa saa 7 Mkuranga

IMEANDIKWA NA MROKI MROKI, MKURANGA
IMECHAPISHWA: 27 AGOSTI 2016


MAJIBIZANO ya risasi baina ya polisi na majambazi yaliyodumu kwa takribani saa saba kuanzia saa 8:20 usiku wa kuamkia jana Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mkuranga mkoani Pwani, yamesababisha vifo vya watu wawili, akiwemo askari Polisi na mtu mwingine anayedaiwa kuwa ni mtuhumiwa wa ujambazi.

Mbali ya milio ya risasi, mtaa huo pia ulitanda moshi kutokana na mabomu ya machozi yaliyopigwa mfululizo na kuibua taharuki kubwa kwa wakazi wake. Mmoja wa majirani katika nyumba iliyozingiwa waliyoishi watuhumiwa, Mjenge Faki alisema walishtuka usingizini na kuanza kusikia milipuko ya risasi na ghafla wakaanza kutokwa na machozi kufuatia hewa hiyo ya machozi kuanza kusambaa.

Katika majibizano hayo, askari aliyekuwa katika mapambano na mtuhumiwa, walikufa papo hapo. Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventure Mushongi, licha ya kuwepo eneo la tukio, hakuwa tayari kuzungumzia lolote, akisema mwenye jukumu la kuzungumzia tukio hilo ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro.

Naye Kamanda Sirro akizungumzia hilo, alisema taarifa kamili za tukio hilo zitatolewa leo, kwani bado wanakusanya taarifa kuhusiana na tukio hilo. Lakini Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema katika mapambano hayo, Jeshi la Polisi limepoteza askari mmoja, lakini bado liko imara na litaendelea kuwasaka wahalifu popote watakapokuwepo.

“Askari wetu akiwa katika shughuli zake za kupambana na majambazi ameuawa hapa leo (jana) usiku, ni tukio baya katika wilaya yetu, katika mkoa wetu na ni tukio baya sana katika nchi yetu. Hawa ni wahalifu, lakini mbaya zaidi hata familia na watoto wao inaaminika wana mafunzo maalumu ya kulinda wazazi wao ambao ni wahalifu,” alisema Ndikilo.

Aliongeza kuwa, kama wahalifu hao walidhani kwa kuua askari watakuwa wametimiza malengo yao, basi wamechelewa kwani watawawinda popote pale watakapokwenda. Kwa mujibu wa Faki, milio ya risasi na mabomu ilisikika katika nyumba inayosadikiwa kumilikiwa na mkazi wa Temeke, aliyetajwa kuwa ni Salum Kingungo, majira ya saa 8:20 usiku.

“Tulianza kusikia kama watu wanakimbizana kutoka eneo la juu barabarani na kelele hizo zikaja kuishia ndani ya nyumba hii ambapo yalianza kusikika majibizano ya risasi baina ya watu walioko nje na mingine kutoka ndani, lakini hatukuweza kujua kinachoendelea kwani tulijawa na hofu kubwa ya kinachoendelea,” alisema Faki.

Alisema alishindwa kutoka nje na hata walipofanikiwa kubaini kuwa ni askari, hawakuruhusiwa kutoka nje hadi ilipotimu saa tano asubuhi. HabariLeo ilifika eneo la tukio na kushuhudia idadi kubwa ya polisi waliovalia sare wakiwa na silaha za aina mbalimbali huku wakiwa wametanda katika eneo hilo wakiongozwa na Kamanda Mushongi.

Katika majibizano hayo ya risasi na mabomu, nyumba inayodaiwa yalikuwa makazi ya watuhumiwa hao, iliharibiwa vibaya. Baada ya hali kutulia, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Ndikilo akiwa na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani, alipata fursa ya kuzungumza na wananchi.

Baada ya kutembelea nyumba hiyo na kujionea hali halisi ilivyokuwa, aliwataka wananchi wa Mkuranga na mkoa wa Pwani kwa ujumla kuwa watulivu kwani serikali imejipanga kupambana na watu wachache wasio waaminifu, ambao wamekuwa wakivuruga amani na utulivu.

Aliwataka wananchi wenye taarifa zozote za uhalifu kufika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkuranga au ofisini kwake huku akiahidi kutoa zawadi ya Sh 300,000 kwa mtu atakayewezesha kukamatwa kwa wahalifu. Pia aliwataka kuimarisha ulinzi, ikiwa pamoja na kujiwekea utaratibu wa kufahamu nyendo za majirani zao.

Taarifa za awali kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mohammed Maundu alisema watu saba kutoka katika familia hiyo wanashikiliwa na Polisi ambapo kati yao wanawake wawili, mwanamume mmoja na watoto ni wanne akiwemo mwenye umri wa miezi miwili.

Wananchi wa eneo hilo walisema tangu wakazi hao wahamie katika nyumba hiyo miaka mitatu iliyopita, hawajawahi kuwaona nje wanawake hao na hata wakionekana ni nadra sana na muda mwingi wamekuwa wakiwaona wanaume wawili na watoto hasa wa kiume mwenye umri wa miaka kati ya saba na 10, ambaye alikuwa haendi shule, lakini akiwa anatumwa dukani na kurudi ndani.

“Sisi hata siku moja hatujawahi kuwaona wamama wenzetu wa nyumba hii, lakini mara zote tukiona wanaume wawili mmoja mweupe na mwingine mweusi mfupi wakichota maji na kununua mahitaji tu lakini tulikuwa hatuwaelewi kutokana na mwonekano wao,” alisema mmoja wa majirani, Bahati Mawinga.

Baadhi ya watoto na akinamama waliokuwa eneo la tukio, walisema moshi wa kuwasha uliotokana na mabomu ya machozi ulisababisha watoto kulia usiku kucha na kutapika. Tukio la Vikindu limekuja siku nne baada ya askari Polisi wanne waliokuwa wanaingia kazini, kuuawa katika shambulio lililofanyika katika eneo la benki ya CRDB, Mbande, wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam

habari leo online
 
Yaan mkuu nilicheka mpaka basi,,unajua ukitaka kucheza sinema lazima kwanza u plan sinema yako itakuaje sawa sawa,, sasa jamaa zangu hua wakiamka wanakurupuka tuu..binafsi mm kidogo nilikua namkubali kova kwa visinema vyake mwenye akili unajua ila ilikua sio rahisi kama hawa jamaa...asikari aliepigwa risasi jana mbona hata picha tuu hakuna,,wale wa mwanzo picha zilikua kila mahali,, hiivi kwel inaingia akilini kama wanavyosema kwamba askari kanal mstaaf...ambae alikua sniper afanye tukio la namna ile alafu aende akajivundike na wenzake wengi kwenye nyumba moja?? Nyumba yenyewe ilikua imezungukwa na wao kabla kurushiana risasi hazijaanza, na tushukuru mungu kwamba eneo lilikua la makaz ya watu waliona kila jambo la sivyo wangesema tushamuua, huyo jamaa katorokea wap?? Basi wangewaacha waandiahi wa habari wakaingia watuonyeshe labda kuna underground tunnel kama zile za drug dealer kule mexico ndani ya hio nyumba
kucheka na kupumua ndo saizi yako..mambo ya usalama waachie wenyewe...ulitaka uone pcha za za maiti ya kamanda wa polisi ili ikusaidie nn...wewe kula kyepe lala ..wanaume wanakufa coz they r protecting ur sleeping ass...STUPID
 
Mi nilikuwa najiuliza hao majambazi walikuwa wajinga kiasi gani eti wakajilundike wote sehemu moja kama ndege kwenye kiota hadi wakamatike kwa pamoja hivyo
 
swali langu ni hivi polisi wameizingira nyumba alafu wameishambulia kwa masaa 8 hiyo nyumba halafu wametoka watu hai tena wakina mama hapo bado sijaelewa kabisaa kwa jinsi nnavyojua bunduki ikishambulia nyumba kila pembe hakuna wakupona aliyeko ndani ya nyumba
 
Sinema zote zinakuwa na mpangilio, beggining-middle-end.
MWANZO: majambazi yanashambulia polisi
KATI:polisi kibao ndani ya defender 16 wazingira nyumba yenye uzio mrefu na kurushiana risasi na majambazi mfulululizo masaa zaidi ya Saba - Oh my God mrehemu marehemu.
MWISHO: Suspense .............
mihemko itakuja kukucost sikumoja...
 
swali langu ni hivi polisi wameizingira nyumba alafu wameishambulia kwa masaa 8 hiyo nyumba halafu wametoka watu hai tena wakina mama hapo bado sijaelewa kabisaa kwa jinsi nnavyojua bunduki ikishambulia nyumba kila pembe hakuna wakupona aliyeko ndani ya nyumba
Walijificha nyuma ya TV, TV zenye chogo ni bullet proof
 
Huu ni mzuka tu uliowafanya polisi "kufanya uharibifu wa nyumba" wakati ndani kuna watoto na wanawake, haa! halafu askari kauwawa kwa risasi kwenye MAPAMBANO, hakuna silaha iliyopatikana kwenye hiyo nyumba, nani kamuua huyo marehemu?!
 
Huu ni mzuka tu uliowafanya polisi "kufanya uharibifu wa nyumba" wakati ndani kuna watoto na wanawake, haa! halafu askari kauwawa kwa risasi kwenye MAPAMBANO, hakuna silaha iliyopatikana kwenye hiyo nyumba, nani kamuua huyo marehemu?!

Hahaha! Marehemu hauawi akishauawa ndo anakuwa Marehemu!
 
Back
Top Bottom