Kutoga masikio-Vijana wa kiume

Sijakufahamu...!

Wacheni kubeza asili zenu, kutoboa masikio, pua na ghasia zingine za kujiremba zipo tele kwenye tamaduni zetu. Leo hii eti imekuwa kero? Au ni kwa sababu badala ya kutia betri chakavu ama vipande vya miti kwenye masikio na badala yake kuweka almasi na dhahabu?

Rudi nyuma na kuwatizama Wamasai wa kiume na hasa Morani, jinsi wanavyojitahidi kuweka vipande vya miti na betri kubwa kwenye masikio yao, tizama Wagogo na nyunda zao, waangalie Wamakonde na chanja zao.. Watidinga na vimini vya miti...

Haya yote sio kero kwenu, kero ni tu pale sikio linapokuwa na dhahabu ama almasi...? Wacheni ulofa wa mawazo. Kwangu, hii si kero bali ni ufinyu tu wa kutazama wapi tumetoka na wapi tunaelekea...

Jamaa zangu wa kiume wanaweka mpaka wanja, na wanaita ni suna, hamjaliona hilo?
Sasa hao wanaofanya hivyo nao ni wamasai...???? wamakonde...??? Kwa mmasai kufanya hivyo hatushangai kwa vile ni mila yake. HATA HIVYO TUPO MBIONI KUONDOA MILA POTOFU

Umeshajiuliza kwa nini jeshi la polisi TZ halipokei wenye tatoo..???
 
Hahaha! Mpwa bana. Wanaanzaga na masikio, then wanasuka nywele, kisha suruali inashushwa mpaka makalioni. Baada ya hapo wananunua line ya TiGo!

Kemeeni sana tabia hiyo. Madhara tayari yameanza kuchanua. Jeshini vijana hawa wanalalamikiwa kugawa uroda kwa Ma-colone na Ma-brigedia. Ushahidi, kuna ambaye alienda kwenye peace keeping mission LEBANON, akiwa huko aligeuka kuwa asusa ya waarabu, amerudishwa na amefukuzwa kazi. kabla ya kufukuzwa kazi, mke ndiye alikuwa wa kwanza kuondoka.

Tabia hii chafu, haiishii kuvaa heleni, kuvalia suruali matakoni, kutoga vitovu na masikio, bali wanaenda nayo mpaka kwenye ajira zao baada ya masomo. tusipoangalia tutakuwa na Wabunge, mawaziri, maaskofu, mashekh, wakurugenzi na Rais, Makamu wa Rais, magenerali, ma-commissioners mashoga. Tukemee hili kwa nguvu zote
 
Wacheni kubeza asili zenu, kutoboa masikio, pua na ghasia zingine za kujiremba zipo tele kwenye tamaduni zetu. Leo hii eti imekuwa kero? Au ni kwa sababu badala ya kutia betri chakavu ama vipande vya miti kwenye masikio na badala yake kuweka almasi na dhahabu?
Kibunango leo vipi hoja zimepitia upande gani?
Tamaduni gani hizo unazozizungumzia hasa? Mimi binafsi hizo tamaduni sizijui na sijui wewe umezipata kwenye nchi gani? Hapa sijakupata labda ufafanue hizo mila ni zipi na uyataje hayo makabila ambayo wanaume wanatoga masikioa na pua. Vinginevyo weekend imeshaanza kwa upande wako

Rudi nyuma na kuwatizama Wamasai wa kiume na hasa Morani, jinsi wanavyojitahidi kuweka vipande vya miti na betri kubwa kwenye masikio yao, tizama Wagogo na nyunda zao, waangalie Wamakonde na chanja zao.. Watidinga na vimini vya miti...
Hamna sababu ya kurudi nyuma hapa Kibunango, wewe unawazungumzia Wamaasai wa wapi? Wamasai staili ya kutoboa masikio ni tofauti kabisa na tunayoisemea hapa. Kama hujui leo ukitoka kwenye kazi zako tafuta walipo Wamaasai wa Asili uwaangalie, husiwangalie waliovaa mavazi ya Kimaasai hapana ila Wamasai, kwa sababu kuna tofauti ya Wamaasai na wanaovaa mavazi ya Kimaasai ambao nahisi wewe ndio unawafahamu
Haya yote sio kero kwenu, kero ni tu pale sikio linapokuwa na dhahabu ama almasi...? Wacheni ulofa wa mawazo. Kwangu, hii si kero bali ni ufinyu tu wa kutazama wapi tumetoka na wapi tunaelekea...
Kumbe kuvaa hereni ya dhahabu au almasi kwako ndio kero. Aisee waambieni Kibunango amesema wakitoboa wavae pini za kushonea nguo ngo. Hivi umewahi kuwauliza hao vijana kwanini wanatoga masikio au pua? Au umeandika hivi tu? Sasa mimi nilioongea nao wala sio mila zao wala sio kwamba wanavaa hereni za almasi wala dhahabu ndio maana imekuwa kero ila ni kwasababu hawajui hata sababu za kutoboa zaidi ya kuwaona akina Lil Bow Bow wametoboa ndio nao wakatoboa. Chunguza kwanza kabla ya kutuambia tuna ulofa wa mawazo otherwise inawezekana umejisemea mwenyewe Mkuu

Jamaa zangu wa kiume wanaweka mpaka wanja, na wanaita ni suna, hamjaliona hilo?
Bro una saluni nini ya kufanyia haya mambo? Mbona unapigia sana debe au ndio mambo ya kura na kuanza kutambua umuhimu wa vijana. Hahahahaha
 
Sipo:
Pengine sijajua maana ya hii kero! Kwangu mimi sioni kama ni kero kwa vijana hao kujiremba kwa hereni za dhahabu ama almasi. Kwani haya yamekuwepo na yapo na yanaendelea kufanywa na baadhi ya jamii zetu hapa nchini, ingawa kwa viwango tofauti.

Kama kuzungumzia kero, ingefaa zaidi kuzungumzia tabia mbaya kama vile kufakamia machungwa na kutupa maganda yake barabarani, tabia za uchafu miongoni mwetu na mambo mbalimbali ambayo yanakwamisha maendeleo yetu.

Hili la kuvaa heleni sio kero kabisa, kwani lipo kwa miaka chungu nzima, sana sana vijana wa sasa badala ya heleni za betri na vipande vya miti.. wao wanatia heleni za dhahabu. Hii inawasaidia kutokuwa na masikio marefu mpaka kwenye mabega.

Tujaribu kuzungumzia kero zinazo zorotesha maendeleo yetu, badala ya kuangalia umaridadi wa mtu.
 
Kibunango
Mimi nahisi kila mtu ana mtazamo wake kwenye nini maana ya kero na kero ni nini kwa maana ya yeye anavyoitazama.
Labda mimi nikwambie kwanini naiona hii kuwa kero. Ni kero kwa sababu vijana wadogo pasipo kujali mila na tamaduni zao wanatoga masikio na wanafanya hivi kwa kutokujua wanachofanya baadae kuja kujuta. Nikupe mfano kuna kijana mmoja wa Arusha (namfahamu siongei from nowhere) kakosa nafasi ya kuingia jeshini kwa kuwa alikutwa kuwa ametoga sikio moja.
Halafu wewe unachozungumzia kuwa mila toka zamani sio kweli (kwa upande wangu, labda na wengine) sababu kubwa ni kwamba vijana wa leo wanatoboa sikio moja. Kwenye hizo mila mfano Wamaasai wanatoboa masikio yote mawili. Hata hayo makabila mengine hawatoboi sikio moja ila masikio mawili halafu pia hawatoboi videvu, kujichora tattoos, kuvaa kata ***** na mengine yanayofanana na hayo.
Ni kwero pia kwa sababu sio makabila yote ambayo ni utamaduni wao ila vijana wa siku hizi wote pasipo kujali utamaduni wao wanatoboa masikio, videvu, vitovu na sehemu nyingine. Sasa mfano kama vile Wambulu, Wameru, Wachaga, Wanyakyusa na mengine mengi sio tabia yao kutoboa hizo sehemu nilizohahinisha hapo kabla.
Nway sitaki kukushwaishi uikubali hii kama kero kwa upande wako lakini ninachokuomba husiwashauri vijana kutoga hizo sehemu ni kero na haifai Mzee Kibunango
 
Jamani wakati ni ukuta ukipigana nao utaumia wewe, amini usiamini mwaka 1965 ilikuwa kuvaa suruali za jeans, ni uhuni. Nakumbuka bibi yangu alikasirika sana kumuona baba yangu mdogo kavaa suruali ya jeans na t-Shirt ya kubana, ilikuwa scandal kubwa watu wazima walinonong'ona utadhania ameua, bibi aliwaambia watoto wake wote wamuonye mdogo wao, ilikuwa kasheshe kubwa ilibidi baba mdogo aiache hiyo suruali yake. Sikubaliani na vijana kutoboa masikio, kusuka nywele kupakaa madawa ya kulainisha nywele na kadhalika, lakini ndiyo hali ya maisha. Sisi wenyewe enzi za kuvaa laizoni na mabugaluu tuliipata, kwa hiyo ni zamu yetu kuwa baba zetu. ( we have become our parents)
 
Sijakufahamu...!

Wacheni kubeza asili zenu, kutoboa masikio, pua na ghasia zingine za kujiremba zipo tele kwenye tamaduni zetu. Leo hii eti imekuwa kero? Au ni kwa sababu badala ya kutia betri chakavu ama vipande vya miti kwenye masikio na badala yake kuweka almasi na dhahabu?

Rudi nyuma na kuwatizama Wamasai wa kiume na hasa Morani, jinsi wanavyojitahidi kuweka vipande vya miti na betri kubwa kwenye masikio yao, tizama Wagogo na nyunda zao, waangalie Wamakonde na chanja zao.. Watidinga na vimini vya miti...

Haya yote sio kero kwenu, kero ni tu pale sikio linapokuwa na dhahabu ama almasi...? Wacheni ulofa wa mawazo. Kwangu, hii si kero bali ni ufinyu tu wa kutazama wapi tumetoka na wapi tunaelekea...

Jamaa zangu wa kiume wanaweka mpaka wanja, na wanaita ni suna, hamjaliona hilo?

Naomba nikuulize swali dogo tu,umetoboa masikio na pua?

Kama ndiyo, Mungu atakuchukuliaje ukiwa katika hali hiyo wakati YEYE kakuumba katika hali ukamilifu?

Akikuuliza "mbona umetoboa sikio? ina maana nilivyokuumba hukuridhika?"
Utamjibuje?
 
Kasi ya vijana wadogo wa kiume, miaka 15 - 25 kutoga masikio imeogezeka sana sio mijini tu bali na vijijini sasa tabia hii imeshika kasi. Sababu ni nini? Nawaomba waache
Wakuu mbona naona kama ndugu Sipo hajajibiwa swali lake?..sababu ni nini...? Naona kama kila mtu amepandisha jazba na kutoa lawama na hatimaye kwenda nje ya mada...na kusahau "JF: Hoja hujibiwa kwa hoja"

Yamkini hao vijana watoga masikio hawatembelei huku JF (na kama wapo..shame on them!) ila tunakutana nao mitaani na majumbani.

Mimi kwa mtazamo wangu,kumjibu ndugu Sipo, sababu ni malezi duni ya maisha ya awali ya hawa vijana/watoto. Kosa linakua kumuachia mtoto/kijana achague mwenyewe nini ''cha maana'' kwenye maisha yake na nini "cha madhara" kwenye maisha yake.. Tofauti hiyo ndio hufanya vijana wanapopita kwenye kipindi cha kubalehe (ambao wengi ndio hilo group) kutoka na tabia tofauti. Watakaochagua kipi cha maana vizuri ndio watakua vijana bora/wastaarabu..watakaochagua vinginevyo ndo watakua kama hizo lawama zilizotolewa hapo juu.

Nawasilisha.
 
Kasi ya vijana wadogo wa kiume, miaka 15 - 25 kutoga masikio imeogezeka sana sio mijini tu bali na vijijini sasa tabia hii imeshika kasi. Sababu ni nini? Nawaomba waache
inaonyesha kuwa hiyo ni tabia ya kuiga toka nje ya nchi wameharibika vijana wa siku hizi inafika mpaka wanavuta unga wateja sasa waswahili husema mtoto ukimleavyo ndivyo akuavyo sasa wakulaumiwa ni Wazazi wa watoto hao wanaotoga masikio hawakuwalea vizuri watoto wa kulaumiwa ni Wazazi wao sio hao watoto upo an mimi mkuu sipo?
 
haipendezi na haina mvuto kwa vijana wa kiume kutoboa masikio na pua kwanza si maadali ingawa wao wanaona kama wanaenda na fashion
 
Kasi ya vijana wadogo wa kiume, miaka 15 - 25 kutoga masikio imeogezeka sana sio mijini tu bali na vijijini sasa tabia hii imeshika kasi. Sababu ni nini? Nawaomba waache

....... NA mUYAONAPO HAYO MJUE KIAMA KIMEWADIA...GET READY FOR THAT MAANA HAMJUI SIKU WALA SAA MWANA WA ADAM ATAPO RUDI KUCHUKUA WATU WAKE.
 
Tatizo la uigaji,Wakiona wamarekani weusi kwenye tv na muvi na lifestyle yao basi wanataka wafanane nao wakidhani ndio ujanja.
 
inasikitisha sana, sijui tunakwenda wapi yani sijui tunawasaidia hawa wadogo zetu inabidi tutafute mbinu jamani ili waelimike coz tuna washangaa na wanazidi kuongezeka then mwisho wa siku wanakuwa wengi na inakuwa tabu kuwa toa walipo....anyway there is alot to be done.. about hereni, tigo and many more..
cheerz!!!
 
Kasi ya vijana wadogo wa kiume, miaka 15 - 25 kutoga masikio imeogezeka sana sio mijini tu bali na vijijini sasa tabia hii imeshika kasi. Sababu ni nini? Nawaomba waache

Kumbuka enzi ya platform shoe bellbottom,slimfit shirt na afrohair style/hili la kutoga sikio ni fad pia,litapita tu na kusahaulika.
 
Back
Top Bottom