Kuteleza kwa wanasiasa na serikali katika mazishi ya kanumba

peter tumaini

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
573
94
Salaams Wanabodi,

Naamini watu wengi waliona Mazishi ya Kanumba kwa kushuhudia umati mkubwa wa watu ulioambatana na vurugu na hatimaye zoezi la wananchi kuaga mpendwa wao kukwama.Huku likiwa chini ya serikali na wanasiasa pamoja na kamati husika.Wengi wetu hatukupendezwa na kilichotokea.
Kwa mtu maarufu kama Kanumba shughuli hii ilitakiwa ifanyike pale DIAMOND JUBILEE na liwe zoezi la siku 2 na pia kungewekwa kiingilio cha kumuaga Lets say Tsh.3,000/ hizi pesa zingetumika kuanzisha Foundation yake ambayo ingetumika kukuza vipaji vya wasanii wachanga na hii ingekuwa kumbukumbu yake kwetu siku zote.

Hatungependa fujo kama hiyo kutokea na kusababisha vifo vya takribani Watz 6 hakuna tulichomuenzi zaidi ya kuongeza majonzi.

MY TAKE.Serikali badilikeni pamoja na wanasiasa kama hamuwezi waachieni watz wengine wafanye kuliko kutafuta cheap popularity kwenye misiba ya watu maarufu.

Nawasilisha.
 
Mawazo mazuri lakini hapo kwenye Blue, nina wasiwasi. Kwani Michango haiwezi kuchangwa hata baada ya kifo cha Kanumba. Mfano mzuri ni Mwalimu Nyerere Foundation japo Mwalimu hakuwa msanii kama Kanumba.
 
Sijawahi kusikia watu wakilipa fedha ili kutoa heshima za mwisho kwa marehemu! Hata ukiipamba kwa maneno mazuri jinsi gani mwisho wa siku utaonekana huna maana unayetaka kujitajirisha juu ya majonzi ya wengine! Marehemu Nyerere alikuwa maarufu kuliko huyo na nakuhakikishia hata kwa kiingilio cha Tshs 10,000/- watu wangeingia. Angalia hekima iliyotumika!
 
Duuu, hap Serikali inaingiaje? Ilikuwa ndo msimamizi wa mazishi?
 
jamani watanzania tunaenda wapi? kuaga mwili wa marehemu iwe sh.3000?
 
Duh! Kuuaga mwili marehemu kwa kiingilio, hiyo kali mkuu. Halafu taarifa za kufa watu 6 umezitoa wapi kiongozi?
 
6 people died? Tell me this is not true! Aaaah!

Mleta mada ni kweli serikali ilitumia fursa hiyo (kifo cha kanumba) kupata cheap popularity. Maamuzi mengi ikiwa ni pamoja na kutumia pesa za walipakodi kugharamia mazishi ya kanumba hayakuwa sahihi. Taratibu na kanuni hazipo in place kuamua the best way ya ku-handle mambo haya ni hivyo serikali inafanya maamuzi kwa kutumia hisia zaidi

Haya yote tunasema si labda kuna chuki juu ya kanumba, la hasha, bali tunaongea ili taratibu zilizo wazi ziwepo ili na wengine watakaokufa siku zijazo zifuatwe

Mungu atujalie rehema zake, na ailaze roho ya marehemu kanumba pahala pema peponi, AMEN
 
Back
Top Bottom