Kusuluhisha ugomvi baina ya wapenzi: Is it possible...?

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Habari wanajamvi

Leo nilipokuja ofisini nimemkuta office mate wangu amevimba jicho la upande wa kushoto, Kuuliza kulikoni shost akanisimulia kuwa amepigwa na mpenziwe. Nikamaka kisha nikamwuliza kisa? akanambiia walikuwa na kajiugomvi kao kama siku mbili zilizopita wakawa wamechuniana kila mmoja na hamsini zake........

Jana jioni mpenzi wake yule alimfuata nyumbani kwake akaanza kumpapasa ili apatiwe 'starehe' lol ...... binti akauchuna akagoma kata kata kuufungua 'mlango wa club'. Shemeji yangu yule hasira zikampanda yakamtoka ya kumtoka mitusi mara oh unaye bwana ndo mana umeninyima mimi..... almradi yakamtoka tu ya kumtoka (nadhani ni frustrations!) na mwisho akammalizia na kibao cha shavu........ akatimka zake (sikuamini wakati nasimuliwa hayo!!)

Mwisho wa mazungumzo, shost akanipa mtihani, kaniuliza swali eti.
" Kosa langu nini hadi anipige? tumekorofishana halafu yeye anakuja anadai 'chachandu' si ni haki yangu kukataa au nakosea?"

Nimeshikwa na kigugumizi, nimempoza nikamwambia tuliza kwanza hasira halafu kesho ukija tutazungumza! Ila ukweli ni kuwa sina jibu la kumpa

Je wanajamii.......... Is it possible kutenganisha hivi vitu viwili?
 
aaah!!
mi nadhani huyo rafiki yako amekosea sana!
waliogombana ni wao lakini wale "rafiki wawili" (jogoo na mtetea) hawajagombana wanatakiwa waendelee kusalimiana!!
 
aaah!!
mi nadhani huyo rafiki yako amekosea sana!
waliogombana ni wao lakini wale "rafiki wawili" (jogoo na mtetea) hawajagombana wanatakiwa waendelee kusalimiana!!

Eh zamaulid

Kwa hiyo ah hata sijui niulizeje ... kwa hiyo its possible kutenganisha hivi vitu viwili!! Aksante
 
Mpe pole sana kwanza, pili hajakosea kitu ni haki yake kukataa...sasa basi kwakua sheria zetu hazifuatwi alikua aende kumshitaki tu ili achukuliwe hatua hakuna sheria inayo mruhusu yeye kumpiga kwanza hata hawajaona sio? hata kama anampenda bora uwe huru ama mfungwa wa kula kichapo? i hope ni jasiri wa kuchukua hatua za kisheria
 
no huyo dada kakudanganya kitu flani,
kwa siku mbili wamegombana, wakachuniana maana yake walikuwa hawaongei hawa kila mmoja akawa na 50 zake.
then jamaa aje moja kwa moja na kuanza ''kudai tunda la uhuru'' si kweli,

muulize kisa cha ugomvi kilikua nini mpaka wachuniane?
 
Kweli JF patamu...vituko haviishi..hii ndiyo ya kufunga wiki eh??? one simple thing...mtu amekukosea, umekasirika naye, utatoa wapi raha ya kumpa mchezo!!! hana haki yoyote kumzaba mwenzie kibao...duh kama ingekuwa mimi nimgemwekelea nyundo hapo hapo!!!!
 
Mh Edson hadi huko? si ntaambiwa mfukunyuku?... hapana mie nimeangalia tu kilichojiri yaani kupigwa kwa sababu ya kunyima kutoa tunda. Inawezekana amenidanganya eh!
 
Kweli JF patamu...vituko haviishi..hii ndiyo ya kufunga wiki eh??? one simple thing...mtu amekukosea, umekasirika naye, utatoa wapi raha ya kumpa mchezo!!! hana haki yoyote kumzaba mwenzie kibao...duh kama ingekuwa mimi nimgemwekelea nyundo hapo hapo!!!!

Na ndio pa kujifunzia baadhi ya mambo shishi!

Yaani nahisi wewe ungemaka kama nilivyomaka mimi! Au kwa kuwa ni mwanaume anahisi anayo nguvu ya kumlazimisha?

Hivi mpenzio wewe shishi ukimkosea afu akakasirika, utakuwa kweli na nguvu ya kumpelekea mkono kumtekenya?....... kabla hujamwomba msamaha?

Mi mwenzenu roho yangu ndogo.:(
 
Hapo kwa maoni yangu kuna kitu hakijakaa vizuri, yaani wagombane, kisha jamaa aend enyumbani kwake na kuomba mchez (ina maana hawakai pamoja) hiyo inakujaje? MJ1 hebu muulize chanzo cha ugomvi ni nini, cause kama ulikuwa kweli ugomvi, asingeweza eti kwenda hadi kwao na kufikia kulala kitandani na kuomba mchezo na binti kubana miguu!

Chanzo ni nini? simtetei mwanaume lakini mazingira ya huu ugomvi yamekaa kinamna namna!

Nikirudi kwenye swali la msingi...ni vigumu kutenganisha hasira na starehe....kama kuna mwenye hasira hapo hakuna starehe, hata katika vitu vya kawaida,, lakini pia kama hasira ipo ni kuiondoa kwanza na sio kuipalilia. walichotakiwa kufanya ilikuwa kutatua kwanza ugomvi wao, labda binti badala tu ya kubana miguu,, angempooza kwanza jamaa ili wayaongee yaishe kabla ya kumpa kidude,, au huyo binti hajafundwa?
 
George_Porgie mvivu wa kusoma!
Kwenye thread hapo nimeandika : kutenganisha hasira na ile starehe!

Jamani

Oooh, kumbee!
aisee ile starehe bana yataka akili i-relax, ukiwa na hasira starehe haipandi kabisaaa, ndo maaana jamaa katolewa nje matokeo yake hasira ikampanda.
ila hapo nahisi jamaa hakutumia busara hata kidogo alikua analazimisha, mwanamke hata akasirike mpaka atake kupasuka ukimwingia na maneno mataamu ya kumpoooza mbona anakuelewa na mzigo anakupa bila nongwa!, wanawake bana wameumbwa na huruma ya hali ya juu, huruma ya ukweli toka moyoni.
 
Hapo kwa maoni yangu kuna kitu hakijakaa vizuri, yaani wagombane, kisha jamaa aend enyumbani kwake na kuomba mchez (ina maana hawakai pamoja) hiyo inakujaje? MJ1 hebu muulize chanzo cha ugomvi ni nini, cause kama ulikuwa kweli ugomvi, asingeweza eti kwenda hadi kwao na kufikia kulala kitandani na kuomba mchezo na binti kubana miguu!

Chanzo ni nini? simtetei mwanaume lakini mazingira ya huu ugomvi yamekaa kinamna namna!

Nikirudi kwenye swali la msingi...ni vigumu kutenganisha hasira na starehe....kama kuna mwenye hasira hapo hakuna starehe, hata katika vitu vya kawaida,, lakini pia kama hasira ipo ni kuiondoa kwanza na sio kuipalilia. walichotakiwa kufanya ilikuwa kutatua kwanza ugomvi wao, labda binti badala tu ya kubana miguu,, angempooza kwanza jamaa ili wayaongee yaishe kabla ya kumpa kidude,, au huyo binti hajafundwa?

Kusema ukweli kaka sikuuliza chanzo cha ugomvi wa juzi mie nilichouliza ni kwa nini kapigwa lol si unajua mie nlishaathirika na hawa wadudu so nikisikia ugomvi basi nafanya reference lol.... sifai kuwa hakimu!

Ila Zamaulid kaniambia eti mkigombana nyie wale marafiki wawili hawagombani yaani hapa kaniacha hoi asa huyu mwangu mie akija....... ntaweza kwelimpokea? kama hataambulia mateke lol
 
Oooh, kumbee!
aisee ile starehe bana yataka akili i-relax, ukiwa na hasira starehe haipandi kabisaaa, ndo maaana jamaa katolewa nje matokeo yake hasira ikampanda.
ila hapo nahisi jamaa hakutumia busara hata kidogo alikua analazimisha, mwanamke hata akasirike mpaka atake kupasuka ukimwingia na maneno mataamu ya kumpoooza mbona anakuelewa na mzigo anakupa bila nongwa!, wanawake bana wameumbwa na huruma ya hali ya juu, huruma ya ukweli toka moyoni.

Nakupa tano hapa Georgie_Porgie

Wanaume wengi hawalijui hilo. Huyu kafanya hivi ni girlfriend wake ila kwa wale ambao wako ndoani mara nyingi wapo wale ambao wakimkorofisha mamsap hawakumbuki kuomba misamaha wala kubembeleza ikifika usiku mkubwa wanaparamia tu utafiikiri abiria wa magari ya Mbagala matokeo yake mama anakuacha tu uchakarike mwenyewe- asa starehe iko wapi hapo? utamlaumu kweli.?
 
Kusema ukweli kaka sikuuliza chanzo cha ugomvi wa juzi mie nilichouliza ni kwa nini kapigwa lol si unajua mie nlishaathirika na hawa wadudu so nikisikia ugomvi basi nafanya reference lol.... sifai kuwa hakimu!

Ila Zamaulid kaniambia eti mkigombana nyie wale marafiki wawili hawagombani yaani hapa kaniacha hoi asa huyu mwangu mie akija....... ntaweza kwelimpokea? kama hataambulia mateke lol

Si rahisi kutoa ushauri ambao utabalance pande zote mbili (Mume na Mke) mpaka akueleze vyema waligombania nini mara ya kwanza. Inawezekana kabisa ni muendelezo wa ule ugomvi wa awali. Labda jamaa alikuwa hana imani na huyo dada na dada naye akawa anabisha wakatoutiana. sasa jamaa kuja kuomba tunda baada hizo siku 2 na kunyimwa inawezekana akaona ndio yale yale akamuua ku "loose control" ya mikono yake.
 
mwendapole inawezekana kabisa ndugu yangu kuwa jamaa alikuwa anahisi kuibiwa afu binti akakanusha so jamaa akaamua kuzuka home pengine alihisi kuwa binti katoka kumegwa so akaona ngoja ni'ingie' nihakikishe lol binti akaona atashtukiwa dawa ni kubana no matter what lol....... ila hii sikuuliza ningejua ningechokonoa zaidi
 
Wameoana au ni marafiki tu? Hivi hawajaoana hiyo jeuri ya kuanza kumpiga dada wa watu wakati kila mtu anaishi kivyake kaitoa wapi? Nahisi huyu dada amemfia sana jamaa na ndo maana jamaa anaweza kumpiga akiwa nyumbani kwake na mdada akavumilia, yaani ingekuwa ni mimi yuko kwangu halafu ananipiga break ya kwanza ingekuwa ni polisi,halafu suluhu zingine zingefanyika baadae.
 
Back
Top Bottom