Kutoka ITV: Mjadala kuhusu DOWANS; wachangiaji wataka maandamano nchi nzima

"Wanafunzi wa UDOM hawana akili" - Mkinga (akimaanisha wale waliomchangia mgombea wa chama "chao" 1m). Bravo Mkinga.
 
kuna mdau mmoja kachangia kasema juu ya sheria kuna katiba ya nchi na juu ya katiba kuna Wananchi
sheria sio kitu ila wananchi ndio kila hivyo tunaweza kufanya kila kitu tukitakacho katika katiba na sheria hivyo maamuzi ya sheria sio kitu kwetu ilamaamuzi ya wananchi ndio ya kuyasikiliza.
 
Ndugu yangu Dr. Slaa, nimefuatilia mjadala wa malipo tata kwa Dowans ITV, you are a potential presidential candidate and our inspired president candidate, why so quite regarding this issue! ?

It is so dissappointing to note that neither you nor any top official from your party has recently took trouble on discussion regarding this very partinent issue, you real should be on top of these burning issue as will enhance our confidence in you and your part at large.
 
Mkuu pamoja na kwamba siungi mkono malipo hayo lakini pia sioni DOWANS wamevunja sheria gani. Kama wangevunja sheria basi mahakama isingebariki hayo malipo. Tatizo si la DOWANS tatizo ni la viongozi wetu walioingia mkataba mbovu ambao kisheria una nguvu.

kaka mimi si mtaalamu wa mambo ya sheria,yawezekana ukawa sasahihi
lakini niseme tu siku zote kinapotokea kitu angalia source ili ikuongoze katika kutafuta solution
kaka mkumbuka mwizi wa mali na mnunua mali wot wana hatia
naomba unielewe kama ni kulipwa dowans walipane hukohuko walipokutania na si kwa fedha za watanzania,mi sitaki kujua nani kavunja sheria nasema ushenzi wao wapeleke huko si kwa fedha za mlipa kodi never ever
 
mama Ananilea Nkya katusihi watanzania wote wenye uchungu tufanye haraka kabla ya rufaa ya dowans tuingie barabarani nchi nzima kupinga malipo haya ya kihuni! watanzania tupo tayari au ni maneno matupu?
 
Mkuu Slaa tena aseme nini ? It is time kwa Watanzania nao kusema na waache kusemewa kila siku .Naye ni mtu ana angalia kama na sisi sote tuna uchungu au tunamwacha yeye aseme then tuseme hana issue kila siku downs nk? Now it is our time yeye atakuja kumalizia .
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Ndugu wana JF nimepata hamasa baada ya kumsikiliza mama NANILEA NKYA ambaye yuko live ITV ameshauri tuandae maandamano makubwa kupinga kulipa deni haramu la DOWANS.

Napendekeza tuandae maandamano haya siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Nyerere, 14/10 ili kumuenzi mwalimu.

CDM tunaomba mtupe muongozo.

Nawasilisha.
hamna haja ya kulifanya hili jambo ni la cdm, maana wapo ccm, ccj nk nk wanaolipinga hili suala, hivyo ni vizuri likawa la waTz wote wanaopinga huu wizi?
hivi jamani kwani wenzetu wanaweza sisi bado angalia Satta wa Zambia na kurudisha Benki iliyo uzwa kwa rushwa mikononi mwa Serikali, M7 sasa hivi kamtia ndani VP mstaafu, Uganda Wabunge 1/3 wamemlazimisha Spika Kadaga kuitisha bunge kwa dharura kujadili Oil Deals (contract),
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Dr Slaa wewe ndiye rais wangu mpaka sasa kwakua ni mmoja wa wasiotambua ushindi wa kikwete katika uchaguzi uliopita

Je, umesikia kauli ya mama Nkya upo tayari kuhamasisha watu tufanye maandamano ya amani please nasubili kauli yako tumechoka
tusaidie kutafuta vibali kisha alikeni watu tupo tayari.
 
Umeme wakatika ghafla wakati akizungumza mkinga ITV, je ni mgao? au hujuma wa tz tusipate kufunguliwa macho?

Ndugu wanajamvi ninapokaribia kukata tamaa na nchi yangu huwa nakumbuka ukweli na haki haviwezi kushindwa, nchi yetu imejaa watu wezi na katili sana kwa wananchi wao,LAKINI pamoja na umeme kukatika waTz hatujalala kiivyo na hakuna anayeweza kutufumba watz macho.
 
Hili deni hata kama likilipika wachawi wetu ni wale wapumbavu waliokubali kusaini makubaliano eti kitakachoamuliwa na huyo mslulishi wao uchwara hakitakua na rufaa.

Hivi jamani utasaini vipi ushenzi kama huu? Tuseme labda kiengereza kilichotumika hakiueleweka? Nani huyu aliesaini haya makubaliano?
Bado anaishi mpaka sasa? Anajiskiaje?

Kama kweli bado yupo na anakula kuku tu mjini basi elimu ya "kujitoa mhanga" itakua haijaingia kabisa hapa kwetu, maana lasivyo tungekua tunaongea habari ingine muda huu!!
 
Vibali vitacheleweshwa mpaka malipo yafanyike tayari.. Kibali ni uamuzi wako, wao wanatengua sheria n why should we worry kuhusu kuandamana?
Twende Barabarani hata kesho asubuhi wengine watatufuata
 
Wawajibishwe wote waliolifikisha taifa hapa! Nguvu ya umma inahitajika. hakuna sheria itakayopindua maamuzi hayo kwani mfumo mzima umeoza1
 
...tatizo nyie mlie nje ya system inawauma sana kuona wachache ndani ya system wanakula kuku kwa mrija.

Mi naamini watanzania wengi ni wabinafsi na mafisadi ila hawajapata nafasi tu. Mfano, mzazi anampeleka mwanae shule na kumsisitiza asome kwa bidii ili awe na maisha bora na aweze kuwasaidia wadogo zake...ona hapo mtoto anapo lishwa sumu ya ubinafsi. Nani anamsisitiza mwanae asome ili aje kuitumikia nchi yake?

...mi naomba niwe muwazi. Nikipata nafasi ya kula ntakula haswaaa....tena hata hilo deni la dowans na issue nyingine wala haziniumi coz najua hata ningekua mimi kwenye hzo nafasi ningefanya the same....tuacheni roho mbaya jamani, eti wengine wanataka maandamano...huo ni wivu. Leo mnataka maandanano coz hayawafika nyie, kwanza jichunguzeni nyie je ni wasafi?
 
Ndugu yangu Dr. Slaa, nimefuatilia mjadala wa malipo tata kwa Dowans ITV, you are a potential presidential candidate and our inspired president candidate, why so quite regarding this issue! ?

It is so dissappointing to note that neither you nor any top official from your party has recently took trouble on discussion regarding this very partinent issue, you real should be on top of these burning issue as will enhance our confidence in you and your part at large.

Dr Slaa wewe ndiye rais wangu mpaka sasa kwakua ni mmoja wa wasiotambua ushindi wa kikwete katika uchaguzi uliopita

Je, umesikia kauli ya mama Nkya upo tayari kuhamasisha watu tufanye maandamano ya amani please nasubili kauli yako tumechoka
tusaidie kutafuta vibali kisha alikeni watu tupo tayari.

Kwa akili hizi..hakika bado kuna kazi kubwa ya kuwaamsha waTZ toka usingizini...
Yaani mpaka sasa nyie mnasubiri Dr. Slaa ndie ahamasishe watu wafanye maandamano? Hadi sasa hamjafahamu haki zenu kama raia? Mnataka mpaka mzee wa watu aje awapige makonzi mabichwa yenu?!
 
Ndugu wana JF nimepata hamasa baada ya kumsikiliza mama NANILEA NKYA ambaye yuko live ITV ameshauri tuandae maandamano makubwa kupinga kulipa deni haramu la DOWANS.

Napendekeza tuandae maandamano haya siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Nyerere, 14/10 ili kumuenzi mwalimu.

CDM tunaomba mtupe muongozo.

Nawasilisha.
Kwani lazima Chadema hivi vyama vingine viko wapi kutetea masilahi ya taifa.
 
Back
Top Bottom