kutoka bungeni, my best quote of the day

Negotiator

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
303
44
"Mwisho, Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali iwaeleze Watanzania juu ya hatua, kama zipo, ilizozichukua kuzuia ukiukwaji huu wa Makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba. Na mwisho, Serikali itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu kama - kwa ukiukwaji huu wa Makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano – Bunge hili tukufu litakuwa ndani ya mamlaka yake kuchukua hatua za kumshtaki Rais kwa mujibu wa ibara ya 46A ya Katiba kwa kushindwa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Muungano kama kiapo cha kazi yake kinavyomtaka."

Hii ni nukuu ya aya ya tatu kutoka mwisho ya maoni ya kambi rasmi ya upinzani ofisi ya rais Muungano kama ilivyowasilishwa na Tindu Lissu leo bungeni.
 
muungano kila siku wa nn tuwape znz yao
tumechoka na kelele wakat tunanyonywa ss bara cz wao wapo wachache alafu wanataka kila ktu sawa
 
Jinsi shughuli za bunge zinavyoendeshwa mpaka sasa nashindwa kujua ni Speaker hajui kanuni na taratibu za bunge ama ni wabunge ndiyo hawajui, Kwani ukibahatika kuangalia jinsi vurugu mechi kabla mmoja hajamaliza mwongozo ushaombwa kabla moungozo haujajibiwa mwangine anaingilia na kuhusu utaratibu.
Aaaaargh.......... tired of this.
 
Rais anapaswa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ila kama muungano utaonekana ni kero kwa pande zote mbili basi tutengane tu, tubaki nchi mbili jirani.
 
Back
Top Bottom