Kutakuwa na faida gani kurudisha JKT?

hadithi ya chemponda haiwezi kufuta maana na umuhimu wa JKT. Hata mtaani watu wanabakwa kila siku. Ukitaka vya urahisi utaliwa tu, iwe jeshini, uraiani hata misioni. kikubwa ni kzingatia yale yaliyokupeleka kule.
Mimi nilikua Makutupora, wasichana walikua wanagombea post ya kuhudumia rest house ya maafande wakati wanajua ni nini kinafanyika kule! Kisa chakula kizuri na soda!
 
JKT inahitajika kwa ajili ya kulinda uzalendo wa nchi yetu!!

Tatizo hapa ni namna ya kuliendesha kwa maslahi ya taifa, kwani naimani hiyo taasisi ikiundwa vizuri itasaidia sana kuweka mshikamano katika nchi yetu. Tatizo lingine ni kuiga iga kila kitu kutoka mataifa mengine!! " We must define our own rules and direction for the future of our country" siyo kung'ang'ana tu, eti kwa sababu marekani au jumuia ya ulaya imesema hivi basi tuache yetu mazuri na kufanya yanayowapendeza donors. Lazima tukubali US, EU na nchi zingine, hawata furahia kutuona tunajitegemea kwani utakuwa mwanzo wa wao kusambaratika.

Kuna nchi moja, iliwaaambia watalaamu wote kaeni chini mjadili nini kifanyike kwa ajili ya hiyo nchi! wanataaluma, na wasio wanataaluma walikaa wakadraft mipango yote A - Z, hadi leo vijana wa kiume (under 22yrs old) wanapiga jeshi miaka 2 then anarudi kuendelea na maisha yake, na kama akipenda kuajiriwa jeshini is up to him.

Kwa hiyo, mimi naona ni muundo tu wa mitaala (training program) inatakiwa kuwekwa vizuri, na kuweka uwazi katika inshu nzima ya namna ya training zinavyfanyika, faida yake pamoja na mambo ya kiusalama. Mfano: Kama ni kucheza mpira basi kikosi kitakachokuwa kinafanya hiyo shughuli kiweke maslahi ya taifa mbele siyo ujomba jomba, kuitana itana tu bila mpango.

Kitufe cha thanks sikioni mwana.
 
Kama JKT ingekuwa asasi inayoyojenga UZALENDO kama wengi wetu tunavyoelekea kuaminishwa, basi leo hii tusingekuwa na kansa hii ya UFISADI. Watawala wetu mafisadi walipitia ama walipikwa JKT hiyo ya enzi za Mwalimu! Bila kupoteza muda pitia ile orodha ya mafisadi ya Mwebeyanga uone ni nani hakupitia JKT. Kama wapo pengine ni mmoja au wawili waliokwepa. JKT kwa mujibu wa sheria is a waste!!!!
 
Ndugu yangu maisha ya JKT ni maisha tofauti kabisa na maisha tunayoishi kawaida majmbani mwetu. Huoni kuwa vijana watakuwa wakakamavu na kuwa tayari kwa maisha yao wenyewe na kuacha kuwa wazembe wa kushinda kutwa kucheza kamari tu???
Swala la vijana kwenda jeshi ni swala jema kwetu sisi watanzania na hasa kwa vizazi vijavyo. Sasa hivi huwezi kujilinganisha na kijana wa sasa kwani wewe unaweza ukawa mkakamavu zaidi ya huyu kijana unayemnyima kwenda jeshi.
Swala la kunyanyaswa jeshini ni swala la kawaida kabisa wala hata usiogope. Kijana kunyanyasika ni muhimu sana ili angalau apate ya kusimulia huko aendako na si kuwa legelege tu.
Kwa ushauri wangu wa bure jitahidi sana yasahau yaliokupata wewe na badala yake waruhusu waruhusu vijana kwenda jeshi.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Kwa hali ya sasa ambao uzalendo umetupwa mbali, watoto wetu wasio na uvumilivu, kutokuwa na kazi baada ya kutoka jeshini na ukimwi uliotapakaa kila mahali, kwa kweli naungana na waliotangulia kwamba kurudisha jeshi ni kukaribisha janga la kitaifa. Faida zake kwa sasa ni ndogo kuliko hasara. Kwa mzazi makini hawezi kuruhusu binti yake aende jkt. Ni vizuri serikali ilifikirie upya au iachie wale tu wanaotaka (volunteers)
 
hadithi ya chemponda haiwezi kufuta maana na umuhimu wa JKT. Hata mtaani watu wanabakwa kila siku. Ukitaka vya urahisi utaliwa tu, iwe jeshini, uraiani hata misioni. kikubwa ni kzingatia yale yaliyokupeleka kule.<br />
Mimi nilikua Makutupora, wasichana walikua wanagombea post ya kuhudumia rest house ya maafande wakati wanajua ni nini kinafanyika kule! Kisa chakula kizuri na soda!
<br />
<br />
Umesema vema. Hivi wanawake wanabakwa JKT tu? Vipo vyuo vya jwtz, polisi na magereza. Sijasikia wanawake wakisema wasiende huko.
Wanawake wanalalamika kwamba
Wanabakwa maofini na mabosi. Sijasikia hata mmoja akisema suluhisho ni kuacha kazi
Mimi nimepitia JKT wasichana walioamua kuzini na maafande waliendeleza uzinzi na lecturers na wanafunzi wenye uwezo kifedha. Hivyo kusema wasichana watabakwa, nakiona kama kitendo cha kuwazalilisha wanawake.
Tulikuwa na wasichana wazuri na wakakamavu sikusikia wala kuoana wakifanya uzinzi. Hivi msichana akihenyeshwa, suluhisho ni ngono? Huu utakuwa ni udhaifu mkubwa!!!
Tusitafute visingizio.
Ikumbukwe kwamba maafande hawako juu ya sheria. Ikithibitika afande kabaka atahukaukumiwa
Kama raia mwingine.
Wakuu nawasilisha.
nawa
 
[h=2]Tuesday, August 02, 2011[/h][h=3]Marudio - Miaka Baada ya tukio kaniomba Msamaha![/h]

(Pichani Ukaguzi wa Gwaride Mlale JKT Songea - Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)


Naona, kuna 'Anonymous' fulani kagusia hii swala ya yalionipata nikiwa jeshini JKT. Watu wengi wamenitumia e-mail kuulizia details. Nimeamua kuibandika tena. Ni posti ya kutoka April 2006. Lakini mjue enzi za JKT, wasichana wengi walinyanyaswa kijinsia, mimi nilikuwa na bahati maana nafahamu wasichana waliokuwa gang raped. Dada fulani, alimkubali afande, alivyomaliza kaita wenzake kwa kusema, "Njooni, Mboga hii hapa!" Yule dada hakuweza kutembea vizuri kama wmezi baada ya hapo!

*****************************************************************************

Nilipokuwa Jeshi ya Kujenga Taifa (JKT) karibu nibakwe na afande Fulani (jina nahifadhi). Lazima niseme kuwa katika kipindi hicho wanaume wengi waliona makambi ya JKT kama ‘buffet’ ya wasichana. Si maafande wa jeshi tu, bali hata viongozi wa serikali walikuwa wanapitia makambi ya JKT kula tani yao!

Mimi nilikuwa Masange JKT, Tabora. Wakati huo huyo jamaa alikuwa ni Kepiteni wa JKT. Nadhani alidhania kwa vile yeye ni kepiteni basi alikuwa na haki ya kutembea na yeyote aliyemtaka. Kwangu aligonga ukuta! Bila shaka alikuwa hajawahi ‘kunyimwa’ mpaka siku hiyo alipokutana na mimi.

Miaka baada ya tukio nikiwa nafanya kazi Daily News mara nyingi nilikuwa napishana naye Posta Mpya. Basi ananisemesha, na mimi namnunia halafu napita zangu kimya bila kumjibu kwa hasira. Siku moja kanisimamisha kaniambia, "Chemi, naomba msamaha, nisemahe tafadhali, kweli nilikukosea!” Aliongeza kuwa miaka mingi imepita hivyo sina sababu ya kuwa na hasira naye! Na mimi nilimjibu, “Mshenzi sana wewe!” nikaenda zangu.

Ikapita kama mwaka mwiingine. Jamaa anaendelea kunisalimia kila nikimpita njiani na mimi kwa uchungu bado nikashindwa kusema kitu. Basi nikafikiria alichoniambia Posta Mpya. Lakini niliona kama jambo hilo linamsumbua. Na nikasema kama Bwana Yesu aliweza kusamehe watu kwa madhambi yao kwa nini mimi nisimsamehe. Basi baada ya hapo ikiwa nikimwona na akinisalimia naitika na naendelea zangu na nikaona kidogo hata yeye alikuwa na raha.

Lakini bado najiuliza kama kitendo chake kilimsumbua miaka na miaka kama ilivyonisumbua mimi.Unauliza ilikuaje mpaka nikajikuta kwenye situation ya kubakwa. Au mnasema nilitaka mwenyewe. Ngoja niwaelezee ilivyokuwa.

Nilikuwa mhudumu Officer’s Mess, mpishi na msafishaji. Huyo jamaa alikuwa ni mgeni kutoka Makao Makuu ya JKT Dar es Salaam. Kwa kweli sikutaka kufanya kazi pale Mess lakini tulichaguliwa special na Matron, mimi kwa vile niijua kupika vyakula mbalimbali hasa za kizungu. Lakini uzuri wa hiyo kazi ni kuwa uanambulia mabaki ya vyakula (leftovers), na mara nyingine kulikuwa hakuna.

Basi huyo Afande alikaa kambini wiki kadhaa. Katika kumhudumia tukawa tunaongea na mimi nikawa namheshimu kama kaka vile. Wala sikusikia mapenzi yoyote kwake. Basi jioni fulani, kanialika chumbani kwake kunywa soda na biskuti na kwa Maongezi zaidi. Sasa kama ulienda jeshi unajua njaa kali unayokuwa nayo. Nikaenda, kanikaribisha vizuri, nilipewa soda na tukawa tunaongea. Basi nikaona mwenzangu anabadilika ghafla! Mara ananikumbatia kwa nguvu, na kunibusu na mengine. Nikajaribu kuaga lakini jamaa hakuniachia. Baada ya ku-plead naye aniachie, kaniachia. Kaomba msamaha na kaniomba niendelee kukaa nimalize hizo soda alizoninulia.

Kama mjinga nikamwamini, nikakaa nakunywa hizo soda. Tukaendelea na Maongezi, kukaa kidogo huyo kanirukia, najaribu kusimama huyo, kanivuta na kuniangusha kitandani! Mimi saa hizo nikawa naogopa kabisa nia yake!Kaniambia eti, “ukipiga makelele najua nitasema nini! Nyamaza! Huna sababu ya kunikatalia!” LOH! Kanizaba kibao! Nikamwuliza kwa nini anaifanyia hivyo, na mimi nilikuwa namwona kama kaka yangu!Hapo sasa ikaniingia. Nabakwa! Loh!

Nilimpiga mangumi na mateke lakini jamaa alikuwa na nguvu huyo kachana chupi yangu! Baada ya hapo, jamaa kashika miguu yangu huko anafoka kwa sauti kama vile anatoa amri “panua miguu! PANUA MIGUU!” Huko katoa ume wake uliyosimama kwenye suruali! Basi kuona sipanui jamaa kaongeza makofi na kafanikiwa kupanua miguu yangu! Kuona kafanikiwa kupanua huyo kajaribu kupenya. Ilipogusa kwangu nilipiga kelele cha kufa! Nikasema, “Nakuufaaaa!”

Heh! Ghafla jamaa kaniachia kaniambia niende. Alisema, “Nimeigusa na ume wangu, unatosha!” Nenda zako! Na ukimwambia mtu najua nitasema nini!”Loh nilikimbia bwenini na giza lile la Masange huko nalia. Wenzangu wananiuliza vipi, nikashindwa niseme nini! Kwanza niliona haya! Fikiria, niliona haya (shame)!Kesho yake nikaenda dispensary na kujiandikisha mgonjwa. Sikwenda kazini Officer's Mess bali nililala bwenini.

Siku iliyofuatia huyo Afande mshenzi kapita bwenini kwetu kaulizia hali yangu, na mimi huko natetemeka kwa woga nikashindwa niseme nini. Alininunulia Orange squash na biskuti na kuzileta bwenini. Sitasahau alivyonitazama! Ilikuwa kama vile anapanga jinsi gani atanipata. Baada ya hapo alimwopoa msichana mwingine na huyo alimkubali kabisa. Akawa analala kabisa huko Officer’s Mess. Hakuna anayemsumbua wakijua ni bibi wa Afisa. Basi, siku za yule jamaa kukaa kambini zikaisha, na yule binti alienda naye Tabora mjini kwa siku kadhaa. Halafu jamaa karudi zake DSM. Yule binti karudi zake kambini! Kumbe alienda bila pass. Alidhania kwa vile yuko na mkubwa hana haja ya pass. Na yule Afande ndo kaondoka kimoja! Maafande waliobakia wacha wamtese huyo binti alivyorudi kambini! Walimtesa kwa Extra drill na mengine mpaka ikabidi Military Police waombe wakuu wamsamehe la sivyo atakufa. Raha yake iliishia kwa suluba! Sijui yule binti alidhania jamaa atamwoa! Kwa nini alimkubali yule mshenzi.

Anyway, kila mtu na vyake. Alivyotoka kwenye suluba tulimwuguza! Siku haizkupita na mimi nilitolewa kazi Officer’s Mess na kupelekwa kwenye kikosi cha Ujenzi na lazima nisema hapo nilifurahi sana. Basi miaka ilipita. Mimi nilikuwa mwandishi wa habari Daily News, tena nilijenga jina. Sasa nikawa napishana na yule jamaa huko kapandishwa cheo na yuko JWTZ. Jamaa anajaribu kunisalimia na mimi napita zangu kimya, namnunia kabisa.

Nilimwona mshenzi, mnyama, na kila kitu kibaya ndo ilikuwa yeye! Angefanikiwa kuingiza na kunimwagia uchafu wake ningejiona mchafu mpaka leo! Miaka kama 20 imepita sasa na bado nina uchungu naye.Jamani nyie wanaume nawaambia kubaka kinaathari zake kwa wanawake. Unataka raha ya dakika na unamwachia mwenzio na uchungu wa maisha! Wengine mpaka wanakuwa wagonjwa wa akili.

Kwa nini nimeamua kuzungumzia kubakwa kwangu hapa, ni kwa sababu naona wasichana wengi wanabakwa, halafu wanaamua kunyamaza kimya. Kisa wakienda polisi na hospitali wanahofia kuambiwa ni Malaya au walitaka wenyewe! Hata mwamanke mwenzako anaweza kukufokea kuwa ulitaka mwenyewe. Tanzania, wanaume walikuwa na usemi wao kuhusu wanawake na ngono. Walisema eti ukimwomba mwanamke halafu akijibu ndiyo, manake ndiyo atafanya. Akisema labda, manake atafanya, akisema hapana, manake hapana. Lakini jamani tendo si inakuwa tamu kama wote mmekubali? Na kama angefanikiwa kuingiza si angeniumiza sana!

Wengine wanasema ningemshitaki. Je, ningemshitaki ingekuaje? Kwanza jeshini mimi ningepewa Extra Drill mpaka niumie au kufungwa jela ya jeshi iliyojaa maji na mbu kusudi niteswe. Kumbuka ilikuwa Tanzania na yule alikuwa ni Kepiteni wakati huo na mimi nilikuwa Private. Hakuna ambaye angekuwa tayari kunisikia zaidi ya wenzangu maPrivate, na yeye alijua hivyo. SHENZI TAIPU!


Posted by Chemi Che-Mponda at 4:13 PM

Labels: Jeshi, Jeshi la Kujenga Taifa, JKT, Masange JKT, Matron, Ubakaji

Kwa mimi sikubaliani kabisaaaa na huyu dada.

Mimi naona labda alijirahisisha kwa kutaka mteremko.

Kwa tuliopita JKT tunasema wazi hakuna issue ya kubakana bali kukubaliana kwani ndani ya JKT hakuna kazi wala shughuli za faragha , shughuli zote zinafanwa mchana kweupeee na linapoingia giza basi mnakutana kwa makundi kwa ajili ya DISCO (kuimba).na baada ya Disco basi ndio utaona watu wawili wawili wanasimamisha minazi kwa makubaliano.

Ila niliona wakina dada wengi sana wakijirahisisha kwa maafande kwa nia ya kupewa kazi rahisi na kuepuka kazi ngumu zinazofanywa na wengi. namkumbuka sana rafiki yangu Sir mejor wa D COY Mazani na Dr Omary (meja) wa pale ruvu namna walivyokuwa wanawashughulikia kwa nia ya kupokea C (mapumziko).

lakini vile vile JKT kulikuwa na uhalali wa kurripoti tukio lolote kwa chief matron kama itatokea afande amekubaka hata kukunyanya sa kijinsia. Na hata CO na OC milango ipo wazi kuripoti tukio lolote.

mama kuwa muwazi katika maandishi yako

 
Ukishaona watu wanarudisha vitu vya zamani ili mradi tu, ujue wamekosa maarifa, nostalgia inawasumbua.

Mafunzo ya jeshi sio kitu kinachohitajika kwa maendeleo ya vijana wa sasa, jeshi linafundisha kutii amri tunahitaji watu ambao wako teyari kubadili mambo na sio kufuata amri za wakubwa.

Pia sioni inasaidia vipi tatizo la ajira,sana sana unafunika tatizo kwa kipindi cha mafunzo, tena wasipoangalia watatengeneza watu hatari zaidi wasio na ajira.
 
jkt ni kupotezea muda watoto wetu, kwani jwtz haitoshi? nafikiri kama lina ulazima wa kuwepo basi kujiunga kwake kuwe kwa hiari lakini isiwe shuruti. mwaka mzima ukifanya mambo ambayo nafsi yako haitaki ni hasara ktk maisha ya binadamu, kwani unaweza kufanya mambo mengine muhimu ya kukusaidia maishani. maisha si lazima jkt.
 
Watu wanaandika mabaya tu ya JKT lakini hawataki kueka mazuri ambayo ni mengi. Kama ni kupima mazuri na mabaya ya JKT mazuri ni asilimia 99.9. Ukweli ni kuwa JKT ni chombo muhimu sana kwa taifa hili. JKT inajenga umoja; ukakamavu kwa vijana; uvumilivu; na uwezo wa kufikiri; na kadhalika. Mtu ukiwa JKT unajifunza mengi yakiwemo ya ubunifukwani hata kughushi ED na ikakubaliwa na afande ni ubunifu. Je, Israel haina JKT ya kwao? vipi, Russia au hata USA kuwa na namna ya JKT au civil defence. Tulishinda vita against Iddi Amin kutokana au kwa sababu ya JKT na mgambo.

Viajana wa siku hizi ambao wanajiita wa dot.com ni bure na hovyo kabisa wengi wao. Hawana uvumilivu hata kidogo wala ubunifu hawana. kazi yao kuiga tu namna ya kuvaa kata K na mikufu kibao. Ni lazima wafundishwe adabu na uvumilivu. Vijana wa dot.com anatoka leo chuo kikuu anataka kuwea na BMW na ghorofa. Itawezekana hiyo? Wamejaa tamaa nyingi. Wengi wao hawaifahamu hata nchi yao. Mtu amezaliwa Muhimbili, amesoma upanga primary; akaja Azania, au Tambaza au Jangwani na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Likizo zote anaishia Dar es Salaam aliko babake na mama yake wanakofanya kazi. Yaani hata Kibaha hapafahamu. Kwa mawazo yake anadhani Dar es Salaam ndio Tanzania hajui kabisa kuwa Tanzania ni nchi kubwa na ina makabila mengi. Kijana wa namna anahitaji JKT imtoe tongotongo za ujinga wa civics.
 
Yaani nimesoma maneno ya watu hapa mpaka nimelia machozi. Mimi nilishuhudia dada zangu wakinyanyaswa na maafande lakini nilishindwa kusema kitu kwa kuhofu Extra Drill. Naona haya, lakini ndo woga niliyokuwa nayo wakati ule. Kwa waliopita JKT wanajua kuna maneno ya Kuruta haina maana! You are nothing hivyo they can do anything to you! Umwambie matron, umwambie afande hawatakutetea hata kidogo! Afande mwenye anamwogopa ule afande juu yake!

Kama JKT itarudishwa basi kuwe na sehemu ambao vijana wataweza kupeleka malalamiko yao bila hofu. :A S-omg:
 
Mimi nilipitia JKT Opresheni Nguvu Kazi. Nilikuwa Mlale JKT. Kwa kweli najiuliza kwenye JKT ilinisaidia nini zaidi ya kupoteza mwaka wa maisha yangu. Tulikuwa tunalipa wananchi kwa kutusomesha A level eti? Nilishuhudia mabiniti wakinayayaswa kwa kuwa mboga ya maafande. Nimeona vijana waliojifanya eti wasomi wakisurubiwa hadi kujinyea. Wanasema Jeshi la Kujenga taifa, tulijenga nini?

Kuna mwanablogu Da Chemi ametoa mada kali kuhusu yaliyompata akiwa JKT. Swahili Time: Marudio - Miaka Baada ya tukio kaniomba Msamaha! Nasikia JKT inarudishwa mwakani. Vijana wamekuwa wengi mno sasa hayo makambi yatakuwa wapi? Hela ya kuwalisha itatoka wapi? Idadii ya vijana ni karibu mara 10 ya enzi zetu. Siwezi kuruhusu vijana wangu hasa binti zangu waende jeshini. Hapana.:yell:

Wanatafuta totos na kusambaza ukimwi. Sisi tuliopitia huko tunajua, kilichowajili mabinti.
 
..ilifikia mpaka waziri mmoja wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa akawa "anajinafasi" na makuruta wa kike wakati wa kikao cha bunge.
 
Watu wanaandika mabaya tu ya JKT lakini hawataki kueka mazuri ambayo ni mengi. Kama ni kupima mazuri na mabaya ya JKT mazuri ni asilimia 99.9. Ukweli ni kuwa JKT ni chombo muhimu sana kwa taifa hili. JKT inajenga umoja; ukakamavu kwa vijana; uvumilivu; na uwezo wa kufikiri; na kadhalika. Mtu ukiwa JKT unajifunza mengi yakiwemo ya ubunifukwani hata kughushi ED na ikakubaliwa na afande ni ubunifu. Je, Israel haina JKT ya kwao? vipi, Russia au hata USA kuwa na namna ya JKT au civil defence. Tulishinda vita against Iddi Amin kutokana au kwa sababu ya JKT na mgambo.

Viajana wa siku hizi ambao wanajiita wa dot.com ni bure na hovyo kabisa wengi wao. Hawana uvumilivu hata kidogo wala ubunifu hawana. kazi yao kuiga tu namna ya kuvaa kata K na mikufu kibao. Ni lazima wafundishwe adabu na uvumilivu. Vijana wa dot.com anatoka leo chuo kikuu anataka kuwea na BMW na ghorofa. Itawezekana hiyo? Wamejaa tamaa nyingi. Wengi wao hawaifahamu hata nchi yao. Mtu amezaliwa Muhimbili, amesoma upanga primary; akaja Azania, au Tambaza au Jangwani na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Likizo zote anaishia Dar es Salaam aliko babake na mama yake wanakofanya kazi. Yaani hata Kibaha hapafahamu. Kwa mawazo yake anadhani Dar es Salaam ndio Tanzania hajui kabisa kuwa Tanzania ni nchi kubwa na ina makabila mengi. Kijana wa namna anahitaji JKT imtoe tongotongo za ujinga wa civics.


Loh! alisema kweli marehemu Shaban Robert "faraja kubwa ajabu kwa mtu ni kusahau". JKT ni jeshi la kubomoa nchi wala si kujenga. Kweli kulikuwa na sababu za maana mno kuanzisha jeshi la kujenga taifa wakati huo ambazo kwa sasa zinabidi kuwekwa kwenye kaburi la sahau. Kwanza kilichosababisha kusimamishwa kwa jeshi la kujenga taifa kwa mujibu wa sheria ni ukweli kuwa jeshi halikuwa linajenga taifa bali lilikuwa linabomoa taifa. Pamoja na mbwembwe za uzalishaji wote kuanzia mahindi, mpunga, kahawa, tumbaku na vingine vingi badi jeshi lililobatizwa la kujenga taifa lilihitaji fedha nyingi kutoka serikalini ili lijiendeshe. Huo ni ushahidi tosha kwamba halikuwa la kujenga taifa. Mheshimiwa mmoja alieleza vizuri kabisa kwamba jeshi hili limekuwa chanzo mahususi kabisa cha ufisadi. Ni nani ambaye kweli alienda JKT ambaye hajawahi kuiba? Anyooshe mguu (maana mkono anaweza kuona haya). Kumweka mtu kwenye mazingira kama hayo (wengine wameita ubunifu) ni kumlazimisha kuwa na tabia mbaya ambayo ni hasara kubwa kwa taifa letu. Kwa kiasi kikubwa ubabaishaji ndani ya taifa letu tunaoushuhudia sasa kuanzia wanasiasa na hasa wataalam unatokana na JKT. Kule ungeweza kuwa daktari bila kusomea ilimradi uwe miongoni mwa watu wa awali kufunga mguu na kusonga mbele pindi wito huo unapotolewa. Tumejionea wenyewe uzoefu huu ukitumika ambapo watu wasio na utaalam unaohitajika mahali hujipachika kwa hasara kubwa ya taifa hili. Wizi wa vitu kama fedha za umma na mitihani umekithiri kwa kuendekeza tabia za JKT. Kama kuna tofauti ya dhahiri kati ya waliopitia JKT na wale ambao wamepona ni uaminifu (hasa wa mali).

Pamoja na mengi yote kurejesha JKT ni kutaka kuliangamiza taifa haraka zaidi (kabla ya wakati). Achilia mbali suala la ujambazi unapoongeza watu wanamudu kutumia silaha za kivita na wakakamavu, lakini tumeshuhudia vijana wa sasa ambao hawaogopi vitu kama mabomu na risasi (maandamano ya Arusha, Mwanza na vyuoni ni ushahidi). Sasa kwa jinsi nchi ilivyo na maono, inataka vijana hawa (kwa wingi kabisa) wazijue silaha zenyewe na wawe na ukakamavu mkubwa zaidi, kama hamuichimbii kaburi nchi mnafanya kitu gani? Sasa hivi kwa kukosa ukakamavu, vijana hawa hata ukuwaruhusu wafanye maandamano kwa siku mbili, nusu yao hutawaona siku ya pili. Leo unataka uwape ukakamavu! Ukakamavu una mahali pake na usipotumika vizuri ni hatari. Tutakuwa na watu wanaojua kuzitumia silaha kwa wingi kabisa hasa vyuoni - sikilizeni penalti hiyo kwenye redio zenu! Mimi simo, simo kabisa.

JKT ilihitajika wakati ule tuna mapambano ya ukombozi wa Afrika ( sasa hivi makaburu ni rafiki zetu - "wapendwa wawekezaji"), haya huyo adui Idd Amin nchi yake na zinazotuzunguka tuna mpango wa kuuungana (Shirikisho la Afrika Mashariki). Adui yetu wa kutufanya tuhitaji jeshi kubwa kiasi hicho kwa gharama kubwa ni nani hasa? Kama kuna fedha ambayo haina kazi wale maadui watatu bado hatujawapiga vya kutosha hata baada ya geresha za miaka hamsini, bora zielekezwe huko.

Jambo muhimu kabisa, hivi katika ufisadi huu ni nani miongoni mwa hao vijana atakuwa yuko tayari kufa kulinda nchi ambayo inapigwa mnada asubuhi, mchana , jioni na usiku (mara nne kwa siku). Kwa ujumla mazingira ya wakati JKT iliposhamiri hayapo na wala hayatakuwepo kwa muda mrefu. Tusijidanganye kuwa tutajenga uzalendo kwa kupelekana JKT. Wala tusilishane uongo eti tunajenga mshikamano na umoja (mitandao ya simu imefanya makubwa zaidi ktk uwanja huo) kwa kupotezeana muda huko JKT. Hivyo vitu havipo huko. Kijana wa kidato cha sita hata kama hajatoka nje ya Dar es salaam, enzi hizi za (zanyasi na tekelinalotujia, akitaka) atakuwa anajua yanayotokea sehemu si za Tanzania tu bali duniani kote. Hivi kweli watu hawaijui Somalia kwa vile hawajafika huko? Mawazo ya ajabu sana katika enzi na wakati huu.

JKT ya mujibu wa sheria, inatakiwa kuzikwa kwenye kaburi la sahau. Sahauni tu kwani kusahau ndiyo faraja kubwa ajabu binadamu aliyotunukiwa na Mwenyezi Mungu. JKT ni utumwaduni mbaya sana usiohitaji kuhuishwa wa kutumia vibaya muda, nguvukazi na fedha za taifa hili. Laana na iwe juu yake atakayekuwa mstari wa mbele kushabikia uhalifu huu!
 
Watu wanabakwa majumbani kwao, mashuleni, mtaani, mahotelini n.k. Hiyo tu haitoshi kusema JKT haina faida. Mimi nilikuwa Makutopora ( makutu poa! ) operation vyama vingi. Kuna tuhuma kama hizo zilimfikia Maj Gen Makame Rashid...nilishuhudia Afande akifukuzwa kazi kwa unyanyasaji wa kijinsia.

JKT ilinifundisha mengi, ikiwa ni pamoja na kujiheshimu, kuwa mkakamavu ( kila gwaride sikuwahi kukosa TANO BORA! ), kufanya kazi za kujitegemea. Nilijifunza kufyatua na kuchoma matofali, nilijifunza namna ya kuandaa na kulima bustani ya mboga mboga, pia nilijifunza kuwa mjanja - niliwahi kushinda kesi mahakama ya kijeshi.

Mbali na yoye hayo, JKT nilipata marafiki kutoka kila kona ya Tanzania ambao hadi leo hii ni marafiki wangu wa karibu sana, kwani kwenye magogo tulienda wote, mbinu za medani na ujanja wa porini tumejifunza wote, kwenye miraba ya zabibu tulikuwa wote - kupalilia na kuzinyatia usiku pia! Nilijifunza kupiga pasi na kutia wanga kwenye nguo, nilijifunza kung'arisha kiatu hadi nikapewa zawadi! pia nilijifunza kushona viatu.

Kama kuna kitu ambacho kimeacha taswira ya kudumu ya JKT akilini mwangu ni mafunzo ya silaha za kijeshi. Ku dismantle SAR na AK47 na kuzi assmle tena huku afande akiwa amekusimamia mgongoni ulikuwa mtihani mkubwa ambao ukipita unajiona umefika hata pale ilipokugomea na afande akakuambia weka jino! Mafunzo ya kulenga shabaha kule "range" nayo yalikuwa muhimu ingawa mwanzoni risasi nyingi zilikosa "bull" na kulenga mijusi vichakani! Niseme tu kuna akinadada walinitoa jasho kwenye range kwani kila risasi waliyo fyatua iligonga target! Kama siyo JKT, nisinge pata nafasi ya kujifunza silaha mbali mbali kama vile bastola, bunduki ( SAR, AK, LMG ), mabomu ya kutupa kwa mkono etc etc!

JKT pia nimejifunza uvumilivu wa shida both physically and mentally. Bootcamp design yake ni kuhakikisha kwamba mrengwa anakuwa na mental and psysical resilience. Pia inakupa uwezo wa kustahimili a certain amount of stress. Hata sasa nikiangalia nyuma naona JKT imenisaidia sana katika kujenga stadi za uongozi i.e. Leadership Skills, na team work. Pia kuthamini mchango wa watu wngine katika kufanikisha kazi ya kikundi.

Pia JKT ilinifundisha kuwa humble. Kama mzee umepandisha vidato ( form six !) halafu unakuwa chini ya afande ex form 4 ama volvo ( volunteer ) ex darasa la saba inabidi kweli unyenyekee. Hii inasaidia sana kutojiona nshomile hata baada ya kumaliza chuo kikuu nimeweza kwenda vijijini na kukaa meza moja na wazee na wanavijiji na ku-appreciate local knowledge and expertise. respect!

On the bigger picture, JKT imenisaidia sana kuwa na mtizamo wa kitaifa zaidi and not parochial insular attitude. Tusichukulie kwamba nazi moja ikiharibika, au mbili au tatu basi tenga zima limeoza!. Kuna haja ya kuangalia mfumo mzima wa JKT kwani advantage zake zinazidi disadvantage. Pia issue ya enforcement ya maadili ya kijeshi na kibinadamu nayo iangaliwe pia. Given the opportunity I would recommend everyone kwenda JKT.
 
Watu wanaangalia ukakamavu but serikali imeiandaa vipi nchi kuwa na watu wenye mbinu za kijeshi lakini hawana ajira?je wiz¨¬ hauta ongezeka?
 
Aaah wapi? JKT ya Nyerere si ndiyo iliwapika hawa akina Lowassa, Sitta, Mahalu na mafisadi wengine? Kama umeshindwa kujenga uzalendo kwa mtu tokea akiwa mtoto mdogo hauwezi kuujenga kwa mwaka mmoja atakapokuwa JKT.
<br />
<br />

Nakubaliana na wewe, inabidi vijana wafunzwe uzalendo tangu wakiwa shule za msingi.
 
ukishaona watu wanarudisha vitu vya zamani ili mradi tu, ujue wamekosa maarifa, nostalgia inawasumbua.

Mafunzo ya jeshi sio kitu kinachohitajika kwa maendeleo ya vijana wa sasa, jeshi linafundisha kutii amri tunahitaji watu ambao wako teyari kubadili mambo na sio kufuata amri za wakubwa.

Pia sioni inasaidia vipi tatizo la ajira,sana sana unafunika tatizo kwa kipindi cha mafunzo, tena wasipoangalia watatengeneza watu hatari zaidi wasio na ajira.

yaani umeongea pointi tupu...
 
vocational training kama mawazo yangu yalivyo ninyi ccm si mna hela na hiyo serikali yenu dhaifu msipoteze muda wa vijana wetu na kwenda kuwaambukiza ukimwi bure anzisheni vyuo vya ufundi,vijana wakasome huko.mimi hadi leo sielewi ni faida gani nilipata kwenda jkt,nikupe pole dada yangu kwa masaibu yaliyokupata,nakumbuka nilikuwepo masange hata intake nimeishaisahau ila ni 1988 acha kabisa mabinti kwa jinsi walivyo si wavumilivu wa shuruba wengi waliishia kufanya mapenzi na hao maafande,nakumbuka dada mmoja aliyemaliza form six shule moja maarufu ya wasichana hapa dar alipata mimba na akaja dar kuitoa waligalagazwa mno,jkt haifai na wenye mabinti DONT TRY THIS,jkt si kwa sisi inawafaa waisrael kwa vile wao wana vita isiyoisha na waarabu.
 
Back
Top Bottom