Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeshindwa kazi; yatumika kumhujumu Rais Kikwete

Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
550
Kwa niaba ya Chama changu makini CCM naomba kuwataka radhi Wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano mliokesha usku kucha kusubiri hotuba ya Mpendwa Rais wetu Mh Jakaya bila mafanikio hivyo naomba mtusamehe kwa uzembe uliofanywa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kwa kutokutoa Tangazo la Mh Kuhairisha kuhutubia Taifa siku ya tararehe 30/06/2012.

Kwa sisi wananchi na wapenzi makini wa Chama cha mapinduzi tunaona kuna uzembe wa hali ya juu uliofanywa na wasaidizi wa Rais na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kutokana na sakata hili ambalo hadi kufikia sasa bado wahajatoa kauli kwa vyombo vya habari ya kuhairishwa kwa hotuba ya Rais.

Kutokana na Rais kushindwa kuhutubia Taifa hapo jana baada ya Taarifa kuwa zimetolewa na Vyombo vya habari Wananchi wapo katika taharuki kubwa kwani hawajui kitu kinachoendelea na kitu kilichompata Rais Wetu hadi kufikia kushindwa kuhutubia Taifa.

Kwasasa Tunaitaka Kurugenzi ya Mawasilino Ikulu kuwajibika kwa kuupotosha Umma juu ya jambo hili nyeti kwa Taifa na aidha tunawataka kutoa tamko kwa vyombo vya habari na kuwaomba radhi wananchi wote waliokesha ucku kucha kusubiri hotuba ya Mpendwa wao Rais na kupelekea wengine kushindwa kwenda kwenye Ibada siku leo.

===============

Sababu 10 kwanini Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Kikwete ni mzigo
Rais alitoa hotuba ambayo imesifiwa na watu wengi jana asubuhi (15 Desemba 2013) kwenye mazishi ya Madiba. Leo saa 5:27 asubuhi (11:27am) ya tarehe 16 Desemba 2013, yaani zaidi ya masaa 24 tangu tukio hilo, eti Ikulu ndio wanatoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu tukio hilo na kuiwekea tarehe ya jana.

Zifuatazo ni sababu 10 kwa nini Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ni mzigo mkubwa kwa Rais Kikwete, serikali na wananchi kwa ujumla. (Sijui nao waitwe na Kamati Kuu ya CCM kuhojiwa?)

1. Kushindwa kutoa habari zinazomhusu Rais kwa muda unaotakiwa

2. Kushindwa kutoa habari zinazomhusu Rais kwa Kiswahili, Kiingereza na kwa mfumo wa electronic media
(yaani redio na TV). Wao daima hutoa taarifa kwa Kiswahili tu, hata kama Rais alikuwa anaongea Kiingereza. Magazeti ya Kiingereza yanapotafsiri taarifa za Ikulu kutoka Kiswahili, maneno hayaendani na maneno halisi aliyoongea Rais (real meaning lost in translation)

3. Kushindwa kutoa hotuba za Rais kwa wakati
(Rais akihutubia leo, hotuba yake hutolewa kesho au kesho kutwa)

4. Kushindwa kuwa na tovuti rasmi ya Ikulu, mpaka leo wanatumia blogspot

5. Kushindwa kuwa na professional email address
(wanatumia ikulucommpress@googlemail.com)

6. Kushindwa kumuweka Rais awe karibu na media
. Hii ni pamoja na kushindwa kumshawishi Rais afanye mikutano ya mara kwa mara na media

7. Kufanya PR blunders mara kwa mara
(kama walivyotoa picha ya Rais akiwa anabembea Jamaica wakati nchi ikikumbwa na matatizo makubwa kama mgao wa umeme)

8. Kushindwa kumsaidia Rais kujenga vizuri taswira yake
(image) kwenye jamii kupitia kwa media

9. Kushindwa kumsaidia Rais kwenye reputation management kwenye social media
(yaani kwenye mitandao kama humu JF, Twitter, Instagram na Facebook)

10. Kutoa taarifa za mambo trivial (madogo madogo) au ya shughuli za kibinafsi za Rais ambazo siyo habari na hazisaidii kumjenga Rais
(eg kutembelea wagonjwa fulani hospitalini au Rais kukutana na Ray C). Siyo kila kitu anachofanya Rais lazima kipelekwe kwa media, hakuna uchujaji wowote unaofanywa kujua matukio gani ni shughuli binafsi za Rais na siyo habari au yanaweza kuleta taswira mbaya.
 
Kwa sisi wananchi na wapenzi makini wa Chama cha mapinduzi tunaona kuna uzembe wa hali ya juu uliofanywa na wasaidizi wa Rais na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kutokana na sakata hili ambalo hadi kufikia sasa bado wahajatoa kauli kwa vyombo vya habari ya kuhairishwa kwa hotuba ya Rais.

naichukia hii statement
 
Haikuwa hotuba nahisi ilikua ni kuwakilisha beti za mipasho ya taarabu karatasi ya beti imepotea ataimba nini. Wamechemka hana jipya la kuwaambia wananchi laana iko juu yake na yeye yuko juu ya laana. Na laana hii haitomwacha kamwe mpaka ifikapo 2015 atakua amechakaa pasipo mfano.
 
...mwenzao hakuwa na cha kusema, wao wamekariri tu kuwa mwisho wa mwezi anahutubia...
 
Kwa nini msiseme wazi tu kuwa mheshimiwa alipagawa na onyo kali{biti?} KUTOKA WASHINGTON?
 
Mr emmy pamoja na kuona uzembe kama huo bado unaendelea kukufagilia chama chako ni chama makini? Kama mpaka kurugenzi ya habari Ikulu inamhujumu rais kuna amani kweli hapo Ikulu?

Yetu macho mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Mr emmy pamoja na kuona uzembe kama huo bado unaendelea kukufagilia chama chako ni chama makini? Kama mpaka kurugenzi ya habari Ikulu inamhujumu rais kuna amani kweli hapo Ikulu?

Yetu macho mkuu.

nadhan ni kejeli za mtoa uzi
 
Last edited by a moderator:
Kwa niaba ya Chama changu makini CCM naomba kuwataka radhi Wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano mliokesha usku kucha kusubiri hotuba ya Mpendwa Rais wetu Mh Jakaya bila mafanikio hivyo naomba mtusamehe kwa uzembe uliofanywa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kwa kutokutoa Tangazo la Mh Kuhairisha kuhutubia Taifa siku ya tararehe 30/06/2012.

Kwa sisi wananchi na wapenzi makini wa Chama cha mapinduzi tunaona kuna uzembe wa hali ya juu uliofanywa na wasaidizi wa Rais na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kutokana na sakata hili ambalo hadi kufikia sasa bado wahajatoa kauli kwa vyombo vya habari ya kuhairishwa kwa hotuba ya Rais.

Kutokana na Rais kushindwa kuhutubia Taifa hapo jana baada ya Taarifa kuwa zimetolewa na Vyombo vya habari Wananchi wapo katika taharuki kubwa kwani hawajui kitu kinachoendelea na kitu kilichompata Rais Wetu hadi kufikia kushindwa kuhutubia Taifa.

Kwasasa Tunaitaka Kurugenzi ya Mawasilino Ikulu kuwajibika kwa kuupotosha Umma juu ya jambo hili nyeti kwa Taifa na aidha tunawataka kutoa tamko kwa vyombo vya habari na kuwaomba radhi wananchi wote waliokesha ucku kucha kusubiri hotuba ya Mpendwa wao Rais na kupelekea wengine kushindwa kwenda kwenye Ibada siku leo.

Wekeni kwenye agenda ya kikao chenu cha Nec
Coz sisi huku uswazi hatuna kumbukumbu sahii kama hiyo kurugenzi imewahi kuwepo nakama ina tija kwa watanzania achilia mbali hiyo hotuba ya raisi
 
Kweli ccm imekwisha kabisa manake mpaka Dhaifu kashindwa kuhutubia taifa kama anavyofanyaga. HATA ANGEHUTUBIA SIWEZI MSIKILIZA NA WALA SIJAWAI KUMSIKILIZA NIKISKIA TU SAUTI NAHAMA CHANEL KWA SABABU ANATIA HASIRA SANA HUYU DHAIFU.
 
Wewe Miss Emmy utuombe msamaha humu JF maana we kwa kimbelembele chako ndo ulileta uzi humu kuwa Dhaifu atahutubia kumbe hamjawasiliana. Au aliahirisha hotuba kuficha udhaifu kwani hata Pinda aliahirisha tamko kuficha udhaifu. Chama dhaifu huzaa serikali dhaifu na rais dhaifu, maskini Tanzania yenu...
 
haina mantiki na haja ya kuhutubia taifa wakati kashindwa kuongoza...akusanye watoto wake pale anatoglu awahutubie italeta maana zaidi kuliko kuhutubia watanzania
 
Ni aibu kwa jk kuahidi vitu ambavyo hawezi kuvifanya jana nimesubiri sana kumsikia dhaifu wangu ataongea nini!
 
Kweli sikuelewa kwa nini! Lakini kwa mara ya kwanza kwa kadri ninavyokumbuka, nilikaa muda mrefu sana nikisubiri Hotuba ya Raisi. Hata ilipofika saa 5.30 usiku nilishauriwa niende kulala lakini bado niliamini pengine ni vyombo vya habari vimechelewa kurusha na ni lazima vingerusha tu. Sijui nilitegemea nini kwenye hotuba ile. Nilipatwa mvuto na hamu ya ajabu, nikasubiri bila kujali usingizi ili mradi nimsikilize Raisi wangu. Lakini Raisi wangu- oh kumbe ni Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeninyima uhondo nilioutegemea! Basi na wajitokeze waseme SAMAHANI- ni neno moja tu na roho yangu itasafishika.
 
Hakujua atoke vipi:
- Kivuli cha Dr. Slaa bado kinamtisha
- Msuli wa Dr. Uli umekuwa mgumu mno kwake
- Dogo Mnyika na kombora lake la "DHAIFU"
- Mfupa wa Obama umeingia mchanga shauri ya deal za Iran - kwa kuandikiwa "Onyo kali" na Afisa wa level ile ni kiashiria kuwa tayari wamemshusha grade sana.
Labda mumtungie nyie biti hapa Jamvini yeye akazishushe tu kwa "wazee wa Dsm"! Walao ktk sanaa hiyo sio DHAIFU hata kidogo!
 
Back
Top Bottom