Hivi kwa sisi Waafrika halisi kusaidiana kwa jinsi hii na mzazi mwenzako kunawezakana, au tunaiga wazungu????? TUJADILI!!!
Hivi kwa sisi Waafrika halisi kusaidiana kwa jinsi hii na mzazi mwenzako kunawezakana, au tunaiga wazungu????? TUJADILI!!!
Sasa ndugu unaposema tunaiga wazungu unamaanisha nini?Huoni kuwa huyo mtoto aliyebebwa ni chotara ikimaanisha kuwa huenda mama ni mzungu,au mwarabu.Kwa hiyo hapo haigi ndio maisha yenyewe hayo.
Ninamaanisha kuwa si utamaduni wa mwafrika kumsaidia mwnza wake.... Ebu nikuulize tu kidogo, samahani kama nitakuwa nimekosea ulishawahi kumwona baba yako mzazi akimsaidia mama yako kwenye kazi kama kuosha vyuombo, kufua nguo, kubeba mtoto n.k??? . Nahisi haya mambo ya kusaidiana yamekuja miaka ya karibuni, baada ya beijing meeting. Na nahisi ni zaidi kwa wale watu ambao wamesoma nje, au wamekaa sana na mchanganyiko wa watu, na kujifunza.
Mimi kama mimi naweza na nasapoti asilimia mia maana mtoto ni wangu na nilimzalisha mwenyewe sasa akitoka tumboni kwa mama yake ni wajibu wangu kumsaidia maana ye alinisaidia miezi tisa kitu gani mi nikimpa tafu sa ivi?wala sio kuiga wazungu.
Lakini ni vizuri ukakumbuka kwamba wote wawili ni wazazi. Na wewe mwanaume ndio uliyempatia hiyo mimba!!!!!!
Sasa ndugu unaposema tunaiga wazungu unamaanisha nini?Huoni kuwa huyo mtoto aliyebebwa ni chotara ikimaanisha kuwa huenda mama ni mzungu,au mwarabu.Kwa hiyo hapo haigi ndio maisha yenyewe hayo.
Ninamaanisha kuwa si utamaduni wa mwafrika kumsaidia mwnza wake.... Ebu nikuulize tu kidogo, samahani kama nitakuwa nimekosea ulishawahi kumwona baba yako mzazi akimsaidia mama yako kwenye kazi kama kuosha vyuombo, kufua nguo, kubeba mtoto n.k??? . Nahisi haya mambo ya kusaidiana yamekuja miaka ya karibuni, baada ya beijing meeting. Na nahisi ni zaidi kwa wale watu ambao wamesoma nje, au wamekaa sana na mchanganyiko wa watu, na kujifunza.
Kwa kweli mi nimewahi kumuona baba akifanya hayo. Na ni mkulima kabisaa wa kule Rombo hajawahi kwenda ulaya wala nini.
Tena enzi hizo tuna umri wa miaka minne mitano alikuwa anatuogesha, anatufulia nguo, mi nimefuliwa nguo na baba nikiwa darasa la nne, naona na macho yangu kabisa. Mama anaweza akawa anafanya mambo mengine baba yupo anapika, tena tulikuwa tunakiona chakula chake kitamu kama nini!!
Na hiyo imetujenga vizuri, sasa hivi hata kaka zangu wanapika vizuriiii,
Hakuna kusema huyu wa kike wala wakiume, tena enzi hizo tulikuwa na zamu kabisa, huyu anapika leo, kesho kuchota maji, kuosha vyombo, kuokota kuni nk nk nk.
We MHUBIRI ni mbinafsi sana!Swala la kufurahisha nafsi yako tu linaisha pale unapokua na mwenza!Hapo unatakiwa ujitahidi kufurahisha yake na yako..COMPROMISE is the word!!Mtoto wako mwenyewe huwezi kumwangalia?Siku mama yake akiumwa na hamna mtu mwingine wakusaidia itakuaje?Hatuko enzi za ujima bwana!Nenda na wakati!
Mhubiri kazi yoyote ile..na mazingira yoyote!Kwani akiwa na mashoga zake huwezi kumpa break kidogo?We ukiwa na wako anakuja kubanana na nyie sebleni?I don't think so!Ile dhana ya kuonekana bw.ege futeni bwana...be helpfull at all times just like we always are!
ha ha ha mambo ya mume bwe ge hayo na wanawake wenyewe wa kibongo,yeye ndiye atakuwa wa kwanza kukuona bwe ge!
Shiumiti;lakini kumbuka kuwa kuna roles za nyumbani ambazo unaeza sema ziko more musculine na nyingine inapendeza zaidi akifanya mama,kama pia unazingatia mila,desturi na utamaduni wa wahusika.Hapo kwa mfano mama angekuwa anafanya hiyo kazi ya kuosha vyombo,halafu mimi ningekuwa natoa vumbi kwenye carpet au napanga magunia ya mkaa store..Mtoto nitambeba,tena saana lakini siyo katika mazingira na kama alivyobeba huyo jamaa.Na hata kama uko na mzungu,binafsi hawezi akanibebesha mtoto kwa mtindo huo,huku nikiosha vyombo.Imagine hapo mara vuuup wanakuja washkaji au ndugu au jamaa zako na wanakukuta katika hali hiyo,huku bibie kaweka miguu juu kwenye sofa anacheki ma episodes ya dr house!
anyway,tuko tofauti na kila mtu na afanye anachoona kinaifurahisha nafsi yake
Kwahiyo Lizzy utataka nimbebe mtoto na kuosha vyombo wewe ukiangalia TV ? mi napika,kusafisha nyumba na kupiga pasi lakini kuosha vyombo na nguo labda uwe mgonjwa au unataka ninyoshewe kidole mtaani ?Mhubiri kazi yoyote ile..na mazingira yoyote!Kwani akiwa na mashoga zake huwezi kumpa break kidogo?We ukiwa na wako anakuja kubanana na nyie sebleni?I don't think so!Ile dhana ya kuonekana bw.ege futeni bwana...be helpfull at all times just like we always are!
Kumbe na wewe ni mkoloni ehh?Mbona ndoa yako itakua na kazi!Labda ukaoe kijijini!Kwahiyo Lizzy utataka nimbebe mtoto na kuosha vyombo wewe ukiangalia TV ? mi napika,kusafisha nyumba na kupiga pasi lakini kuosha vyombo na nguo labda uwe mgonjwa au unataka ninyoshewe kidole mtaani ?