Kusamehe ni kitu kigumu sana:

Kusahau inakuwa ni ngumu ila kumtakia mtu uliyemsamehe kuwa nimekusamehe ila sitakusahau ni kama hujatekeleza sawa sawa msahama wako
Msamehe na ishi kawaida na lione tukio limepita japo kuna sehem unakumbuka kitu kinakutia machungu ila usimlaani yule mhusika moyoni mwako kuwa bila yeye lisingetokea

Lakini mbona mwenyezi mungu anatusamehe makosa yetu?
 
bebii nakubaliana na wewe kusahau ni ngumu sana ila we reach a point ya kusema it is over now we have to move on with our life and life has to go on
sijaelewa hayo maneno ya mwishoni mwishoni
 
Kusamehe bila kusahau ndi kutosamehe.....

bora useme sijasamehe but i let it go......
Nafikiri zuri la kufanya ni hilo la kuwacha yapite, kwani
unaweza kusamehe kwa dhati na baada ya muda ukusahau.
Tatizo linakuja pale uliyemsamehe akarudia kosa lile lile.
Hapo anafufua kumbukumbu zako na kusahau na penginey
kusamehe ako inakuwa kazi bure.
 
sijaelewa hayo maneno ya mwishoni mwishoni

Namaanisha ifikie mahali useme sasa basi nimeshahuzunika vya kutoha na kukasirika vya kutosha na kulaani vya kutosha wacha sasa nisahau na niendelee na maisha yangu kwani tukio lishatokea na limeisha
 
Namaanisha ifikie mahali useme sasa basi nimeshahuzunika vya kutoha na kukasirika vya kutosha na kulaani vya kutosha wacha sasa nisahau na niendelee na maisha yangu kwani tukio lishatokea na limeisha

Soma post ya MAMMIA,unaweza samehe alafu yule kiumbe au mtu uliye msamehe anakuja kufanya ujinga tena utafanyaje?
 
Kusamehe na kusahau au kutosahau kunategemeana na jinsi MUNGU alivyokupa nguvu i!!Wengine ni wepesi kusema nimekusamehe lakini kila siku anarudia kuongelea jambo hilo hilo, hapo kuna kusamehe kweli! Kanuni ya MUNGU Usiposamehe si rahisi kusamehewa, sharti usamehe ili na wewe usamehe.
Wengine Mungu amewapa nguvu ya kusamehe, utashangaa unakosea na kusamehewa, unarudia tena Bado unasamehewa, Kama na wewe ni MMojawapo Mungu akubariki sana, Na hata wewe ambaye ni ngumu kusamehe na kusahau ubarikiwe pia na upewe nguvu ya kusamehe na kusahau.
 
Soma post ya MAMMIA,unaweza samehe alafu yule kiumbe au mtu uliye msamehe anakuja kufanya ujinga tena utafanyaje?

Ahhhhh mkuu huo ni ujinga na ukiona mtu wa aina hiyo jua hata la kwanza alifanya kusudi na wala sio kwamba hakukusudia
Ahhh hapo ni kwamba kama ni uhusiano bora ufilie mbali bana maumivu mara mbili aise
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom