Kustaafu maana yake nini? Kwanini viongozi waliojiuzulu kwa kashfa wanaitwa wastaafu?

Rabin

Senior Member
Mar 21, 2009
181
39
Ndugu zangu naomba minieleweshe hasa matumizi ya neno hili kustaafu katika siasa zetu hizi za kimasikini, kwa nini kiongozi anaye ondoka madarakani kwa kashfa kabla ya kumaliza muda wake anatambuliwa kama mstaafu? hakuna neno lingine linalofaa kutokana na namna alivyoachia madaraka? wanaposema waziri mkuu mstaafu mh. EL siwaelewi, nisaidieni, kwani tunamuogopa nani?
 
Mstaafu lazima astaafu kwa heshima zote za utumishi wa umma ikiwemo nidhamu, uadilifu, utii na heshma. kwa kesi ya EL mie sidhani kama ana heshma ya kuitwa PM mstaafu kwa kweli. Je amestaafu akiwa na hivyo vigezo vyote nilivovitaja hapo?

Tafakari!
 
Back
Top Bottom