Kusaga kamwe haguswi, Ruge anaonewa?

Buyaka

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
1,643
1,786


Joseph Kusaga ndio mwanzilishi na kinara wa kampuni ya Clouds FM, kama anavyoelezwa kwenye clip hiyo. Ruge Mutahaba ni General Manager, obviously ni bosi mwandamizi wa Clouds, lakini mwisho wa siku mwajiriwa asiye na hisa wa Joseph Kusaga, CEO and 50% stakeholder wa Clouds. Kwa maneno mengine Joseph Kusaga ndio anaemtuma Ruge.

Beef kati ya Clouds FM na wasanii wanaoongozwa na Mheshimiwa Joseph Mbilinyi, mbunge msanii, limezidi kuchukua sura mpya ambapo tumeshuhudia matamasha ya makundi hayo yakipangwa siku moja na zaidi kuwa na sura ya kupambanisha wasanii wa nyumbani na waalikwa kutoka nje, ambao labda hawana kosa lolote katika tafrani zinazoendelea. Hii picha ina mustakabali gani katika sanaa ya Tanzania katika lenzi za kimataifa, sijui.

Hata hivyo lawama zote na mashambulizi dhidi ya exploitation ya wasanii zinaishia kwa Ruge tu na hazipandi kwenye ngazi za maamuzi, yani the don mwenyewe Kusaga. Hii inachangia tatizo hili kutopatiwa ufumbuzi kwa kukosa nguvu ya maamuzi? Je, Kusaga anaogopwa kwa sababu ya nguvu yake kifedha na heshima ya nafasi yake kijamii kama mmiliki wa chombo kikubwa cha habari?

Binafsi naamini wasanii wanaoilalamikia Clouds na Ruge wana hoja kwa kiwango fulani. Kwenye dili la Malaria No more, kwa mfano, ambalo ndio moja ya mzizi wa fitina wa yanayoendlea leo, nililiona lile timbwili toka mwanzo, nimeona text messages kwenye simu ya Sugu akiwa anaanza kuwasiliana na mabalozi wa USA way before anybody alijua chochote kuhusu mchakato ule. NIlisikiliza utetezi wa Clouds kupitia Ruge lakini sikushawishika, na mwishoni naamini Sugu alikuwa robbed.

Lakini je, nani mhusika mkuu? Ruge anatumiwa kama tambala la deki la Joseph? Joseph Mbilinyi na Vinega wanamwogopa Joseph Kusaga? Isije kuwa Ruge ni anaonewa.

Naomba kuwasilisha.
 
Last edited by a moderator:
Kusaga mtotomwa mjini Ruge wa kuja,kilichopo ni kwamba kusaga anamtumia ruge bila kujijua,ni kama ilivyokuwa nyerere akimtumia kawawa enzi zile na kusababisha kawawa kuchukiwa na wengi huku nyerere akipendwa na wengi wakati maamuzi yote mabaya na mazuri yalifanywa na julius bila kuambilika na yeyote....ruge kwa kuwa mshamba na mpenda sifa kusaga anamtanguliza mbele
 
Time to lay off Clouds you people. Find someone else to bash.
It's just a begging, Anti virus with no apology, virus scan detect and found two virus, Kusaga & Ruge.

390781_164392423660126_100002681085480_249044_1738653985_n.jpg

Kwenye vita ya haki ushindi ni lazima,...........
 
jose kusaga si mwanzilishi ; kama huna uhakika na jambo usililete humu , kampuni imeanzishwa na marehemu alex miaka hiyo jose akiwa mtoto .
 
Mimi kwa mtazamo wangu naona kama kusaga anahusika kimtindo na sio kivile coz jamaa ruge huwa anafanya kazi za nnje sema anatumia wafu fm.........kutangaza mipango yake jamaaa mwizi mmnyonyaji na mzandiki..........nafikili dawa ni kukata virole viwili vya mkono wa kushoto........ili akiwa anataka kuzurumu watu anakumbuka maumivu ya vidole,,,tamaa itamuisha fasta.
 
Back
Top Bottom