Kutoka Bungeni:CUF wajitoa Kambi ya Upinzani kwa mnadhimu kukosa sifa

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
298
Mbunge wa CUF leo kaonesha wazi kuwa ni damu damu, kwani kaomba mwongozo wa mkiti wa kuwa wao na CDM hawako kambi moja .

Nawsilisha.
 
Mbunge wa CUF Mheshimiwa Kombo amesema CUF hawapo kambi ya Upinzani kwani Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Ndugu Tundu Lissu hana Nidhamu na wao CUF wanaona hawawezi kuongozwa na Mtu asiye na Nidhamu,kwani anatolewa nje kwa kukosa Nidhamu!
 
Mbunge wa CUF Mheshimiwa Kombo amesema CUF hawapo kambi ya Upinzani kwani Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Ndugu Tundu Lissu hana Nidhamu na wao CUF wanaona hawawezi kuongozwa na Mtu asiye na Nidhamu,kwani anatolewa nje kwa kukosa Nidhamu!
<br />
<br />
mbona wao ni sehemu ya serikali ! Hao ni ccm B, ni wajinga tu. Ndo maana Nape kamtukana Maalim Seif, hata kumkemea kwa dhati wameshindwa, Ni wapuuzi tu.
 
Mbunge wa CUF Mheshimiwa Kombo amesema CUF hawapo kambi ya Upinzani kwani Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Ndugu Tundu Lissu hana Nidhamu na wao CUF wanaona hawawezi kuongozwa na Mtu asiye na Nidhamu,kwani anatolewa nje kwa kukosa Nidhamu!

sishangai kabisa! cuf ni chama cha wapemba na wako kwa ajili ya interest za wa Pemba,kwa hiyo sawa tu alivyo sema maana wao tayari wakopamoja na ccm visiwani wakisimamia interest za nchi yao.tunasubiri siku warudi kwao basi
 
Wanatokaje kwenye kambi ya upinzani wakati wao waliingia mkataba na chama tawala na wanatambulika wako kwenye kambi ya chama tawala?
 
Huwezi ukasema umejitoa kwenye kitu ambacho hukuwepo.
Ni sawa na kusikia nchi kama Botswana ikidai imejitoa JUMUIA YA AFRIKA MASHSRIKI.
 
Wanajipendekeza wakati wenzao Magamba washawaona majuha na wanapita mitaana wakiwananga, hao CUF lini watakuwa na akili wakazinduka? Haowani katibu mkuu wao anavyosimangwa wao bado wanang'ang'ania tu hiyo ndoa yao ya mkeka.
 
Kwani wamepeana talaka lini hawa wote wanajifunika shuka ya kijani hawa.
 
Nmefurahi sana kuona CUF wanadhalilika kuitetea ndoa yao ya mkeka,CDM inajitosheleza kila idara wala hatuhitaji mkopo wa wapinzani walioolewa
 
hao Wapemba wana nini cha kuongea kwa watanganyika? wao wanafiki tuuu. kura zenyewe 1500 halafu mtu unajiita mbunge huku ukipewa haki zote za wabunge. wao wasubiri posho warudi kwao Pemba siku zote hoja zao PUMBA!
 
Haya ndio matatizo ya vyama vya Upinzani nchini... Tatizo kubwa ni Wanasiasa Uchwara kama huyu..
Haya mambo huwezi kuyakuta CCM hata kidogo, ila vyama vya Upinzani tu siku zote sababu ya kutofautiana ni watu na maamuzi yao binafsi..

Jambo moja muhimu sana nawaomba wanasiasa uchwara walifahamu. Kwanza ni heshima kwa viongozi wako hata kama hukubaliani nao kwa maana kwamba ndani ya CCM toka Nyerere huwezi kukuta migogoro ya kiuongozi ndani ya chama. Nyerere alikuwa na sekretariet yake na akabadilisha mara kibao, akaja Mweinyi na yake akaja Mkapa na yake na leo hii JK anayo yake baadaye kubadilisha hivi majuzi tu...


Pamoja na mabadiliko yote haya haijatokea hata siku moja viongozi wake kudharauliwa na wanachama ama viongozi hata kama hawapendwi. Tulikuwa na Rostam kama mweka hazina wa chama na alikuwa na maadui lakini haikutokea mtu kuodnoka chama wala kubishana na uongozi kwa sababu kachaguliwa Rostam..Na hata wakati wa misukosuko ya Rostam hakuna kiongozi wala mwanachama aliyejitoa chama kwa sababu Rostam ni mweka fedha isipokuwa walitafuta njia za kumwondoa kuilaini na wakaweka kundi jingine.. majuzi tu wamebadilisha tena hakuna kinyongo maanake nafasi za chama ktk uongozi ngazi za juu hazifiki 100 na wanachama ni zaidi ya 2mil.. utaweza vipi kuwadhirisha wote!

Lakini tazama vyama vya Upinzani..kila mtu anataka kuwa kiongozi makao makuu ya chama, kila mtu anataka kuwa mwenyekiti, katibu au mweka hazina..Usipofanikiwa kuna mchawi wako na unaunda uadui..Kuna watu wanahama CDM kwa sababu ya Mbowe au Dr.Slaa au Zitto sijui Lema kafanya hivi ama vile. Nenda CUF, NCCR, TLP kote kumejaa wanasiasa ambao kwao chama ni MTU, ukiwa na ugonvi na Mbowe basi chama hicho hakikufai unaondoka kwenda NCCR au CUF, vivyo hivyo toka CUF na NCCR ili mradi maamuzi yako yanatokana na MTU sio SERA wala hoja..

Haya tazama mbunge kama huyu, ni kiongozi wa chama na anathubutu kusema CUF inajiondoa ktk kambi ya Upinzani kwa sababu Tundu Lissu hana nidhamu! kweli hii inaingia akilini kukiweka chama ktk nafasi mbaya ya kutetea maslahi ya wananchi..Ukijiondoa ktk Upinzani unajinyima fursa ya uwakilishi ktk maswala ambayo ni muhimu zaidi kwa wananchi halafu basi kinachochekesha zaidi sii ajabu huyu mbunge anakubaliana na maudhui ya hoja isipokuwa kitendo cha kutolewa Lissu..CUF kuingia kambi ya Upinzani ni kazi iliyofanywa kwa nguvu kubwa sana pamoja na kwamba haikuwa halali. Wamewezeshwa kupata fursa hiyo leo unaitupa kwa sababu ya Lissu? huu si ukichaa jamani?
Wanasiasa wa Bongo kweli ni kichwa cha mwendawazimu..
 
Nafikiri wabunge wa CUF uwezo wao ni mdogo kiasi cha kutokutambua alama za nyakati.
Hata naa hivyo lini walijiunga na CDM.
 
mwananchi

Pamoja na kusindikizwa na askari wa Bunge, baadhi ya wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi walitoka nje wakimsindikiza Wenje.Walipofika nje ya ukumbi wa Bunge walianza kumlalamika kwamba, Mabumba ameshindwa kuongoza Bunge na kudai kuwa anaonyesha upendeleo wa wazi katika uendeshaji wa vikao vya chombo hicho.

Nje ya Ukumbi wa Bunge
Nje ya Ukumbi wa Bunge ilizuka tafrani nyingine iliyosababisha Mbunge Filikunjombe (CCM), kunusurika kupokea kichapo kutoka kwa wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi baada ya kuingilia mazungumzo yao wakati wanajadili suala la Wenje kutimuliwa ukumbini.

"Tatizo lenu ninyi wabunge wa Chadema mnaishia kuwa wabishi kila wakati, jambo ambalo linawapotezea heshima kwa wananchi,'' alisema Filikunjombe na kuongeza: "Acheni mambo ya kitoto rudini ndani kuendelea na Bunge. Sio kila siku ninyi Chadema tu, watu wamewachoka.''

Kauli ya ilikuwa kama kumwaga petroli kwenye moto, kwani kundi la wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi ambao kwa wakati huo wakiongozwa na Moses Machali (Kasulu Mjini NCCR), walimvaa kama nyuki mbunge huyo na kuanza kurushiana maneno makali.

"We mjinga kweli, hapa sio wabunge wa Chadema hata sisi wa NCCR-Mageuzi tupo tunachojadili ni maslahi ya nchi sio ushabiki wa vyama, toka hapa mshamba wewe,'' alisema Machali.
ndoa ya magamba na mke wa pili nccr imevunjika siku nyingi sasa hivi bwana magamba amebaki na wake watatu akiwemo bi mkubwa kafu, tlop na udipii
 
Kusema ukweli wana CUF wanajipendekeza kwa CCM kutokana na NDOA waliofungia ZANZIBAR. nilifikiri angekataa kwa nguvu zake zote kitendo cha wabunge wapinzani kutolewa nje ili wasiendelee kupinga maovu ya MWANANDOA mwenzi. wasahau Maalim Seif alivyokuwa anabondwa na Polisi kule Pemba enzi hizo? wamesahau walivyosusa nchi hadi kuishtaki kwa Donor Community kwa vitendo kama walivyofanyiwa wananchi wa Arusha. Jeshi la Polisi liliua wanachi Arusha kwa kuandamana kuipinga CCM. Leo hii CDM wakisema wanaambiwa hawana Nidhamu. Sawa tuu.
 
Back
Top Bottom