Kuruhusiwa Maandamano kupinga ziara ya Joji Kichaka: Je, ni kupanuka kwa demokrasia?

Ninalichukulia jibu lako hilo kuwa ni 'Ndio' mradi mwananchi huyo havunji sheria.

Nadhani nimejitahidi, kwa maana nimesoma x10 kama ulivyosema mwalimu.

Vizuri. Ndivyo hasa nilivyosema. Kumbe "kukremisha" bado kunalipa! Miaka mingi imepita tangu nilivyofanya hivi mara ya mwisho, na wa siku hizi wananiambia mbinu hii imepitwa na wakati, wanazungumzia "student-centred" learning! Mimi nilifundishwa syllabus-bound "teacher-centred" teaching/learning, mwanafunzi anajifunza kile mwalimu anachojua kuwa ni sawa, ndio maana wakifaulu wanafunzi sifa inakwenda kwa mwalimu na wakifeli lawama kwa mwalimu, na pia ndio msingi wa kuwepo kwa syllabus.

Asante kwa kunirejeza kwenye tafakuri hii.
 
Kuna agenda ya siri kuhusu haya maandamano. Hakuna demokrasia ya namna hiyo katika Tanzania kwa sasa labda miaka 20 ijayo.

Kama uhuru wa namna hiyo upo katika Tanzania basi wana JF twendeni tukaandamane kutaka serikali ituambie ukweli ni kiasi gani kilichochotwa toka BOT (EPA), Kampuni ya meremeta na tangold zililipwa kiasi gani, kwanini na lini?. Na pia tutake Mkapa&Co wakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na bila kusahau Lowassa & CO. Kama tutaweza kuandamana bila ya kupigwa virungu, mabuti, mabomu ya machozi na Polisi + FFU ambavyo ni vyombo vya mabavu na mali CCM tokana na ukweli kwamba Polisi, FFU, Usalama wa Taifa wapo kwa ajili ya kuilinda CCM na wala si kuwalinda Watanzania basi nitasema sasa Tanzania kuna demokrasia.

Haya ni maandamano ya kidini kwani yameanzia misikitini na kuandaliwa na mashehe. Kitu cha kujiuliza ni kwanini yamepata kibali na baraka toka serikalini?????????
 
Nawashauri Wazenj waandamane kupinga mazoezi yoyote ya kijeshi ya submarine za kimarekani katika bahari ya Hindi, kwa kisingizio cha ugaidi. Hasara waliotupa mwaka 2006 bado ipo vichwani mwetu!
 
Mie nitaitisha maandamano kupinga makao makuu kuwa Dodoma ni white elephant project over 30 years mihela inaliwa tu wote wako Dar
 
Kuna agenda ya siri kuhusu haya maandamano. Hakuna demokrasia ya namna hiyo katika Tanzania kwa sasa labda miaka 20 ijayo.

Kama uhuru wa namna hiyo upo katika Tanzania basi wana JF twendeni tukaandamane kutaka serikali ituambie ukweli ni kiasi gani kilichochotwa toka BOT (EPA), Kampuni ya meremeta na tangold zililipwa kiasi gani, kwanini na lini?. Na pia tutake Mkapa&Co wakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na bila kusahau Lowassa & CO. Kama tutaweza kuandamana bila ya kupigwa virungu, mabuti, mabomu ya machozi na Polisi + FFU ambavyo ni vyombo vya mabavu na mali CCM tokana na ukweli kwamba Polisi, FFU, Usalama wa Taifa wapo kwa ajili ya kuilinda CCM na wala si kuwalinda Watanzania basi nitasema sasa Tanzania kuna demokrasia.

Haya ni maandamano ya kidini kwani yameanzia misikitini na kuandaliwa na mashehe. Kitu cha kujiuliza ni kwanini yamepata kibali na baraka toka serikalini?????????

Mtambo,

Kuna agenda ya siri gani hapo? Watu wamepanga maandamano yao na wameruhusiwa. Wameandamana, wameenda kulala. Bush kaja naye kapeta, nchi inazidi kwenda mbele, hiyo ni ishara ya kuwepo kwa demokrasia Tanzania hata kama haijafikia kiwango tunachotaka wengine lakini at least kuna hatua.

Ukitaka kuandamana kupinga mafisadi kwani nani amekukataza? Andaa wana JF
wako unaodhani wataweza kwenda mitaani na kuacha kuendelea kuikoma serikali kwa keyboard.

Kuna mambo JK amefanya kuhusu demokrasia ambayo hayakuwepo kipindi cha Mkapa. Toka JK ameingia ni kiongozi gani wa upinzani kapigwa mabomu ya machozi? Au maandamano yapi yamevunjwa na polisi?

Dawa ya kukomesha maandamano yasiyo na maana ni kuyaruhusu, baada ya muda watajiona wajinga na kuachana nayo.

Binafsi ni maandamano machache sana ninayoweza kuhudhuria kwani naona yaliyo mengi ni upuuzi tu na kupoteza muda, lakini bado ninataka kila anayetaka kuandamana aruhusiwe na ikiwezekana kupewa ulinzi, ili mradi havinji sheria za nchi.
 
Kuna agenda ya siri kuhusu haya maandamano. Hakuna demokrasia ya namna hiyo katika Tanzania kwa sasa labda miaka 20 ijayo.

Kama uhuru wa namna hiyo upo katika Tanzania basi wana JF twendeni tukaandamane kutaka serikali ituambie ukweli ni kiasi gani kilichochotwa toka BOT (EPA), Kampuni ya meremeta na tangold zililipwa kiasi gani, kwanini na lini?. Na pia tutake Mkapa&Co wakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na bila kusahau Lowassa & CO. Kama tutaweza kuandamana bila ya kupigwa virungu, mabuti, mabomu ya machozi na Polisi + FFU ambavyo ni vyombo vya mabavu na mali CCM tokana na ukweli kwamba Polisi, FFU, Usalama wa Taifa wapo kwa ajili ya kuilinda CCM na wala si kuwalinda Watanzania basi nitasema sasa Tanzania kuna demokrasia.

Haya ni maandamano ya kidini kwani yameanzia misikitini na kuandaliwa na mashehe. Kitu cha kujiuliza ni kwanini yamepata kibali na baraka toka serikalini?????????

Wangeyazuia mngesema serikali haifuati demokrasia na uhuru wa kujieleza wameyaruhusu mnasema kuna agenda ya siri..welcome to the New World and Millenium
 
Back
Top Bottom