Kutoka Bungeni: Maswali ya Papo Kwa Papo kwa Waziri Mkuu!

Hiki kipindi cha maswali na majibu hakina faida yeyote yani waziri mkuu anajibu simple sana yani sijui nisemaje jamani dah! Mfano,serikali itachukua hatua gani kwa sumatra jibu.yaliyopita c ndwele ila uchunguzi bado unaendelea ukimalzka tutachukua hatua stahiki yani hapo mtu mzima ndo kajibu tayari mi kiukweli siridhiki kabisa na Mizengo pinda jamani.
 
Waziri Mkuu ,MIZENGO PINDA amesema Siyo mgomo uliosababisha baadhi ya Walimu kutochukuliwa katika zoezi la sensa.
Waziri mkuu amesema hoja iliyotumika ni kuyapa fursa makundi yote (Walimu, wanafunzi walihitimu shule na whitimu wa vyuo vikuu ambao hawana kazi) kutumia fursa hiyo.
Hawa nao watawajumuisha kwenye idadi ya ajira walizotoa, serikali ya kisanii sana hii.
Lakini kama si mgomo mbona mwanzo waliwaambia walimu wakuu wapeleke majina ya walimu watakaokuwa makarani wa sensa, kipindi hicho hawakujua kwamba kuna wahitimu wasio na ajira? Hiyo ajira ya wiki moja itawasaidia nini, wakubali tu kwamba wanawakomoa waalimu kwa sababu ya mgomo.
 
Anajibu kwa dharau sana wakati maswali yale ni mawazo yetu na tunahitaji majibu ya kuridhisha kwa nini anajibu kama si ya lazima?na kwa jeuri?nimemchukia sana liwalo na liwe tangu alipomsulubu uli!
 
huyo binti aliyeuliza swali bungeni kabla ya leticia kuuliza swali la nyongeza ni nani (amevaa hijabu)?
 
SWALI LA KWANZA: UWEKEZAJI HOLELA
JIBU: Kuna wawekezaji wazuri na wabaya.

Swali la pili toka kwa Mohamed Nyaa, linahusu Tanzania kujitolea katika ulinzi wa amani, ila Tanzania tunanyimwa fungu la malipo.

Jibu: Ni kweli, lakini sasa tutatumia fursa hizo vizuri amemshukuru Migiro kusaidia na Wamarekani wamejitolea kutufunza.
Hajui nini kifanyike kwa wawekezaji wabaya? Sisi ni maskini hizo gharama za kujitolea zisizo na tija za nini kwani lazima?

Swali la 3. Toka kwa Mchemba, ameuliza kuhusu sheria ya manunuzi ndio chanzo cha ufisadi na huduma za kiwango cha chini na kupaisha bei, amelink na direct sourcing kuokoa zaidi mapato.
Jibu: Inategemea uaminifu wa wahusika, watendaji sio waaminifu wana collude na suppliers kupaisha bei ili kupata cha juu!.
Kwani hakuna utaratibu unaowatia hatianai hao watendaji au na yeye ni mmoja wao?

La nyongeza, watendaji hao wa makosa ya manunuzi tuwaingize kwenye kosa la wahujuu uchumi.
Jibu. Ni wazo zuri, ila inategemea uwezo wa kuwabaini kutoka na usiri uliopo.

Swali la 4. Uwezo wa serikali yetu kukabiliana na maafa toka kwa Rajab Mbaruku.
Jibu: Usimamizi wa kuzuia majanga hatuko makini!. Pande zote mbili zitazingatia viwango, lazima tukubali kulikuwa na laxity,
Hachia ngazi kazi imekushinda!

la nyongeza, utachukua hatua gani kwa uzembe wa SUMATRA,

jibu, : yaliyo[ita si ndwele, tunasubirio taarifa ya uchunguzi tutachukua hatua stahiki.
Chunguzi zipo nyingi kuhusu ajali mbali mbali hatua zipi zimechukuliwa kudhibiti ajali nyingine?

Sali la 5: Tundu Lissu.
Kwanini watendaji waandamizi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa kuwa wabunge,
Jibu: Sina uhakika na hili, mwanasheria mkuu yupo atalishughulikia.
Ina maana yeye hawajuia wakuu wa mikoa na wilaya mpaka mwanasheria mkuu?.

nilishapendekeza kipindi cha maswali na majibu kifutwe na kisiwepo kabisa...sababu kuu ni moja tu..majibu ya wazri mkuu hayaridhishi hata kidogo
Ni kweli mkuu wanapoteza muda bure maana hana majibu anachofanya ni kuongea maneno kuhusu swali husika lakini sio majibu kabisaaa!. Ni mchezo wa kitoto unaofanyika bungeni. UPUUZI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
 
Huo nao ni udhaifu. Ina maana hajui kuwa Stella Manyanya ni mtendaji wa serikali (mkuu wa Mkoa) na wakati huohuo ni Mbunge?
Kila anapouliza swali Tundu Lisu, hakuna anaeleza kumjibu, wote wanakimbilia kwa Kishoka Werema.
Hovyo kabisa hawa!
 
Sali la 5: Tundu Lissu.
Kwanini watendaji waandamizi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa kuwa wabunge,
Jibu: Sina uhakika na hili, mwanasheria mkuu yupo atalishughulikia.

Pinda kwa jibu hili ni kilaza!
 
Liwalo na Liwe hivi alishawahi kufanya maamuzi yapi magumu toka awa PM.
 
Pasco ;naomba umuulize makinda maazimio ya bunge kuhusu jairo,richmond na muongozo wa tl kuwaita majaji hawajui kusoma hukumu imeishia wapi ninataka kujua
 
Sali la 5: Tundu Lissu.
Kwanini watendaji waandamizi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa kuwa wabunge,
Jibu: Sina uhakika na hili, mwanasheria mkuu yupo atalishughulikia.

kwa jibu hili la Pinda kweli pinda na yeye ni kilaza
 
Leo PM atakuwa alipata supu ya twiga manake majibu mepes kama ya mtoto. Kiufupi kachemka,kipengele cha dini ni muhim sana na anajua ila anazuga,akumbuke maeneo ya mazishi na nyumba za ibada vinaweza kutengewa eneo vizur endapo idadi kamili itajulikana.
 
Hili neno changamoto nalichukia sana
Swali la 6 toka kwa Marriam Msabaha kuhusu watoto wa mitaani.
Jibu: Watoto wa mitaani ni tatizo la jamii na ni changamoto, jitihada zipo ila idadi inaongezeka kila kukicha, jitihada zinaendelea.
 
majibu ya Pida hayaridhishi ni kweli but uasikia ccm ( wabunge) wakimpigia makofi mwanzo wa hii seshenalikua akijibu but baada ya kuwa anatoa majibu ya kebehi kwa wapinzani na ccm wanampigia meza imekua ndo stail yake ya kujibu maswali.
 
System yote dhaifu tu.
Tusitegemee maajabu toka kwenye utawala huu.
 
Swali la 7: Kutoka kwa Susan lymo, kwanini serikali imeondoa kipengele cha dini kwenye hojaji za sensa?.
Jibu: Hatupangi maendeleo kwa kuzingatia vigezo vya dini, kiserikali tumeona halina tija ili kuepuka kigogoro ya nani wengi.

Hili si swali jepesi hata kidogo hili ni swali gumu na la msingi kabisa kwani limezua mtafaruku mkubwa,

Binafsi sioni sababu ya kuzuia kipengele hicho kwani japo sensa ni ya serikali, lakini taasisi za dini pia zinapata mwanya wa kujua wingi wao na kuweza kuwahudumia kikamilifu waumini wao

Hili ni swali gumu na jibu jepesiiii
 
Mwenye Hotuba ya Upinzani inayosomwa sasa hivi Bungeni ya ufugaji naomba aiweke hapa
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom