sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 644
Kusamehe ni kitu kigumu sana ingawaje ni tendo zuri sana kwa upande mwingine .Kwanini ni msamehe mwingine ambaye ananikosea mara kwa mara na wakati mwingine kwa makusudi na wala harudi kuomba msamaha?Kiakili na kwa kutumia busara ya kawaida,unaweza kusema kuwa naweza kumsamehe ndugu yangu huenda akiwa amenikosea mara moja au mara mbilihivi.
Petro alikuwa yuko tayari kusamehe mara saba.Lakini bwana yesu anasema kwamba tusamehe daima,bila kuhesabu ni mara ngapi umekosewa.Kwanini hayao unaweza kujiuliza .Jibu kwamba ndivyo mungu anavyotenda pamoja nasi,yaaani anatusamehe daima,bila mipaka,bila kuhesabu ni mara ngapi tumemkosoea.
Hivyo tunaalikwa kusamehe kama sisi tunavyosamehewa .Kwa upande mwingine kusamehe ni jambo jema kiafya na kisaikolojia au kwa maneno mengine kutokusamehe ni hatari kimwili na kisaikolojia kwa muhusika yaani yule anayebeba kinyongo.Wanasayansi ya jamii wanasema usipo samehe unatengeneza sumu ndani ya mwili wako ambayo inakuteketeza kimwili na kisaikolojia.
Kwa upande mwingine kusamehe nikuishi amri ya mapendo yaani kumpenda mungu na jirani ,ikiwa namaana kwamba kumpenda mwingine hata anapokosa.