Kusudio la kuishitaki airtel

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,865
4,249
Ndugu zangu, hivi majuzi niliona tangazo la airtel kuwa ukinunua moderm ya airtel kwa shs elfu 30,000 utapata internet bure kwa miezi 6. Baada ya kuona hivyo nilienda kwenye duka lao na kukuta vipeperushi kibao vikiwa na ujumbe kama huyo yaani internet bure kwa miezi 6. Nikanunua. Baada ya kujaribu ikawa haifanyi kazi, kuulizia customer care wakaniambia ni lazima ni recharge eti kwamba offer hiyo ni ya siku moja kwa mwezi na hivyo ni siku 6 ndani ya miezi 6. tena baada ya kutumia kiasi fulani kwa mwezi.

Offer iliyotangazwa ni uongo. Hivyo nakusudia kuwapeleka mahakamani wanipe internet kwa miezi sita kama walivyoandika kwenye mstangazo mimi na wateja wengine wooote walionuna moderm hizo. Vielelezo nilivyonavyo ni tangazo la gazeti, kipeperushi na risiti ya kununulia modem

Naomba nieleweshwe namna ya kuframe madai na sheria ninazoweza kutumia. Pia kama kuna mwanasheria ambaye yuko tayari kuendesha case hii tafadhali ani pm. Nitalipa gharama za case husika. Asanteni.
 
Hapo mkuu watakufunga wewe kwani huwa wanaandika Vigezo na masharti kuzingatiwa, Yaani terms and condition apply. So ulitakiwa uombe kupewa hizo terms na conditions.
 
Mi naomba ushauri,,,,
Nina matatizo na tigo, wanakula hela zangu ile mbaya, ilifikia hatua kuwa nikiuliza salio najibiwa in terms of negative, yaani na daiwa, wakati sijawahi kuchukua mkopo, vile vile, kifurushi cha internt sio 24 hrs kama wanavodai, nikiunga saa 4 usiku natumiwa message kuwa mpaka saa 4 usiku ya siku ya pili kifurushi ndo kitaisha, kumbe ikifika saa 6 usiku ule nloinganisha kifurushi hakifanyi kazi tena, na ukitaka kujiunga na chengine wanakwambia bado upo kwenye kifurushi, kuna siku nyengine nlijiunga na sms zao, hazikufika mia zikagoma kwenda, nkajaribu kuuliza salio nikajibiwa ninazo kiasi fulani za message lakini bado zikawa haziendi, nikavumilie kidogo, kisha nkauliza tena salio nkashangazwa kwa jibu nlopata, message ni zero zeroooo!! Ukiingia facebook na kuitizama page yao utakuta lawama kibao na hawazishuhulikii, customer care utakaa 2 hours umewekwa hold kwenye simu unaambiwa mhudumu yuko bize, PAGE ya FB hawakujibu pia,,,, yani wizi kwenda mbele! Hii TCRA ina umuhimu gani?
 
tatizo tulilonalo Tanzania, hatuna mamlaka ya kutetea watumiaji (end users)..ndiyo maana watu wanafanya mambo wanayoyataka......hii nchi inakela sana:tape2:
 
Wewe wa tigo unatakiwa ukiunganisha wakileta magumash unazima 4n kwanza na unatoa cheap yako unatulia kama dakika 3 then unaweka tena. Mie ilikuwaga hvyo nikapiga custormer care ndo wakaniambia hvyo mpaka leo haisumbui. Kuhusu salio hlo cjui kwa kweli, usisite kuwapigia.
 
Mkuu Vigezo na Masharti Kuzingatiwa, hii ni contract baina yako mnunuzi na airtel.., sasa kwenye hii formal contract mnaingia kwenye makubaliano huku terms and conditions walizoweka wauzaji ndio zinazopelekea wewe kukubali offer..

Alafu bure inamaanisha mambo mengi (Bure inaweza ikawa kwamba unapata bure MB kadhaa) usipozitumia zinakaa miezi sita ukizitumia zinakwisha kwa siku moja.., yaani ule ubure unakaa miezi sita lakini una limit.

Hapo customers wanachoweza kufanya sio kuwapeleka mahakamani bali kuwapa bad publicity kwamba Airtel they are not good with their words and they are ripping people off (Binafsi sijali kuhusu huo ubure, bali speed yao imekuwa mbovu sana.., yaani hata kama ingekuwa kweli bure kwa miaka kumi lakini kuna faida gani kwenda mwendo wa kinyonga kwa miaka kumi)
 
Safi sana aisee, kuna ushahidi mwingine: humu JF wamebandika hiyo adverts na hata muda huu naliona hili tangazo!! Tuwasubiri wanasheria.

Ndugu zangu, hivi majuzi niliona tangazo la airtel kuwa ukinunua moderm ya airtel kwa shs elfu 30,000 utapata internet bure kwa miezi 6. Baada ya kuona hivyo nilienda kwenye duka lao na kukuta vipeperushi kibao vikiwa na ujumbe kama huyo yaani internet bure kwa miezi 6. Nikanunua. Baada ya kujaribu ikawa haifanyi kazi, kuulizia customer care wakaniambia ni lazima ni recharge eti kwamba offer hiyo ni ya siku moja kwa mwezi na hivyo ni siku 6 ndani ya miezi 6. tena baada ya kutumia kiasi fulani kwa mwezi.

Offer iliyotangazwa ni uongo. Hivyo nakusudia kuwapeleka mahakamani wanipe internet kwa miezi sita kama walivyoandika kwenye mstangazo mimi na wateja wengine wooote walionuna moderm hizo. Vielelezo nilivyonavyo ni tangazo la gazeti, kipeperushi na risiti ya kununulia modem

Naomba nieleweshwe namna ya kuframe madai na sheria ninazoweza kutumia. Pia kama kuna mwanasheria ambaye yuko tayari kuendesha case hii tafadhali ani pm. Nitalipa gharama za case husika. Asanteni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom