Kutoka TANESCO: Taarifa kwa vyombo vya habari

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
1629mvd.jpg

aeobjt.jpg

ddls1l.jpg

2dbjt53.jpg
 
Hongera kwa kuanza na hilo i.e. kukusanya madeni,.....anza na idara za serikali, maana pesa wanazo za kuwafadhili hata Brazil.................lol

Komaa pia na wanasiasa wasikuletee mikataba ya hovyo hovyo...............
 
Nakubaliana na Ogah kwamba waanzie serikalini, mashirika ya umma na makampuni makubwa kwanza -- na baadaye ndiyo makabwela.
 
Hivi kwa nini wasi invest kwenye LUKU hasa kwenye idara/taasisi za seriakali? Postpayment plans ndio hasa zinaidumaza TANESCO hasa kama wateja (serikali na taasisi zake) wanadefault kulipa.

Ukiangalia makampuni ya simu yamefanikiwa sana kwa sababu kwa sehemu kubwa wateja wanalipia huduma kabla na hivyo kufanya ukusanyaji wa mapato kuwa rahisi.

Kwa maoni yangu LUKU ni njia ambayo ingewarahisishia sana TANESCO ukusanyaji/udhibiti wa mapato. TANESCO ni mojawapo ya taasisi zinazofanya biashara ambayo mpaka sasa haina ushinani wowote wa kutisha.
 
Kukusanya madeni na kwenyewe ni kampeni? Huo si wajibu wao wa kila siku! Sasa kampeni ikiisha ina maana kuwa watasubiri hadi kampeni nyingine ili wakusanye madeni yao? Wao wangekaa na kujiuliza kwa nini watu hawalipi madeni yao halafu wafanye mpango wa kuwarahisishia kulipa. Kumkatia mtu umeme si jawabu maana unajipunguzia mapato! Naona huyu mtu mpya anaendeleza yale yale ya kuendesha shirika kibabe. Angekaa na kutueleza atafanya nini kuondoa au kupunguza kero wanazopata wateja wake badala ya kukomalia kitu ambacho hakina haja ya kampeni!

Amandla.......
 
Wakifuatilia uadilifu ufuatwe, kama watanikatia mimi pangu pakavu mwenye deni la laki moja basi na vigogo pia wawakatie huo umeme, la sivyo somo litakuwa kugumu kueleweka kwa wengine :painkiller:
 
Hongera kwa kuanza na hilo i.e. kukusanya madeni,.....anza na idara za serikali, maana pesa wanazo za kuwafadhili hata Brazil.................lol

Sasa hilo swala la Brazili limekukera au limekufanya uwe "laughing out loud"?

Kuna siku Kikwete alikwenda California akakutana na Watanzania, akawapa habari kwamba kilio chao cha swala la uraia kwa sasa limepigwa chini kwa sababu waamuzi wanaona "mnataka kula huku na kule." Watanzania kwe kwe kwe kwekweee kwe kwe...

Khaa, Wabongo hawa wamedumaa vichwa nini? Wametoka kupewa habari wasioitaka halafu muitikio wao ni kwe kwe kwe kwe.... vicheko kupindukia.

Kuna mambo mengine yanahitaji kukaza uso kwa hawa viongozi sio kuwalegezea legezea!


...Huo si wajibu wao wa kila siku! ... Wao wangekaa na kujiuliza kwa nini watu hawalipi madeni yao halafu wafanye mpango wa kuwarahisishia kulipa. Kumkatia mtu umeme si jawabu maana unajipunguzia mapato! Naona huyu mtu mpya anaendeleza yale yale ya kuendesha shirika kibabe. Angekaa na kutueleza atafanya nini kuondoa au kupunguza kero wanazopata wateja wake badala ya kukomalia kitu ambacho hakina haja ya kampeni!

Amandla.......

Na kumpa mtu umeme wa bure pia hakutawaongezea mapato.

Na huwezi kudhani tu kwamba uamuzi huu ni mpango mpya wa Mkurugenzi aliyekuja mwanzoni mwa wiki.

Na huwezi kudhani tu kwamba Tanesco hawajakaa na kujiuliza ni kwa nini watu hawalipi.

Na huwezi kudhani tu kwamba watu hawalipi kwa sababu Tanesco haijawarahisishia jinsi ya kulipa.

Inawezekana wameona ni kwa sababu hawashurutishi ulipaji ikiwa ni pamoja na kusitisha huduma.
 
Na kumpa mtu umeme wa bure pia hakutawaongezea mapato.

Na huwezi kudhani tu kwamba uamuzi huu ni mpango mpya wa Mkurugenzi aliyekuja mwanzoni mwa wiki.

Na huwezi kudhani tu kwamba Tanesco hawajakaa na kujiuliza ni kwa nini watu hawalipi.

Na huwezi kudhani tu kwamba watu hawalipi kwa sababu Tanesco haijawarahisishia jinsi ya kulipa.

Inawezekana wameona ni kwa sababu hawashurutishi ulipaji ikiwa ni pamoja na kusitisha hudu
Nani kasema watoe umeme bure? Au unataka kutafuta sababu tu ya kupinga fikra sahihi za Fundi Mchundo?

Kampeni za kukusanya madeni hazijaanza leo. Kama vile ilivyokuwa kwa hao wanaotuletea maji, imekuwa kawaida kila kiongozi kuonyesha umahiri wake kwa kuandaa kampeni za kukusanya madeni! Bila shaka watu wanalipwa posho kwa ajili ya kazi ya ziada wanayofanya wakati wa kampeni hizi. Kinachonishangaza mimi ni kuwa pamoja na kampeni hizo lukuki, bado tatizo liko pale pale. Ndiyo maana nikasema waangalie sababu za watu kulimbikiza madeni. Wakati nilipokuwa na umeme nyumbani kwangu, ilibidi siku ya kwenda kulipa umeme uache shughuli zako zote, ukakae foleni kuwabembeleza wapokee visenti vyako. Zaidi ya hapo ni mara nyingi tu walikuwa wanakisia matumizi. Utakuta mtu ambae hata pasi anatumia ya mkaa anabambikwa bili ya ajabu. Ukilalamika ( na hilo zoezi la kulalamika ni siku nzima) unaambiwa ulipe kwanza, ndiyo watakusikiliza. Kharaha zote hizi ndizo zimechangia wengi kukata tamaa na kutolipa. Inabidi waandae utaratibu mzuri wa kulipia umeme na kushughulikia malalamiko pale yanapotokea! Badala ya kuangalia namna gani wapanue wigo la watumiaji wa umeme wao wanakimbilia kumkamua huyo aliyediriki kuunganishiwa umeme.

Sasa kwa mawazo yako, Fundi Mchundo ana haki ya kudhani nini katika suala hili? Huyu mheshimiwa katumia kikao chake cha kwanza kuzungumzia hili kwa hiyo inaonyesha ni priority yake hata kama alilikuta. Kwa vile yeye ndiye MD basi maamuzi yote ya kitu gani akipe kipaumbele ni ya kwake. Na akitoa tamko ni la kwake na sisi tuna haki ya kuichambua tunavyotaka. Wewe kama una mawazo tofauti, ni haki yako lakini si haki yako kumwambia Fundi Mchundo nini cha kudhania. Inabidi ukue, kutofautiana kwenye ishu haina maana ya uadui mpaka kila mahali tutafutane. Hautafika mbali hivyo maana hapa si mahala pake. Utaharibu jamvi bure!

Amandla.......
 
Mipango mizuri sana... tatizo ni utekelezaji.

Tatizo kubwa pia ni siasa na wanasiasa. Sasa hivi ataundiwa zengwe akianza kuwagusa wanaoitwa wakubwa, maana wengi wao wanapenda kujilipa vizuri na kupenda vya bure hasa katika huduma za jamii kama umeme. Wanajiona wao ndiyo Tanzania na kila kilichomo. Mnakumbuka sakata la dr. Iddrisa na Kiwanda cha Saruji?
 
Nafikiri Iddrissa rashidi alitaka kujiuzuru kwa sababu ya kukata umeme kwa mafisadi sasa tusubiri tuone
 
Anyways I remain doubtful on the following accounts

1. Huyu mkurugenzi mpya ametokea humo humo Tanesco where he's been working for more than 20 yrs, na kwa taratibu za kibongo hususan Tanesco ni very likely atakuwa ni mla rushwa mzoefu, mtoro, master wa forgeries, mwizi to say the most........ In short hana jipya and that is why anaanza na mikwara ileile kwa utaratibu ule ule na kwa watu walewale.

2. Tatizo kuu laTaneso ni kuendeshwa kisiasa na in the mean time hatujasikia mabadiliko yeyote kukinzana na hali hiyo and this is by far not chini ya mkurugenzi wa Tanesco.

Anyways time will tell.
 
Nani kasema watoe umeme bure?

Huyu nani:

Kumkatia mtu umeme si jawabu maana unajipunguzia mapato!

Ukitoa umeme bure ndio utaongeza mapato? Hujajibu, unalia!

Naharibu jamvi, nakufatafata. Nakunyima haki yako ya kudhaniadhania.

Ume assume TANESCO hawakuwa na mpango wa kushurutisha ulipaji ankara kabla ya ujio wa Mkurugenzi mwenye wiki, umetumia assumption kukosoa Mkurugenzi mteule.

Ume assume TANESCO hawajui kwa nini watu hawalipi ankara, umetumia assumption kukosoa mpango kazi wa kampuni. Unatumia assumption kukosoa halafu unasema una haki ya kudhani dhani bila kuambiwa dhihirisha, huna. Sasa usilie, ni hivi:

Hili ni jamvi la vina vya mahojiano. Sio Facebook hapa. Sio jamvi la Jay Dee hili, sio Michuzi. Kama Fundi Mchundo analia kwamba anaesaili alichokisema anamfatafata basi kweli jamvi limepelea, limepwaya. Na akina mimi tunaonekana tunaharibu jamvi. Mnataka palegee legee pawe nini, "Twitter" hapa?

Mjadala tuliokuwa nao kwingine sikudhani unahusiki hapa. Lakini kama unahusika basi anaeharibu ni yule aliyemwambia mwenzake akafikiri kwanza au anyamaze! Hizo ndio fikra ndefu? Kwa wenye nywele hilo ni tusi. Unasema sitafika mbali, unajuaje nilipo? Na nilipofika unajuaje ninapotaka kwenda?

Ulishasema unapoteza muda “kubishana,” basi ukiona yangu yapite. Ila ukihubiri michongo imepindapinda, imejaa ma assumption pasi vina wengine watayabwia, si wote.
 
Huyu nani:



Ukitoa umeme bure ndio utaongeza mapato? Hujajibu, unalia!

Naharibu jamvi, nakufatafata. Nakunyima haki yako ya kudhaniadhania.

Ume assume TANESCO hawakuwa na mpango wa kushurutisha ulipaji ankara kabla ya ujio wa Mkurugenzi mwenye wiki, umetumia assumption kukosoa Mkurugenzi mteule.

Ume assume TANESCO hawajui kwa nini watu hawalipi ankara, umetumia assumption kukosoa mpango kazi wa kampuni. Unatumia assumption kukosoa halafu unasema una haki ya kudhani dhani bila kuambiwa dhihirisha, huna. Sasa usilie, ni hivi:

Hili ni jamvi la vina vya mahojiano. Sio Facebook hapa. Sio jamvi la Jay Dee hili, sio Michuzi. Kama Fundi Mchundo analia kwamba anaesaili alichokisema anamfatafata basi kweli jamvi limepelea, limepwaya. Na akina mimi tunaonekana tunaharibu jamvi. Mnataka palegee legee pawe nini, "Twitter" hapa?

Mjadala tuliokuwa nao kwingine sikudhani unahusiki hapa. Lakini kama unahusika basi anaeharibu ni yule aliyemwambia mwenzake akafikiri kwanza au anyamaze! Hizo ndio fikra ndefu? Kwa wenye nywele hilo ni tusi. Unasema sitafika mbali, unajuaje nilipo? Na nilipofika unajuaje ninapotaka kwenda?

Ulishasema unapoteza muda "kubishana," basi ukiona yangu yapite. Ila ukihubiri michongo imepindapinda, imejaa ma assumption pasi vina wengine watayabwia, si wote.

Kusema kumkatia mtu umeme si jawabu hakuna maana kuwa wampe umeme bure. Wapi niliposema deni lake afutiwe? Wapi niliposema huo umeme atakaoendelea kutumia hautaongezeka kwenye deni lake? Usipende kupindisha maneno yangu katika kutafuta umaarufu. Sasa wakimkatia mtu umeme ndiyo wanaongeza mapato? Kwa vipi? Wako watu ambao baada ya kukatiwa umeme kwa kile walichoona ni uonevu wameamua kutafuta njia mbadala kama solar n.k. Hapo Tanesco wanafaidika vipi?

Kwa mtazamo wako kwa vile mimi siko Tanesco na sina uhakika kuwa ninachoshauri wafanye hawajafanya basi ninyamaze? Sasa wewe mbona una-assume kuwa wamefanya hicho unachosema? Kama una hakika kuwa sikuwatendea haki, jibu kwa hoja. Niambie kuwa assumptions zangu si sahihi kwa sababu kwenye kikao kadha wa kadha walipanga mkakati fulani ambao ulijibu hoja zangu. Kunipinga ati kwa sababu una assume nime assume ( maana hauna hakika kuwa sijui ninachokisema maana haunijui) ni dalili kuwa ulikimbilia kujibu bila kufikiri kwanza!

Siwezi kukulilia. Wewe si wa kwanza na hautakuwa wa mwisho kudhani kujibishana na Fundi Mchundo. Nimekupa ushauri wa bure, ni juu yako kuufuata au kuupuza. Either way kwangu mimi hainipunguzii wala kuniongezea kitu. iNimekuwepo hapa kitambo cha kutosha kiasi cha kutokukuhitaji wewe unifahamisha hili jamvi linaendaje. Huko kwa wakina Facebook, Jay dee na Michuzi sijawahi kuwepo wala sina mpango wa kwenda. Na "Twitter" ndio nini? Mimi nampima mtu kwa kile anachochangia na mpaka sasa (kwa mtazamo wangu) hamna cha maana ulichoongea zaidi ya kunichafulia jamvi.

Hautafika mbali kutoka popote ulipo maana haka katabia ni juvenile. Utabakia hivyo hivyo ukiendekeza tabia hiyo.

Kule kwengine hatukuwa na mjadala bali mabishano. Mimi ndio maana nikakwambia unanipotezea muda. Naona hapa unataka kuleta yale yale. Kubwia au kutobwia michongo yangu ni uamuzi wako. Nipinge kwa kutumia hoja, tutajadiliana. Lakini kuja na inane arguments kuwa ati kwa sababu nimetumia assumption katika argument yangu kwa hiyo ni moot kwangu mimi ni kuleta ubishi usio na maana. Kama nilivyofanya katika mabishano yetu mengine, sitaku-entertain kwa kuyaendeleza. Muda wa ku-suffer fools gladly sina. Kama nilivyoisha kukuambia tena, unanipotezea muda!

Amandla........
 
nafikiri wafanye oparesheni nyingine kubwa ya kutatua tatizo la kukatika umeme ovyo ovyo bila sababu maalumu na kurudi mda wowote na kutatua tatizo la luku kila mara ukienda kununua unakuta network akuna siku 3-5 nimewahi kulala giza marakibao yani
 
Back
Top Bottom