Kutembea na wake za watu: Nani ana MAKOSA?

Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,272
1,034
!Kuna wanaume wanayo taabia ya KUTEMBEA NA WAKE ZA WATU.

Kuna kasumba moja imetawala vichwa vya tulio wengi:

Sasa uchunguzi umedhihirisha wazi kwamba MWANAUME anae chukua mke wa mtu ndiye huonekana MKOSAJI SANA,na pengine hunyooshewa sana mikono mtaani!

Sasa mimi nashindwa kuelewa,kwanini yule mwanamke aliyechukuliwa ASINYOOSHEWE KIDOLE?au asionekane mkosaji kwa kiwango kile kile?ukizingatia walikubaliana?

Hii dhana inaanzia wapi jamani?
 
Wote ni wazinifu, hakuna dhambi kubwa ipitayo nyingine dhambi ni dhambi tu

Na huku tumwombe mod afanye transfer??hongera at least tunajibiana then unatoa ushauri
 
Ndugu mfano humu online unaweza kukuta mama mia ni mke wa mtu si ndio mnaongea pm anasema yuko single kumbe ukweli ni mke wa mtu -- siku mnatembea wote wewe hujui yeye anakulaghai na hata ukishajua ni mke wa mtu ni ngumu kutoka katika kifungo hicho kutokana na maslahi unayoyapata pale kwa mama mia labda pesa na mambo mengine mengi

tunapokuwa na wake zetu lazima tuwe na dira ya maisha yetu lazima tuwe tunaongea mara kwa mara tuwe marafiki na tushirikiane zaidi ndani ya nyumba katika mambo yetu kuliko wakati wowote katika maisha yetu ,halafu twende na wakati tujue dunia na watu wanabadilika lazima tukubali mabadiliko hayo

kwa njia hiyo mwanaume hawezi kutoka nje kila mara utakuwa una miss mwenzako
 
wote wakosaji tu, labda mkaka awe hajaoa then kachukua mke wa m2, but wote wakiwa na ndoa ni wote wakosaji, tena sana sana mwanamke maana akifumaniwa na kwao kunamuhusu lakini wakina baba tukiwafumania ni stori ndefu unashushiwa hapo unalainika, so mwanamke ni bora uwe makini zaidi.
 
Wanaume badili tabia. Kama umeshafanya uchunguzi, wanawake hatutoki nje ya ndoa zetu kama hakuna matatizo. Ukiona mwanamke anatoka ujue kwake siyo kuzuri au hakuna maelewano kati yake na mume wake. Tabia ni mbaya sana hata kwa mwanamke kufanya hivyo, ila wanaume tuwe makini nyie ndo vichwa vya familia inabidi muweke mambo sawa na maelewwano mazuri kati ya mke na mume.

Mwanaume hana athari kubwa akaifumaniwa kama mwanaume though yote ni kufumaniwa. Wanawake tuwe makini sana, kukomoana na waume zetu hatufiki popote.
 
Kuna wanaume wanayo taabia ya KUTEMBEA NA WAKE ZA WATU.

Kuna kasumba moja imetawala vichwa vya tulio wengi:

Sasa uchunguzi umedhihirisha wazi kwamba MWANAUME anae chukua mke wa mtu ndiye huonekana MKOSAJI SANA,na pengine hunyooshewa sana mikono mtaani!

Sasa mimi nashindwa kuelewa,kwanini yule mwanamke aliyechukuliwa ASINYOOSHEWE KIDOLE?au asionekane mkosaji kwa kiwango kile kile?ukizingatia walikubaliana?

Hii dhana inaanzia wapi jamani?

Nitazungumzia kwa mwanaume aliyeoa mnwenye tabia ya kuchukua wake za watu.

Kwa wanaume, kitendo cha mkewe kuchukuliwa na mwanaume mwingine kinauma sana na kwa wengi hakivumiliki (most likely akatoa talaka, kama ni 'red handed'!). Ni kwa mantiki hii basi mwanaume anategemewa ajue kwamba kutembea na mke wa mwenzake ni kitendo kibaya, kinaumiza na cha hatari. Nadhani hiyo dhana ndio inaanzia hapa.
 
Hii ndo dunia ilivyofikia, kupanuka kwa viwango vya technologia ya mawasiliano kumesababisha haya yote. What i believe ni kuwa nature ita-balance haya yote. Mi sioni tabu sana kwa kuwa kuna UKIMWI na mengine yatabalance haya mabadiliko. Enzi za mwalimu haya hayakuwepo lakini sasa yapo inabidi tu-cope na hali halisi.
 
kuna msemo waungwana walinena '.........MKE WA MTU NI SUMU..........'

kwanini isiwe mume wa mtu NI SUMU?

SIELEWI ELEWI HAPA.kwa kauli hiyo hapo juu,inaonyesha katika uzinzi huu,KIBINADAMU mwanamke ndo mwenye makosa,,,,,,,,,,,...........au?
 
Wanaume badili tabia. Kama umeshafanya uchunguzi, wanawake hatutoki nje ya ndoa zetu kama hakuna matatizo. Ukiona mwanamke anatoka ujue kwake siyo kuzuri au hakuna maelewano kati yake na mume wake. Tabia ni mbaya sana hata kwa mwanamke kufanya hivyo, ila wanaume tuwe makini nyie ndo vichwa vya familia inabidi muweke mambo sawa na maelewwano mazuri kati ya mke na mume.

Mwanaume hana athari kubwa akaifumaniwa kama mwanaume though yote ni kufumaniwa. Wanawake tuwe makini sana, kukomoana na waume zetu hatufiki popote.

Hahaha! Sasa wewe kama mme wako ana tabia chafu ndiyo uanze kujirusha na wanaume wa wenzako!?! Hapa wewe ndiyo utaonekana una tabia mbaya. Siku zote hakikisha unamridhisha mmeo asiweze kufikiria mambo ya nje kabisa. Mara nyingi wanawake mnasingizia wanaume kuwa ndiyo chanzo, ila ukweli chanzo ni nyie wenyewe. Tatizo kubwa wanawake wengi huwa hawafikirii kuwa mapenzi ni Art ambayo inakwenda na muda na kwa hiyo wanahitaji kubadilika with time. Ukishaoa mtu, basi anajisahau kabisa na hana habari hata kidogo kuwa mambo ni dynamic. Anakuwa yupo yupo kama hayupo vile!
 
Last edited:
kuna msemo waungwana walinena '.........MKE WA MTU NI SUMU..........'

kwanini isiwe mume wa mtu NI SUMU?

SIELEWI ELEWI HAPA.kwa kauli hiyo hapo juu,inaonyesha katika uzinzi huu,KIBINADAMU mwanamke ndo mwenye makosa,,,,,,,,,,,...........au?

Hapana. Nadhani huu ni msemo unayomuonya mwanaume kwamba ni hatari sana (kama 'sumu') kutembea na mke wa mtu. Mwenye mke akikukuta anaweza kukuuwa (kuna mauwaji mengi yanayoptokana na hili katika jamii yetu!).
 
Kumbuka pia jamii yetu kwa sehemu kubwa polygyny inakubalika. Wanawake zaidi ya mmoja 'kuolewa' au kutembea na mwanaume mmoja inakubalika zaidi kuliko vinginevyo. Hivyo, mume wa mtu 'hawezi' kuwa sumu!
 
Ukweli ni kuwa haya mambo ni magumu, yanaumiza hisia, ila wakati mwingine mke wa mtu anakuwa mchokozi mno, mpaka unaona njia sahihi ni kumridhisha, vivyo hivyo na mme wa mtu anachokoza chokoza mpaka basi tena!

Cha msingi hapa ni kuwa tukishaamua kujifunga kwa ndoa, tuwe na ujasiri wa kusimamia kifungo kicho kwa pande zote.
 
Hilo ndo suala la msingi. Labda kama unaongelea mume au mke mwengeshaji au msanii. Lakini kwa mtu aliyeoa/kuolewa na anajua utamu na uchungu wa kuwa na mwenzake kama wake peke yake hawezi tena kuwa na msamiati wa kuonja onja! Na kama ni kijana ambaye hajao basi ajue kuwa kamba ambavyo asingependa mtu yeyote amuonje mama yake (yaani mke wa baba yake) au dada yake basi aachane na wake au mabinti wa watu hadi akioa.
 
Kumbuka pia jamii yetu kwa sehemu kubwa polygyny inakubalika. Wanawake zaidi ya mmoja 'kuolewa' au kutembea na mwanaume mmoja inakubalika zaidi kuliko vinginevyo. Hivyo, mume wa mtu 'hawezi' kuwa sumu!

Kwa mila na tamaduni zetu mke ni mali ya mwanaume lakini mwanaume hawezi kuwa ni mali mwanamke. Suala la nani mwenye makosa inategemea na nani anayeuliza swali hili, katika muktadha huu muulizaji anaweza kuwa:
a/ Mume wa mke aliye megwa
b/ Mke wa mume aliye mega
c/ Mume aliyemega
d/ Mke aliyemegwa
Kwa mazingira a hapo juu mwenye makosa ni mke wake na mwanaume aliyemmega ila kosa kubwa sana ni mwanaume aliye mmega(kumbuka kuwa mke ni mali yake). Kwa mazingira b mwenye makosa ni mwanamke aliyemegwa tu.Kwa c&d hakuna mwenye makosa. Lakini cha muhimu ni mazingira ambayo kitendo hicho kimetokea ndiyo yatakayo amua ni nani mwenye makosa.
 
Wanaume badili tabia. Kama umeshafanya uchunguzi, wanawake hatutoki nje ya ndoa zetu kama hakuna matatizo. Ukiona mwanamke anatoka ujue kwake siyo kuzuri au hakuna maelewano kati yake na mume wake. Tabia ni mbaya sana hata kwa mwanamke kufanya hivyo, ila wanaume tuwe makini nyie ndo vichwa vya familia inabidi muweke mambo sawa na maelewwano mazuri kati ya mke na mume.

Mwanaume hana athari kubwa akaifumaniwa kama mwanaume though yote ni kufumaniwa. Wanawake tuwe makini sana, kukomoana na waume zetu hatufiki popote.

kichawa????????!!!!!!!!
 
Du sijui mwanadamu unaweza ukamtosheleza vipi? Bila ya muhusika kutumia akili na kupima kiasi alichopata hakuna mwengine atakaemridhisha.
Tukija kwenye suala la mwanamke na kuridhishwa tutaona kuwa mwanamke anaweza akaenda na dereva wake au houseboy (mwanaume pia kwa mama ntilie au house girl)sasa tuseme hatimiziwi mahitaji yake au la?
Maumbile yetu binaadamu ni viumbe visivyotosheka lakini tunasaidiwa na factors mbalimbali kulikabili hilo. Moja ya factors hizo ni kuwa na roho ya kuridhika na ulichonacho. Hata suala la mambo ya kindowa kwa mfano nani asiejuwa raha ya mwanamke biki ra, nani asiejua raha ya mati ti yaliyosimama, nani asiejuwa raha ya kijana shababi kwa kujiliwaza mwanamke mtu mzima lakini haya yote yatapatikana baada ya mtu kuvuka mipaka ya ubinaadamu. Huwezi kubadilisha watoto wa wenzako kila siku kwa kutafuta bikira na chuchu zilizosimama na wala bi mtu mzima ukaanza kufatia wajukuu zako.
Hapo ndipo inapokuja lile suala la nafsi kujitosheleza na unachokipata. Jifanye unaridhika na unakipenda hicho ulichonacho na kumbuka hata yule mwenye mke au mume mzuri kama si kuwa na moyo wa kujitosheleza basi ataacha hicho unachokiwania na kukifuata hicho chako unachoona kibaya.
 
Ushindi kwa Mwanaume aliyekamilika?

Si uwezo wa kumpeleka mwanamke bedroom...that is too easy and almost everyone can do that!

Ushindi na Ukamilifu kwa Mwanaume ni uwezo kuhakikisha anam_handle na kum_manage... in a way hafiki kitandani... itakapotokea kuwa now she is insisting...The really chalenge here is how do you handle that ...

Inactual sense Kuna ubingwa gani na ushindi gani kumplelekea bedroom? Its too easy..!

The question is hawa waanume kamili wamepotelea wapi siku hizi??

Mwanaume kamili kamwe hatambei na mke wa mtu... He can manage her without IT!
 
Hii ndo dunia ilivyofikia, kupanuka kwa viwango vya technologia ya mawasiliano kumesababisha haya yote. What i believe ni kuwa nature ita-balance haya yote. Mi sioni tabu sana kwa kuwa kuna UKIMWI na mengine yatabalance haya mabadiliko. Enzi za mwalimu haya hayakuwepo lakini sasa yapo inabidi tu-cope na hali halisi.

Aisee how old are you kijana? Uliza vibanda maalum vya biashara ya ngono wakati huo unaoita mtakatifu. Bora sasa unaenda barabarani na kuchaguwa taste yako lakini wakati huo jibibi unalolikuta kibandani ni hilo hilo labda bahati yako umkute mdogo wa hilo bibi aliyekuja kumtembelea na hivyo kuamuwa kumsaidia kazi. Tumetoka mbali kijana usione hivi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom