Kutoga masikio-Vijana wa kiume

Mila na desturi zinatofautiana.

Hapa Netherlands, wengi wa vijana waliotoboa masikio yote na tattoos ndio wale wanaoitwa macho man.

Na kutoboa masikio kwa watu wa Europe asili yao ni mapirate.
Na karibia asilimia ya kubwa ya pirate ni macho men.
 
Kasi ya vijana wadogo wa kiume, miaka 15 - 25 kutoga masikio imeogezeka sana sio mijini tu bali na vijijini sasa tabia hii imeshika kasi. Sababu ni nini? Nawaomba waache
vijana hao ni usela mavi! nilisikiaga kwamba katika nchi zilizo endelea 'mashoga wa kiume' ndio hufanya hivyo na ukiona earings basi unajua sio riziki huyo...
 
Hamjui mnachosema , hakuna ukweli wowote una husiana na utoboaji masikio mawili na ushoga .ushoga wa kutoboa sikio ni pale mtu anapo toboa sikio upande mmoja, sikumbuki ni wakushoto wa kulia , ilakila upande una maana yake nammoja kati ya huo ndio una husiano na ushoga.
 
Yes, Na hao M Pirates waliweza kusafiri na kukuta tamaduni zingine ambazo malijali wa kiume ndio wame toboa masikio na kujichora na wao ndio wakajichora.

Wengi hapa mnaongea kwa ushabiki tuu bila kufukiri ,Kusuka na kutoga masikio ni tamaduni zetu za kiafrica, ila zilipo chukuliwa na wazungu na kuboreshwa basi , zinaonekana ni mbaya na ngeni, again kutoboa masikio hakuna uhusiano na ushoga, mnaosema hivyo mna ropoka bila kufanya reesearch yoyote.

Kumbukeni tamaduni zimeingiliana sana kwa sasa, ina wezekana wewe bado uko kwenye miaka ya nyuma kwavile hujaenda na wakati ukadhani unavyo dhani, kwakila kipya unachokiona ambacho utakuta hakuna upya wowote na vilikuwepo siku zote, ila labda hukuwa na uwezo wa kujua kama vipo sababu hukua na uwezo wakuona au kujua wakati.
 
Mimi sijatoboa sikio wala sina plan hiyo.
Ila nimekuwa nikijiuliza kwa lengo la jua tu undani wa swala hili na muda wote nimeshinda kufikia mwafaka hata kwa nafisi yangu mwenyewe.

Mi nilijaribu kuagalia watu wa magharibi ambako ndiyo hasa (kwa mtazamo wangu) hizi pini na hereni(za chuma,almasi,dhahabu...) ndio zinakoanzia.

Niliangalia wale watu tunasema wamepinda au kubararuka kama vile wanamziki wa rock(sijui kama ni wote),watu wa hip hop(siyo wote)
nikasema ah! hawa ndio walivyo ila niliangalia watu wengine ninao waheshimu sana kama kina Michael Jordan na wengine mnao wafahamu, kidogo nikapata utata na kujiuliza inamaana hata M. Jordan naye kapinda?(sijui).

Utata unakuja zaidi pale ninapoangalia viongozi wa hizo nchi mfano USA labda na UK kwakweli mpaka sasa sijafanikiwa(mimi) kuwaona waliotoga.

Basi nikajikuta sipati jibu mpaka leo, pengine kutokana ma mada hii naweza nikatoka na jibu na nafsi yangu ikatulia.

Swali langu hasa ni kwanini hawa watu(wanaume) wanatoga?
Hivi kuna lengo gani hasa? au urembo tu? Lakini kwanini kina Bush,Obama na wengine waliopita hawakujiremba?
Wanojiremba hivyo wote wamepinda?

Mi sijui bana.
 
Naomba nikuulize swali dogo tu,umetoboa masikio na pua?

Kama ndiyo, Mungu atakuchukuliaje ukiwa katika hali hiyo wakati YEYE kakuumba katika hali ukamilifu?

Akikuuliza "mbona umetoboa sikio? ina maana nilivyokuumba hukuridhika?"
Utamjibuje?

Na swali hili akiwauliza waliotahiriwa? Kila kizazi kinakuja na mambo ya kuwakera wazazi wao. Kuanzia mavazi, muziki ili mradi kumnyima raha dingi. Kama alivyosema Lunanilo,dengilizi ilikuwa vazi la kihuni, michinjo iliwaudhi sana wazazi, bichkoma n.k. Usiangalie alichovaa bali angalia tabia yake. Vinginevyo unagombana na ukuta. Mzee Morgan Freeman, Spike Lee, Michael Jordan, 50 cent wote wametoga na hawa ndiyo role models wa vijana wetu. Tuombee tu wapite katika umri huo mgumu wa u-tineja bila madhara yeyote na wao watakujashangaa vioja vya watoto wao!

Kibunango yuko sahihi kabisa. Huku kukemea uvaaji ni morals tulizoiga kutoka kwa hao waliotutawala na kutuletea dini. Wanaume kwa wanawake walijiremba, walitembea nusu uchi bila ya matatizo yeyote kabla ya kuja hao wageni. Leo tunapandisha kwa sababu kijana katoga sikio!

Amandla......
 
Well said, I,m also wonder why is very common these days for Tanzanian women to wear trousers, and some years ago was a big taboo.

First lady where are you?
 
Back
Top Bottom